Mabibi na mabwana heshima kwenu.
Siku ya 9 leo tangu kampeni zianze, hali ya upepo nchini kwa ujumla tayari inatoa picha kuhusiana na uchaguzi mkuu ujao.
Magufuli alidhani anakubalika kwa 100%. Alidhani wapinzani hawatakuwa na hoja na eti labda wangekuwa wanamfanyia yeye kampeni tu.
La haula! Hali si hivyo.
Upepo umebadilisha ile minya minya yote ya habari. Wanapodhibiti radio na Tvs, ndiyo kwanza inawahamasisha zaidi wananchi kwenda mikutanoni.
Ukweli mchungu ni kuwa pana kundi kubwa la watu wenye chuki na hata hasira na mkuu huyu.
Yote kheri, kwa vile kuishi kwingi ni kuona mengi bila shaka huu utakuwa ni wasaa mzuri kwake kuweza kujitafakari.
Kwanini kama binadamu uchukiwe kiasi tunachokiona? Nini alichowakwaza hivi wamchukiao? Afanye nini kuubadili upepo huu?
Leo tu wazima hakuna ajuaye yajayo. Katangulia mzee Mkapa (rip) mema yake mengi yalisomwa.
Hala hala mtu unaweza somewa maovu kimzaha mzaha hivi hivi.
Ilikuwa vyema kuelezana wakati tungali hai na katika hali ya amani. Pana na kesho na keshokutwa pia.
Mbona kina mzee ruksa, mzee kikwette na wengine wapo wanadunda mtaani na amani zao zote za moyo?
Hali isije kuwa tofauti kwa Mzee baba kwani hao wengine hawakuwahi kuchukiwa kwa kiwango cha wazi hivi.
Misahafu inasema heri ya wapatanishi.
Kwa pamoja tuwasaidie watia nia wetu kukubalika kwa wananchi
Bandugu halipo neno mantashari kama tuhoye (kisukuma), rajunah (Italiano), rejoice (English), yaani maridhiano (kiswahili).
Hala hala kabla ya hatari.
Tahadhari inaponya!