KWELI Kuna Chemchemi zinazotoa Maji ya moto

Taarifa hii imethibitika kuwa ya kweli baada ya kufanya tathmini ya kina
Source #1
View Source #1
Nimewahi kusikia kuwa kuna chemchemi zinazotoa maji ya moto je, nini chanzo chake? Msaada wadau
1732105578882.jpeg



1732104088453.png

1732104271123.png


 
Tunachokijua
Chemchemi ni mahali ambapo maji yanatoka ardhini. Mara nyingi chemchemi huwa Chanzo cha mto ambao hutiririsha maji yake mpaka baharini au ziwani kama mto ni mkubwa, au ndani ya mto mwingine kama mto ni mdogo. Kumekuwapo na madai kuwa kuna chemchem ambazo hutoa maji ya moto na nyingine hutoa maji ya baridi.

Je, uhalisia wa Madai hayo ni upi?

JamiiCheck imefatilia madai hayo na kubaini kuwa ni kweli kuna Chemchemi zinazotoa maji ya moto. Aidha, Chemchemi zinazotoa maji ya moto ni sifa ya kijiolojia ya asili, hutokana na maji yaliyo ardhini kupashwa joto na "geothermal" (joto la ardhini) na kuibuka juu ya uso wa Dunia.

Katika maeneo yenye asili ya volkano, maji yanaweza kugusana na miamba iliyochemka kwa joto linalotokana na kupashwa na miamba iliyoyeyuka kutokana joto kali chini ya ardhi (magma). Chemchemi zenye maji ya moto katika maeneo yenye volkano hai zinaweza kutoa maji yaliyochemka zaidi, ambayo yanaweza kuwa hatari na kusababisha majeraha au kifo endapo mtu ataoga ndani yake.

hot_spring.jpg

Katika maeneo yasiyo ya volkano joto la miamba huongezeka kadri kina cha kuelekea ardhini kinapoongezeka ambapo hali hiyo hujulikana kama ‘Geothermal Gradient’ Ikiwa maji yataingia kwa kina cha kutosha ndani ya gamba la dunia, yanaweza kufikia miamba yenye joto kali na kusafiri hadi juu ya uso wa ardhi na kuunda chemchem yenye maji ya moto.

Kwa mujibu wa National Park Service Wanaeleza kuwa Chemchemi zinazotoa maji moto zimekuwepo kwa miaka mingi na zimekuwa zikitumiwa na watu kwa shughuli mbalimbali za kijamii na pia kuvutia watalii maeneo mbali mbali duniani.

Chemchemi hizo zipo maeneo yenye volkano hai na tuli ambapo maji hugusana na miamba chini ya ardhi iliyopashwa joto kutokana na magma. Zipo zinazotokea maeneo yasiyo na volkano ambazo hutokea kutokana na maji kuingia kwa kina kirefu chini ya gamba la dunia na kukutana na miamba yenye joto kisha kuibuka juu ya uso wa Dunia yakiwa na joto baada ya kupashwa na miamba.

1024px-Algal_mats_on_hot_pool%2C_Orakei_Korako_1.jpg

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom