Habari yenu wakuuu wa jamvi. Naombeni kuuliza hivi kuna mtu alishaomba kazi kupita zoom na akaitwa kwenye Interview katika taasisi au kampuni aliyoomba? maana nishaomba sana ndani ya website hii ila sijawahi kuitwa tofauti na kuomba kwa njia ya post.
Unakuta tangazo la ajira ambayo sifa zote stahiki unazo, kupitia kipengele kilichopo kwenye website hii cha Apply Now unaambatanisha all the requirements lakini hata siku moja sijawahi kujibiwa, is this option exists or what?
Maoni yenu wadau.