Kuna haja gani mahakama kutoa hukumu ya kunyongwa hadi kufa kwa mshtakiwa wakati Rais akipelekewa form aisaini ili wanyongwe anakataa?

Hukumu ya kunyongwa hadi kufa inapotolewa na mahakama kwa mshakiwa kama mnavyojua kwa mujibu ya sheria Rais anatakiwa kusaini ili hukumu ya kunyonga itimie ,je!kama mahakam hiyo inatoa hukumu alafu mhusika wa mwisho anakataa sasa kuna haja gani ya mahakama kutoa hukumu hiyo ya kunyongwa,kama ni hivyo ni bora katiba kifungu cha kunyongwa hadi kufa kwa mshtakiwa anapokutwa na kosa hilo kifutwe kutafutwe sheria nyingine ya hukumu inayoendana na kosa.
Kwani wewe kinakuuma nini?
 
Sheria haisemi kwamba Rais atatia saini fomu za wahukumiwa wa kunyongwa (hadi kufa); sheria inasema kwamba baada ya kuhukumiwa adhabu ya kunyongwa, adhabu hiyo itatekelezwa baada ya Rais kutia sahihi yake.

Kwa hiyo hukumu ya adhabu ya kifo haihusiani hata kidogo na uamuzi wa Rais kutia saini au kutofanya hivyo. Muhimu zaidi, sheria haitaji muda ambao Rais anapaswa kusaini utekelezwaji wa adhabu hiyo.
Nini hasa tofauti kati ya kifungo cha maisha jela na kunyongwa hadi kufa??
 
Hukumu ya kunyongwa hadi kufa inapotolewa na mahakama kwa mshakiwa kama mnavyojua kwa mujibu ya sheria Rais anatakiwa kusaini ili hukumu ya kunyonga itimie ,je!kama mahakam hiyo inatoa hukumu alafu mhusika wa mwisho anakataa sasa kuna haja gani ya mahakama kutoa hukumu hiyo ya kunyongwa,kama ni hivyo ni bora katiba kifungu cha kunyongwa hadi kufa kwa mshtakiwa anapokutwa na kosa hilo kifutwe kutafutwe sheria nyingine ya hukumu inayoendana na kosa.
Yawezekana huyo rais Mkatoliki ndio hawanyongi, akija Muislamu hapo atanyonga kama kawa.

Mwinyi alinyonga sana tu.
 
Sasa mbona Rais huwa anatamba jukwaani anasem kuwa ameletewa majina kwenye karatasi asaini ili wakanyongwe na anasisitiza kuwa kakataa na kaelekeza hukumu nyingine hii imekaaje sasa

Sent using Jamii Forums mobile app
Una hoja ya msingi sana kiongozi. Maamuzi yangefanyika ili aidha rais asihusishwe kwenye hiyo adhabu baada ya mahakama kupitisha (hiyo kutia saini ifutwe, ili hukumu ikitoka basi mtu anaenda kunyongwa) au ifutwe kabisa adhabu ya kunyongwa ibakie tuu kifungo cha maisha na kazi ngumu.
 
Hapana mkuu

Design ya hii sheria inampa fursa mkosaji kuwa na Imani kwamba hata kama mahakama itaamuru anyongwe mpaka kufa, bado anayo nafasi ya maamuzi yale kutenguliwa.

Kwa maoni yangu design hii ni nzuri sana! Maana imejengwa kwa msingi wa IMANI /Faith ambayo ndio dhana inayoongoza kila kitu around mwanadamu!

Ima Imani iwe potofu ama kinyume chake bado ni Imani mchango wake kwenye Maisha haumithiliki.
We unafkir wale waliotendwa wakisikia muheshimiwa katoa msamaha kunyongwa watajisikiaje. Maama yawezekana huyu mhalifu ameua mpendwa sana wa aliyetendwa. Hukumu ya kunyongwa ilipotoka at least alifarijika. Then all of the sudden hukumu inakua reversed. Sawa anafungwa maisha lkn si sawa na kunyongwa
 
Nakusoma.
Hili ni shauri tete mno. It's swings both ways. Mungu atupe hekima!
 
Sheria haisemi kwamba Rais atatia saini fomu za wahukumiwa wa kunyongwa (hadi kufa); sheria inasema kwamba baada ya kuhukumiwa adhabu ya kunyongwa, adhabu hiyo itatekelezwa baada ya Rais kutia sahihi yake.

Kwa hiyo hukumu ya adhabu ya kifo haihusiani hata kidogo na uamuzi wa Rais kutia saini au kutofanya hivyo. Muhimu zaidi, sheria haitaji muda ambao Rais anapaswa kusaini utekelezwaji wa adhabu hiyo.
Hawa vijana wa bawacha wao wanachokijua ni lawama tu wala hawana mda wa kupitia vifungu vya sheria kupata ufafanuzi wa kisheria. Linalomjia kichwani mwake analiandika hivyo hivyo anavyofikiria.
 
Hivi hata yule kaka aliyemuua mke wake kwa kumchoma na gunia 2 za mkaa naye Magufuli hapendi anyongwe? Pengine Magu naye haelewi anachotetea.
 
Hivi hata yule kaka aliyemuua mke wake kwa kumchoma na gunia 2 za mkaa naye Magufuli hapendi anyongwe? Pengine Magu naye haelewi anachotetea.
Ukishahukumiwa adhabu ya kifo --- kunyongwa hadi kufa --- hiyo yenyewe tu ni adhabu mbaya zaidi, regardless itatekelezwa lini. Ukiwa kwenye position kama ya Preaident lazima ujue kwa namna fulani una mamlaka uliyopewa na Mungu, which means intelligence, busara na subira ni muhimu sana, Jane!
 
Sheria haisemi kwamba Rais atatia saini fomu za wahukumiwa wa kunyongwa (hadi kufa); sheria inasema kwamba baada ya kuhukumiwa adhabu ya kunyongwa, adhabu hiyo itatekelezwa baada ya Rais kutia sahihi yake.

Kwa hiyo hukumu ya adhabu ya kifo haihusiani hata kidogo na uamuzi wa Rais kutia saini au kutofanya hivyo. Muhimu zaidi, sheria haitaji muda ambao Rais anapaswa kusaini utekelezwaji wa adhabu hiyo.na
Nanukuu "ilitakiwa niwe nimenyonga wafungwa 256 ila nimewasamehe watapewa vifungo vya maisha" mwisho Wa kunukuu.hayo alitamka magufuri mwenyewe jukwaani
 
Kuna mkala niliisoma kwenye Gazeti flan ya mnyongaji maalufu.. Ukweli ni kwamba wananyongwa sema huwa inakuwa kisilisili
 
Mnyogaji maalufu iyo makala niliisoma Gazeti la mtanzania wananyonga sema hawataki kusema tu
 
Back
Top Bottom