Kuna baadhi ya watu wanaharibu lugha yetu

Emc2

JF-Expert Member
Sep 26, 2011
16,808
16,873
Kuna watu kwenye mitandao wanaharibu sana lugha ya kiswahili. Hasahasa kwenye maneno yanayo husu "H" unakuta kwenye kuweka H mtu anaiondoa au anaweka H pasipo takiwa.

Ninaomba tukifunze matumizi ya maneno.
Mfano
Sio akuna ni hakuna
Sio hanakuja ni anakuja
Sio abari ni habari

Vilevile kuhusu nyi na wi
Umoja tunasema wimbo huu hatusemi nyimbo hii.

Wingi wa wimbo ni nyimbo
Kwahiyo zikiwa nyingi tunasema nyimbo hizi.

Tujifunze jamani lugha yetu.
Na ninapendekeza serikali ilete sheria ya kuwachukulia hatua wanaoharibu lugha yetu
 
Wanaoongeza au kupunguza herufi katika maneno wana kitu kinaitwa athari za lugha mama.
Mfano:
Mtu anasema "Hasha hayupo hapa, hameenda mjini"
Kwa usahihi alitakiwa kusema "Asha hayupo hapa, ameenda mjini"
Watu wanaoongeza 'h' sehemu ambapo haikuwepo au kuiondoa ilipo asilimia kubwa wanatoka mkoa mmojawapo kati ya mikoa ya kanda ya ziwa.
Vilevile wapo ambao wanapunguza herufi kwa kuamini kuwa wakifanya hivyo wanaokoa muda wa kuandika.
 
Back
Top Bottom