Kumvusha darasa mtoto wa darasa la sita kwenda kidato cha kwanza

Mwanantala

Senior Member
May 13, 2010
130
26
Naombeni mwongozo juu ya mada hii.

Nina mtoto anamaliza darasa la sita ktk shule inayotumia kiingereza. Uwezo wake kimasomo ni mkubwa.

Naomba ushauri wenu.
 
Mwanao anafanya vizuri darasani kwa sababu ameenda hatua kwa hatua bila kuruka ngazi yoyote.

Nia yako ya kumrusha darasa itamfanya afanye vibaya mbeleni kwani kutakuwa na vitu ambavyo hakuvipitia. Shule nyingi za Medium English zilianzisha tabia hiyo ya kuwarusha watoto na sasa wanajutia kitendo hicho na pia shule nyingi za sekondari hazipokei mtoto ambaye hajahitimu darasa la saba.

KUWA MPOLE kwa faida ya mtoto.
 
Umechelewa kidogo wengi wameshafanya mitihani ya kujiunga na form one;kama umeridhika mrushe aingie form one sio shida wengi sana wanafanya hivyo!
 
Sio issue! kwani kuvusha inasaidia nini wakati hajakamilisha mitaala yote unataka akasome Cambridge kama hapo kwa watani zetu jirani?
 
Ni kawaida tu. Cha msingi afaulu mtihani wo wote wa kuingia Form I. Wanacope vizuri tu mpaka Form VI. Guidance is the key.
 
Mimi mdogo wangu kamaliza juzi Eagles Bagamoyo na tulimvusha darasa wakati yupo darasa la sita,haina tatizo ili mradi awe ana uwezo wa kucover yale ambayo hakuyasoma.
 
Kama unaona cheti cha Darasa la Saba sio issue we mvushe tu. I had a same problem like yours, nikaamua kumuacha tu amalizie la saba.
 
mkuu kama anauwezo mzuri darasani mvushe tu haina shida..
Unawezaje kupima uwezo wake..?
Pima uwezo wake kwa kumpeleka kufanya interview ya form one katika shule zile zenye pass mark kubwa na kama akifanikiwa kupita basi anauwezo mkubwa..
Na kwanini nasema kuvushwa haina shida..?
-Nasema hivyo sabab mimi pia nilivushwa kutoka darasa la 6 hadi form 1 na siku face shida yeyote ile kimasomo.
-kusoma ukiwa na umri mdogo ni nzuri sana na imenisaidia sana cha muhimu tu mwanao mjengee confidence,hii imenisaidia sana na sasa nipo nasoma udaktari mwaka wa kwanza nikiwa na miaka 19
 
Kawaida we vusha tu mi mtoto wa ba ndogo alivushawanae wa2 mmoja la 6 na mwingine la 5, wa drs la tano alipata nafasi loyola,wa drs la sta alipata nafasi shaban robart,hv sasa mmoja anamaliza dgree yake st joseph comptr eng,na mwingine anamalizia adv dpl chuo cha bandari.
 
Mbona haina shida hata wakwangu nimefanya hivyo mradi anamiaka zaidi ya 10 na amefaulu vyema mtihani wa kuingia form one kwenye shule nzuri usimpeleke shule ni shule.Mimi mwenyewe nilirushwa darasa miaka hiyo ya themanini na nilisoma vizuri tu mpaka chuo bila kukwama na nilifanya vizuri kuliko wale waliofanya madarasa yote.
 
Naombeni mwongozo juu ya mada hii. Nina mtoto anamaliza darasa la sita ktk shule inayotumia kiingereza. Uwezo wake kimasomo ni mkubwa. Naomba ushauri wenu.

nna mdogo yuko first year ud, alirushwa la sita na kwenda form one. Huko sekondary alisail vizuri tu mpaka kufika chuo. Lakini inahitaji na uwezo binafsi pia, asiwe mtu wa kukaririshwa majibu
 
Mheshimiwa wa visiwa vya pemba na zimbabwe akiingia kwenye anga zako, dogo atarudishwa akamalizie grd.7 na hiyo shule iliyompokea ataifungia 'on the spot' try 2be smart!
 
Naombeni mwongozo juu ya mada hii. Nina mtoto anamaliza darasa la sita ktk shule inayotumia kiingereza. Uwezo wake kimasomo ni mkubwa. Naomba ushauri wenu.

Ndugu, kuna mifumo miwili ya elimu hapa tanzania kwa shule za msingi

NECTA primary ni miaka 7 (mfano wa shule ni hizi zetu uswazi) , na cambridge primary ni miaka 6 (mfano wa shule ni HOPAC, na zinazoishia na majina academy au international)

hiyo ya kuruka darasa huwa wanfanya gimicks tu kwa ajili ya kuvutia biashara ,

kama amemaliza grade six katika shule yenye mfumo wa cambridge anakwenda tu form one bila matatizo na ni vyema sasa ukamrudisha katika shule zenye mfumo wa NECTA

Mfano nitakupa katika shule ya esacs, amabayo primary inaishia grade six, watoto wa grade six hufanya mitihani ya necta ya darasa la saba, na kumaliza shule ya msingi. kwa wengine huongeza term/mwaka wa grade 7 ili wapate tu hela lakini inakuwa haina maana hata kidogo.
 
Siku za karibuni kumekuwa na madai ya vyeti vya darasa la saba kwa baadhi ya waajiri.
Hii itakuwaje kwa ambao walirushwa?
 
Mdogo wangu pamoja na madogo wa kitaa hawataki kusoma std 7 wana ruka 4m 1 ndo fashion huku ila kwa mdogo wangu kamaliza tusime anafanya vizuri secondary ila math awezi
 
Hao mnao warusharusha tambueni kuwa huko mbeleni mnawanyima fursa ya kulitumikia taifa letu kwenye sehemu nyeti kama JWTZ na TISS make kule wanademand leaving certificates za kuanzia primary mpaka candidate alipoishia. Sasa kazi kwenu nimewapa angalizo tu.
 
Back
Top Bottom