Kuna baadhi ya vyumba vinatisha wakuu

Kuna baadhi ya vyumba vinatisha wakuu

BabaMorgan

JF-Expert Member
Joined
Dec 18, 2017
Posts
5,111
Reaction score
14,079
Chumba changu cha kwanza kupanga hapa DSM kilikuwa kipo vibaya ila kutokana na hali ikabidi nikizoee licha ya uchakavu wa chumba changu ili kuna baadhi ya vyumba mitaani vilikuwa too much nikakumbuka kuna mshikaji alipata kazi ya kupuliza dawa ya mbu kwenye wilaya fulani alikuwa akiniambia brother kuna watu wanalala sehemu mbaya.

DSM vyumba vingi vilivyopo karibu na mjini ambavyo vinarange kati ya 50000 to 80000 ni majanga aisee kama budget yako ni hiyo na unatafuta chumba mitaa ya karibu na town utawakasirikia madalali bure hakuna chumba cha maana vyumba vidogo vyenye uchakavu wa hali ya juu.

Unajua ukuta wenye fangasi brother? Unajua chumba kisicho na singibodi jirani yako akipiga show au kujadiliana na mke wake vyote unasikia achana na hayo vipi choo cha kulenga ukishusha mzigo maji machafu yanakurukia makalioni wewe acha tu usione masista duu na mabraza men wamependeza ila wanapoishi ni balaa tupu.

Tutafute pesa wakuu tuwe na access ya makazi bora
 
Choo cha kulenga jau sana, unaachia kimba chap unasimama, ukikosea hesabu rojorojo la nnya linakurudia kwenye kalio.
Watu wanaishi kwa tabu sana, ni kudra za Mwenyezi hawapati magonjwa ya mlipuko, na kweli pamba wanazinyuka aisee.
 
Chumba changu cha kwanza kupanga hapa DSM kilikuwa kipo vibaya ila kutokana na hali ikabidi nikizoee licha ya uchakavu wa chumba changu ili kuna baadhi ya vyumba mitaani vilikuwa too much nikakumbuka kuna mshikaji alipata kazi ya kupuliza dawa ya mbu kwenye wilaya fulani alikuwa akiniambia brother kuna watu wanalala sehemu mbaya.

DSM vyumba vingi vilivyopo karibu na mjini ambavyo vinarange kati ya 50000 to 80000 ni majanga aisee kama budget yako ni hiyo na unatafuta chumba mitaa ya karibu na town utawakasirikia madalali bure hakuna chumba cha maana vyumba vidogo vyenye uchakavu wa hali ya juu.

Unajua ukuta wenye fangasi brother? Unajua chumba kisicho na singibodi jirani yako akipiga show au kujadiliana na mke wake vyote unasikia achana na hayo vipi choo cha kulenga ukishusha mzigo maji machafu yanakurukia makalioni wewe acha tu usione masista duu na mabraza men wamependeza ila wanapoishi ni balaa tupu.

Tutafute pesa wakuu tuwe na access ya makazi bora
Bora Bora nikae nje ya mji aisee
 
Unajua chumba kisicho na singibodi jirani yako akipiga show au kujadiliana na mke wake vyote unasikia achana na hayo vipi choo cha kulenga ukishusha mzigo maji machafu yanakurukia makalioni wewe acha tu usione masista duu na mabraza men wamependeza ila wanapoishi ni balaa tupu.
Shukuru Mungu km unalala pazuri, kuna watu wanalala nje kabisa tena chini ya madaraja, kwenye makaravati, kwenye stendi za mabasi vile viti vya abiria sehemu za kuangalia TV ndio sehemu zao za kulala na wanaishi mjini, wengine wanalala chini ya flyover ya Kijazi na Mfugale siku zinasonga, madaraja ya juu yote watu wanalala chini na maisha yanasonga
 
Umenikumbusha mbali Mkuu, nilipokuwa kijana niliwahi kukaa mikocheni kule Uswahilini choo sasa kalikuwa kachumba kadogo halafu kamepachikwa juu ya kilima fulani sisi tukawa tunapaita ghorofani 😄😄 ukiwa unapanda kule kila mtu anajua unaenda kukata gogo maana pako juu kwa hiyo ni rahisi raia kukuona halafu hakukuwa na bati wala nini pako wazi
 
Back
Top Bottom