Kumwambia mkewe ukweli sasa kuna mgharimu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kumwambia mkewe ukweli sasa kuna mgharimu

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by maisara, Sep 27, 2012.

 1. m

  maisara Member

  #1
  Sep 27, 2012
  Joined: Sep 7, 2012
  Messages: 93
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mimi ni mfanya kazi katika ofisi moja iliyopo hapa mkoani,jirani na ofisini kwetu kuna ofisi ya serekali kutoka na ushirikiano uliopo wa hizi ofisi nimetokea kuzoeana na baba mmoja wa hiyo ofisi ana cheo kizuri tu ofcin kwake kutokana na ukaribu uliopo hata launch huwa tunaenda wote sehem moja. sasa leo baada ya kupata launch akaniuliza kama nina kazi nyingi ofsin ama tunaweza kuzungumza japo kwa muda wa lisaa limoja nikwamwambia haina shida akaanza kwa kunambia najua uri wako ni mdogo sana kwa mimi kukueleza haya yote lakini nakuomba unisamehe na pamoja na hayo yote unaeza kuwa na ushari ambao unaweza kunipatia, akaanza hivi,,,,

  Nina mke na watoto watano watano, wa kwanza yupo chuo mwaka wa pili, wapili yupo form six ana maliza mwakani.na watatu yupo form three wa nne na watano wapo primary.hii ofisi ninayofanyia kazi hapo awali nilikuwa mtu wa safari sana nimezunguka sana hapa tanzania kikazi hali iliyopelekea kuwa mbali na familia yangu kwa muda mrefu,katika mizunguko hiyo nikawa nikmekumbana na ugonjwa wa ukimwi baada yakujigundua niliumia sana lakini sikuwa na jinsi nashukuru kwa ushauri mzuri na wenye kunipa nguvu niliopatiwa pale kituoni nilipoenda kupima, baada ya kujigundua nikarudi nyumbani na kumweleza mke wangu

  Alilia sana mama watoto wangu na kuona kuwa nilikuwa nilikuwa na mdanganya hadi kuamua kwenda kupima tena zaidi ya mara mbili lkn bado majibu yakaw ni yale yale mke wangu alikuwa akinipenda sana na nililifaham hilo hicho kitu kimuumiza sana ilinichukua mda mrefu sana kumbembeleza na baadae akanielewa nikamwambia naomba ibaki kuwa siri yetu sisi wawili make litakapo toka nje litafika hadi kwa watoto wetu na bado ni wdogo sa na inaweza kuwaathiri na kushindwa kufany avizuri hata shuleni na nimekwambia hi jambo sababu cjapenda kukwambukiza kama nikufa wacha nitangulie mimi we ubaki unaangalia watoto. mke wangu aka nielewa nabaada ya hayo makubaliano nikaenda kununua kitanda kingine nakuweka chumbani kwetu ili kila mtu atumie kitanda chake.

  Mimi tofauti na kufanya kazi hapa lkn pia ni mkulima na mfugaji huko kijiji ni kwetu nina bar na guest house mbili na nina magari matatu moja kwa ajili ya watoto shule moja ni lakwangu na lingine alikuwa akitumia mke wangu so kipato changu ni kizuri sana na mke wangu nilimfungulia duka kubwa sana la nguo na ni maarufu sana hapa mkoani aknitajia jina la duka nikawa nalifaham, sasa baada ya kumweleza mke wangu hali yangu akawa ni mtu anaye jali sana nakula chakula kizuri alichokiandaa yeye na matunda kila siku pale nyumbani kwangu vyakula kama mchele maharage unga huwa natoa kijijini kwetu na vitu vingine huwa kila jumamos nitokapo kazini nanunua kila kitu na bado ninampatia mke wangu hela ya matumizi. ile hali ya kunijali ilidum kwa muda wa wiki tatu na baada ya hapo nikakuta katoa kitanda kimoja chumbani kwetu na kuweka katika chumba kingine pamoja na vitu vyangu vingine

  akaniambia nihamie katika kile chumba nilipomuuliza kwanini akaniambia niameamua tu haoni sababu ya kulala na mimi huku kila mtu anatumia kitanda chake nikamwelewa ili kuepusha maneneo mengi siku tatu baadae akacha kuandaa chakula changu n kumwachia mfanya kazi wa ndani hakutaka tena kufua nguo zangu na akawa nakiburi cha ghafla sana nkakaa naye chini na kumwuliza kulikoni mwenzanu mbona umebadilika sana jibu alilonipa ni kwamba ana kazi nyingi sana na anchoka sana so nisimsumbue na maswali yasiyokuwa na mbele wala nyuma akanyanyuka na kuondoka nakuniacha nimekaa peke yangu a subuhi nilimwita na kumwomba msamaha misamehe mke wangu kwa yaliyotoke jana usiku akanijibu haina shida kazi njema na kuondoka zake nakumbuka hiyo siku alirudi sa sita usiku nalikuwa kazima cm yake mda wote huo kitu ambacho hakikuwahi kutokea kabla

  Nlipomuuliza alinambia alikuwa kwenye kitchen party ya rafikiye na cm yake ilizima charge bas mi sikutaka ugomvi kila mtu akaingia kulala siku mbili tena baadae akaachelewa kurudi na hali iliendelea hivyo hivyo akirudi kwa muda anao taka wakati mwingine hata sa kumi usiku nikimwuliza majibu ni yakiburi na dharau, siku moja nikamkuta na mwanaume ambaye ni kijana mdogo sana kulinganisha na umri wake nikajikaza kiume nakuendelea na mambo yangu nikamfuma tena kama marambili hivi na wanume tofauti tna wadogo wadogo, nikmweleza kwa upole na unyenyekevu na upendo pia mke wangu najua unafanya haya yote ni kwa sbabu siwezi kufanya mapenzi na wewe kwa sasa pamoja nahivyo nakuomba sana utafute tu mwanaume mmoja ambaye ataweza kukumalizia haja zako kuliko unavyo vibadilisha hivi vitotot kama nguo mwishowe na wewe utaambulia maradhi kama haya ya kwangu kitu amabacho sipendi kitokee kwako mke wangu alinyanyuka na kunijibu niache kumfatlia fatilia sana na huku sina uwezo wa kumnanihii huoa ukimwi una wenyewe na wenyewe ndo mimi kisha akaondoka niliumia sana hadi nikatokwa namchozi. kesho yake nikaona gari ya mke wangu imepaki kwenye guest moja hivi akanitajia jina nikaenda hom nikachukua ufunguo wa akiba nikaja nikawasha gari na kuliondoa pale nikaenda kulipaki pale ofsin kwetu wakati wa kutoka hapa nitakuonyesha...

  Baada ya kuchukua lile gari nikamtumia sms nikamwambia kutokana nakushindwa kujiheshm nimemnyang'anya gari atafute usafiri wa kuwa anajirusha na vbwana vyake alinijibu hina shida anajua kinachonisumbua, sikumjibu chochote hiyo siku aliwahi kurudi sa tano tu alikuwa hom sikumwuliza kitu. asubuhi yake msichana wa kazi akaondoka kwenda kwao alikuwa kafiwa na baba yake mdogo na angekaa kwao kwa muda wa wiki mbili so mke wangu hakutoka siku akabaki hom kuangalia mji. mchana wa siku ile nikaamua kupita pale dukani kwake nicho kikuta sikuamini macho yangu duka kubwa liliokuwa na kila kitu limebakiza viatu pear tatu na vinguo vichache vyakuweza hata kutembeza mkononi nikarudi hom mda ulele mchana kwenda kumwuliza ni nini kimetokea dukani alipatwa na shda gani ilompelekea kulimaliza duka na huku huwa ninampa hela za kutosha, nilipofika hom nikakuta mlango upo wazi nikaingia

  ndani na kupitiliza hadi chumbani kwa mke wangu nikamkuta akiwa mtupu kitandani na mwanaume wakirusha roho nilichokiona nilidhani naota nyumbani kwangu mwenyew, chumbani kwangu mke wangu mtupu na mwanaume mwingine nililia sana kama mtoto mdogo huku nimekaa chini yule mwanaume alikimbia akabaki mke wangu amekaa kitandani nikanyanyuka nikamwambia pamoja na yote yalotokea kwangu sidhani kama nina stahili unyama wa aina hii huko nje umechoka umeamua kuleta hadi nyumbani kwangu unatamani sana nife ili urithi mali zangu lakini nakuhakikishia hutapata japo tai yangu nikaondoka tangu siku ile jumatatu hadi leo alhamisi nipo hotelini ni mke wangu tumefunga ndoa tena ya kikatoliki nashindwa pa kuanzia ili niachane naye na katika kipindi chote hicho cjawahi tena kuwa na mwanamke, kurudi nyumbani naona kama nipangoni nipo njia panda na hili swala wazazi wa pande zote mbili hakuna anayefaham nifanyeja mdogo wangu nipo njia panda..

  MPAKA HAPO NILIKUWA NIMELOWA JASHO MWILI WOTE HUKU NASIKIA BARIDI.. NIKAMPA POLE afu nikamwambia arudi nyumbani kwake akaongee na mke wake wakikubaliana wekend waende kijjini kwao wakazungumze na wazazi wao tangia mwanzo mpaka hapo walipofikia wawasikilize wazazi nadhani watawapatia ushauri mzuri sana utakao wajenga, akanambia kwa unyonge nashukuru sana mdogo wangu nitajaribu kufanya hivyo tukawa tumeachana huku mimi siamini baba kama yule aeza kuwa na matatatizo kiasi kile,,,NIMEAMUA KULILETA HUM KAMA NI WW U NGE MSHAURIJE.. Katika maongezi ya huyo baba cjaongeza wala kupunguza kitu labda tu mpangilio.
   
 2. Asulo

  Asulo JF-Expert Member

  #2
  Sep 27, 2012
  Joined: Jun 25, 2012
  Messages: 733
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Ndefu sana..ngoja nikanywe maji nitarudi kuchangia baadae
   
 3. Blaine

  Blaine JF-Expert Member

  #3
  Sep 27, 2012
  Joined: Jan 11, 2012
  Messages: 2,285
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  naomba uweke aya, huu ukuta wa maandishi hausomeki vizuri
   
 4. Zamaulid

  Zamaulid JF-Expert Member

  #4
  Sep 27, 2012
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 16,349
  Likes Received: 6,698
  Trophy Points: 280
  mkuu hii kitu ni ngumu sana!ina hitaji utulivu kuitolea ushauri!!kwa kifupi ngumuuuu!
   
 5. Lateni

  Lateni JF-Expert Member

  #5
  Sep 27, 2012
  Joined: Jun 11, 2012
  Messages: 685
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 45
  Daaah, hii imenisikitisha sana, , ila umeibananisha sana, nitarejea badae .
   
 6. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #6
  Sep 27, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 303
  Trophy Points: 160
  jamani, bila aya tusomeje?
   
 7. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #7
  Sep 27, 2012
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,467
  Trophy Points: 280
  weka aya
   
 8. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #8
  Sep 27, 2012
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,410
  Trophy Points: 280
  Wavivu kama mimi huwa tunazipotezea tu mada kama hizi....
   
 9. platozoom

  platozoom JF-Expert Member

  #9
  Sep 27, 2012
  Joined: Jan 24, 2012
  Messages: 7,325
  Likes Received: 2,317
  Trophy Points: 280
  Kongosho, Blaine, The Boss rudini nimemsaidia kuweka paragraph
   
 10. kalou

  kalou JF-Expert Member

  #10
  Sep 27, 2012
  Joined: Aug 22, 2009
  Messages: 4,369
  Likes Received: 994
  Trophy Points: 280
  Nafikiri uamuzi aliofanya wa kwenda kijijini kuongea na wazee ni mzuri pia afanye utaratibu wa kuongea na huyo mtoto wake wa chuo sababu ni mkubwa anaweza kuelewa.
   
