Kumwonyesha mke 'salary slip'

TANZANNIA

JF-Expert Member
Sep 29, 2015
1,047
384
Huwa najiuliza hivi ni haki kumwonyesha mke salary slip na kujua mshahara wako? Mwenye maoni tafadhali anakaribishwa.
 
Huwa najiuliza hivi ni haki kumwonyesha mke salary slip na kujua mshahara wako? Mwenye maoni tafadhali anakaribishwa.


Kitu cha kawaida sana.binafsi waifu anajua mshahara na allowance zote ambazo ni official but pesa nazopiga kwenye mishe na shughuli zingine hizo hata kumi haioni na wala haijui.akiwa na shida ya pesa nitampa but Nina kiasi gani na zilikotoka ni wapi hiyo siyo habari ya yeye kujua kabisa
 
zamani ilikuwa na maana,siku hizi hakuna mwanamke atakayeamini kuwa ndiyo kipato chako! wabongo maisha yetu ni zaidi ya salary slip! tena ukitaka udharaulike muonyeshe yenye digit chache.UTAJUUUUTA
 
Kimsingi mkeo ndiye mtu wa karibu sana na wewe katika maisha yako ya kila siku, kama mmependana kwa dhati ni dhahili hata uaminifu utakuwepo kwa kila upande. Pia hata kama uaminifu hakuna sioni mantiki ya kuficha salary slip au kumficha kipato chako mkeo au mmeo ni kutokujiamini na kutokomaa kifikra, Kwa sababu kwa namna yoyote ile mimi mwenye mshahara ndiye mwenye maamuzi ya mwisho nikwa namna gani kipato changu kitatumika. Ingawa tunaweza jadili au kushauriana nikwa namna gani tutumie huo mshahara, endapo siridhishwi nitakataa ushauri/maoni yako. Hivyo sioni sababu ya kumficha mkeo/mmeo mshahara au kipato chako. Lakini pia tusisahau kujadili ni nini kinasababisha wanandoa wengi kutokupenda kuweka wazi vipato/ mishahara yao kwa wenzi wao. Hapa nitaorodhesha baadhi tu.
1.Baadhi ya wanandoa kuwa na matumizi ya kificho na yasiyo kuwa na tija kwa familia.
2. Baadhi ya wanawake hupenda akabidhiwe mshahara wote na yeye ndiye awe mwamuzi wa kila kitu ndani ya nyumba na hata nauli na mahitaji madogomadogo binafsi mwanaume awe anaomba kutoka kwake.
Hizo ni baadhi tu ya sababu lakini zipo nyingi zaidi ya hizo.
 
Ruksa kujua lakini marufuku kujua salio lako bank M-pesa nakadhalika
 
hatakiwi kujua chochote ye kikubwa nimpatie matumizi yake tu
 
kweli ndoa za siku hizi ni mitetemo ya ardhi sijui kwanini watu wamevamiwa kiasi hichi
yani inafikia hata kufichiana mshahara kweli dosari limeikumba meli na ipo siku itatumbukia baharini
 
Back
Top Bottom