Kuna dawa inayotibu kabisa ugonjwa wa kifafa?

Habari zenu WanaJF, Nnateseka sana na hii kitu (KIFAFA) Juzi Nimeanguka hadi nmevunja jino na kutoka Jino kabisa, Nshazunguka Sana Bila Suluhisho kama kuna mwenye kufahamu tiba anijuze Tafadhali
Natanguliza Shukrani
Pole sana .
Pole sana..
 
Punguza choyo mkuu.

Kama Dawa unaijua JARIBU kusaidia na WENZAKO.

Kitendo Cha wewe kufa na MAARIFA yako na UJUZI wako ni Dalili ya choyo hata Mbinguni utahukumiwa kwa Hiyo dhambi.

Weka Dawa hapa wasaidie na WATU wengine wapate kupona.
Nishawasiliana nae inbox
 
Pole sana mkuu, nitachungulia kwenye makabrasha yang dheni nitaiandika hapa hiyo dawa, shida dawa zenyewe za kisukuma, sasa sijui utaielewa miti kweli!?
 
Habari zenu WanaJF, Nnateseka sana na hii kitu (KIFAFA) Juzi Nimeanguka hadi nmevunja jino na kutoka Jino kabisa, Nshazunguka Sana Bila Suluhisho kama kuna mwenye kufahamu tiba anijuze Tafadhali
Natanguliza Shukrani
Pole aisee, ili upate tiba inabidi upate chanzo cha shida yako, unahitaji uchunguzi wa hali ya juu kujua shida kisha ijulikane watafanyaje kukutibu, kwa lugha nyepesi ni kama tuseme kuwe na short ya umeme ktkt ya ukuta sasa ili nyumba ibaki salama.lazima short itafutwe ili tatizo la circuit breaker likae sawa, all the best
 
Mdogo wangu alianza huo ugonjwa akiwa na miaka 10. Alianza kutumia Carbamazepine kwa muda wa miaka mitano mfululizo. Kwa sasa tunashkuru Mungu amekaa miaka 5 bila kutumia dawa na haijawahi kumtokea tena.
 
Pole sana, usikate tamaa. Naamini ipo dawa itakufaa. Angalia ambazo umeshatumia na endelea kuuliza wataalamu ipi ni nzuri zaidi.
 
Habari zenu WanaJF, Nnateseka sana na hii kitu (KIFAFA) Juzi Nimeanguka hadi nmevunja jino na kutoka Jino kabisa, Nshazunguka Sana Bila Suluhisho kama kuna mwenye kufahamu tiba anijuze Tafadhali
Natanguliza Shukrani
Nilisikia kuna jamaa anaitwa Sam yupo Misungwi pale pale mjini stand...ukimuulizia mtu yeyote Sam jamaa wa dawa za asili anakupeleka...kuna mtoto wa shemeji yangu huyo shemeji yangu aliniambia anatibiwa pale na jamaa nasikia ndio kazi zake...amerithi kutoka kwa baba yake...inamaana alianza tangu zamani.

Sema ukienda zungumza nae kwa ustaarabu...usilete ujuaji...nasikia anakiburi pia. Lakini dawa nasikia yupo vizuri.
 
Nikipata namba nitaiweka hapa.
 
Pole sana ndugu, huu ugonjwa ni hatari sana, ukipata nafasi nenda kwenye maombi, amini Mungu atakuponya, hakuna kinachoshindikana kwake.
 
Back
Top Bottom