 11. Root

  Root JF-Expert Member

  #11
  Sep 27, 2012
  Joined: Jan 23, 2012
  Messages: 26,281
  Likes Received: 12,993
  Trophy Points: 280
  well nimeisoma nimejifunza mambo yafuatayo.
  Kuwa mwaminifu
  Kupenda kwa dhati kama wangependana hayo yasingewakuta
  Kuishi mbali na familia ni tatizo kubwa.
  Hujafa hujaumbika.
  Tumtegemee Mungu kwa kila kitu
  Ukweli hutuweka huru
   
 12. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #12
  Sep 27, 2012
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,467
  Trophy Points: 280
  Kwani wakiachana itakuwa nini?
   
 13. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #13
  Sep 27, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 303
  Trophy Points: 160
  wakiachana wanachanika.

   
 14. Blaine

  Blaine JF-Expert Member

  #14
  Sep 27, 2012
  Joined: Jan 11, 2012
  Messages: 2,285
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  thx platozoom, its a sad story :crying: indeed. opinions
  1. nampongeza huyo mzee kwa kuwa honest kwa mkewe, big up.
  2. mke ka-react with anger/hate. she thinks mme kapata HIV bcoz ya umal--- so analipa kisasi. she's just frustrated na hakujua how to respond (its traumatic to hear husband ana hiv), laiti angeenda ushauri nasaha asingemtenda mumewe hivyo.
  3. it IS possible kuendelea kuishi pamoja, they need a lot counselling for it to work. nimewahi soma couples hiv+ na hiv- wanaishi together.
  4. the elder children waambiwe ukweli ili waweze kutoa emotional support, the family can make it through this if they remain united
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 15. platozoom

  platozoom JF-Expert Member

  #15
  Sep 27, 2012
  Joined: Jan 24, 2012
  Messages: 7,325
  Likes Received: 2,317
  Trophy Points: 280
  Are we sailing in the same boat? hilo jibu dah!
   
 16. platozoom

  platozoom JF-Expert Member

  #16
  Sep 27, 2012
  Joined: Jan 24, 2012
  Messages: 7,325
  Likes Received: 2,317
  Trophy Points: 280
  Nami nafikiri pia wangepanua wigo wa wanaojua status yao zaidi ya wenyewe wawili..........Hata kumhusisha mtu mmoja wanayemheshimu
   
 17. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #17
  Sep 27, 2012
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,467
  Trophy Points: 280
  Alikosea kumwambia mkewe yeye mwenyewe
  yeye aliambiwa baada ya kupewa ushauri nasaha
  na mkewe alipaswa kwenda kupewa ushauri nasaha kwanza
  kabla ya kuambiwa ukweli uliopo
   
 18. Wi-Fi

  Wi-Fi JF-Expert Member

  #18
  Sep 28, 2012
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 2,070
  Likes Received: 748
  Trophy Points: 280
  Kweli siku za mwisho zimekaribia, ni story ngumu sana kuweka neno!
  Mleta maada, ulikua na tape-recorder nini?
   
 19. Dena Amsi

  Dena Amsi R I P

  #19
  Sep 28, 2012
  Joined: Aug 17, 2010
  Messages: 13,137
  Likes Received: 255
  Trophy Points: 160
  Huyu jamaa anahitaji kumpeleka mkewe kwa ushauri nasaha maana inakuwa too much mpaka alete mwanaume ndani ya nyumba hapa na bana kha! hata kama mwanaume kakosa hii adhabu ni kubwa mno
   
 20. Kaunga

  Kaunga JF-Expert Member

  #20
  Sep 28, 2012
  Joined: Nov 28, 2010
  Messages: 12,591
  Likes Received: 797
  Trophy Points: 280
  Duh hata kama ndio kuchanganyikiwa, huyo mmama kazidi at that age aisee!
   
Loading...