Kumuita Mke/Mpenzi Mama ni sahihi?

Mambo mengine bhana..

Mimi namuita mama, ndio, kwasababu ni mama wa familia yangu. Kila mtu nyumbani kwangu anamuita mama, watoto, dada wa kazi.

Sasa me nikimuita mama ndo inamaanisha amechukua nafasi ya mama yangu mzazi au...!!!? Tuache kucomplicate mambo.

By the way, tunawaita mama watu wengi sana duniani. Kwa mimi, mathalan, mtu mzima yeyote wa level ya umama huwa namita ivo.

Mfano:
Mama karibu kiti. Mama karibu nikusikilize. Mama naomba nipite. Mama umebeba mtoto vibaya, anaumia shingo. Mama huku unakopita hakuna njia. n.k

Sioni tatizo, labda tuamue leo kwa pamoja kuliita tatizo.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom