Kumuamini Mungu lazima uwe na dini za wageni?

Kumuamini Mungu lazima uwe na dini za wageni?

Habari za leo ndugu jamaa na marafiki.

Naomba ufahamu zaidi kwamba

Unafikiri utaratibu wa kuabudu waliotuleta wakoloni ni sahihi?

Ushajiuliza kama wasingetutawala ingekuaje?

Ushajiuliza kama wangetutawala wachina au wahindi tungekuwa Wabudha au Wakrishna?

Waafrka wanatakiwa kumwamini Mungu kwa utaratibu upi? Wa Waarabu au Wazungu?

Mwisho kumuamini Mungu lazima uwe na dini za wageni?

Naomba kuwasiliana.

Sent from my TECNO Camon CX using JamiiForums mobile app
Inategemea Mungu yupi unaemsema
 
Hili huwezi kulithibitisha na utakuwa muongo huwezi kuamini uwepo wa Mola nje ya dini.

Hili nakupa kazi ulithibitishe,ukiweza naacha kujadilo hili. Jambo linalowezekana ni kuwa kila kiumbe aliumbwa na hali ya kumkubali Mola pindi akiletewa habari na kukiri ya kuwa Mola ndiyo muumba na ndito muendeshaji wa huu ulimwengu.
Jurjani inaonekana umekuja kubisha hapa! Ni kipi kumekupatia ithibati ya kuwa ni muongo?

Unasema "..huwezi kuamini uwepo wa Mola nje ya dini." Na inasomeka unajiamini katika haya uliyoandika. Je ni nikasema ".. Unaweza kuamini uwepo wa Mola nje ya dini." Ni nani sahihi baina yetu?
 
Sahihi ni mimi,ndiyo maana nikakuuliza uonyeshe uwezekano wa hili. Lakini nikaolkuonyesha ambalo lipo ni kuwa unaweza kupewa habari za Mola tokakl kwenye dini ukazikubali sababu hili lipo na Allah ameliweka kwa waja wake wote wanapozaliwa.

Kilichonifanya niseme hili ya kuwa wewe ni muongo ni hicho ulichokiandika. Ingekuwa unayo yasema Mola wetu asingeleta mitume na manabii. Ushawahi kujiuliza kwanini walikuwepo mitume na manabii ?
 
Mimi dini yangu ya kiislam haijaletwa na Mzungu Wala Muarabu, Ni dini ya Mwenyezi Mungu, nimetambua Hilo baada ya kuisoma Quraan, yaliyomo humo hakuna binaadam anaeweza kuyaandika na kuyaweka humo.
Tehe tehe Muhammad masalia
 
Mbona umejitwisha haki Bw. Jurjani. Mitume na manabii? Mitume na manabii wapi hao maana siwafahamu na siwatambui. Wait! huwa nasikia hadithi za kale na ngano zikisema suala la mitume na manabii na kudai walifikia mwisho inastaajabisha hakika.
 
Safi kabisa nipo hapa kukuthibitishia ya kuwa wewe ni muongo kwa kauli na matendo yaani unachokisema huishi nacho na hakipo.

Unaweza kuniambia ni hadithi zipi hizo na ngano zipi,na umejuaje kama hizo ni hadithi na ngano. Ukianza kwa kunipa maana ya Hadithi na maana ya ngano utakuwa umefanya la maana sana.

Ila hilo weka akilini,wenzako hasa huyu Kiranga huwa anadai ya kuwa habari za dini ni hadithi tu za kutungwa,ukimuomba ushahidi anakimbia,yaani anaandika mambo asiyo kuwa na ujuzi nayo,sasa huwa nawaambia hivi,hata kama nyinyi si watu wa elimu na si wasomi wa mambo haya,basi mjitahidi sana kuyapa stahiki zake maneno,yaani mjue maana ya maneno fulani kabla hamjayatumia. Hili swali bila shaka litakushinda.

Subiri uone.
 
Habari za leo ndugu jamaa na marafiki.

Naomba ufahamu zaidi kwamba

Unafikiri utaratibu wa kuabudu waliotuleta wakoloni ni sahihi?

Ushajiuliza kama wasingetutawala ingekuaje?

Ushajiuliza kama wangetutawala wachina au wahindi tungekuwa Wabudha au Wakrishna?

Waafrka wanatakiwa kumwamini Mungu kwa utaratibu upi? Wa Waarabu au Wazungu?

Mwisho kumuamini Mungu lazima uwe na dini za wageni?

Naomba kuwasiliana.

Sent from my TECNO Camon CX using JamiiForums mobile app
Kuna miungu mingine ambayo ni pamoja na mizimu inayoabudiwa na waafrika, halafu kuna Mungu Mkuu ambaye ni Mungu wa taifa la Israeli. Sasa huyo Mungu Mkuu wa Israeli ndo alihubiriwa ulaya hasa kule rumi na mtume Paulo na hao warumi wakaja kuhubiri huku afrika na kwingineko duniani kuhusu huyo Mungu Mkuu ambaye anajulikana pia kama Mungu wa Israeli...hivyo unaweza kumwabudu huyo Mungu Mkuu bila kupitia dini yoyote na hata bila kuwa mfuasi wa dini ya kiyahudi kama wakristo wanavyofanya....
 
Mimi dini yangu ya kiislam haijaletwa na Mzungu Wala Muarabu, Ni dini ya Mwenyezi Mungu, nimetambua Hilo baada ya kuisoma Quraan, yaliyomo humo hakuna binaadam anaeweza kuyaandika na kuyaweka humo.
Basi ni sawa sawa na ukristo kama huujui ni bora ukae kimya na ndio maana wanasomea mbaka digrii ya ukristo vipo vyuo
 
Nitakujibu hivi,Ingawa sijajua Elimu yako ya Dini iko vipi,Mungu alimuumba mwanadamu kwa ajili ya lengo moja tu,kumuabudu,hiyo ndiyo tofauti kati ya Wanadamu na Wanyama. Sasa wewe mleta maada ni wajibu wako kumuabudi
Linapokuja swali la dini zililetwa na waarabu sijui wazungu,iko hivi naamini utakuwa na elimu ya darasani.Tunaposema zamani jamii haikuwa imesambaa kama unavyoona leo watu walikuwa wanakaa sehemu moja au eneo moja tuseme ambalo linajumuisha Shamu,palestina mpaka Misri hiyo ni miji ya zamani sana ukisoma historia za Dini. Pindi mwanadamu anapomkosea Mwenyezi Mungu kwa kumkubusha amekuwa akiwaletea mitume,nazani hoja yako hapo ndipo inapoanzia
Wale wazazi wetu walikuwa wanaabudi kisichokuwa Mwenyezi Mungu kabla ya kuwafikia Mitume hawana dhambi kwani hawakulijua hilo,
Lakini wewe mwenzangu ambeya Dini ipo mlangoni kwako lakini bado unaulizwa swali kama hilo usipomfuata Mwenyezi Mungu kifo kikakukuta basi wewe ni moja kwa moja motoni.
Kuhusu Dini Mwenyezi Mungu ana dini moja tu,hata mitume wake hawakutofautiana bali aliyekuja alianzia pale aipoishia Mwingine. Mfano Ibrahimu hakusema Nuhu hafai wala Yesu hakusema Musa hafaina hata Mtume Muhammad hakusema Yesu hafai. Sasa Dini ya kweli ni ile amabyo haibagui mitume wa Mwenyezi Mungu ambayo ni Uisilamu
Umeanza vizuri ila kumalizia ndio umechemka hujui ukristo nadhani umetetea din yako uislam tu
 
Mtoto akizaliwa kwenye Dini ya wazazi wake hana dhambi,na hata akifa anaenda peponi,Zambi anaanza kuhesabiwa pale anapobalehe sasa ndipo penye uamuzi aendelee kufuata Dini ya wazazi wake,au aachane nayo afuate Dini ya ya kweli. Ndiyo maana sisi wengine tumezaliwa kwenye ukristo tukapata sakrament zote lakini baada ya kujitambua tumejikabidhisha kwa Allah
Acha kujidanganisha eti umezaliwa kwenye ukristo na je waliozaliwa na uislam wakaamia ukristo utasemaje??!
 
Miguu ya mja wa Allah hautoondoka kutoka kwenye sehemu yake Siku ya kiama,mpaka aulizwe kuhusu uhai wake,vipi aliutumia;na kuhusu elimu ya Dini,vipi ameitekeleza;na kuhusu mali yake,wapi aliichuma
 
Kalibu kwenye Uislamu,achana na mambo ya kuabudu Miungu na Masanamu. Mungu ni mmoja tu hakuzaa wala kuzaliwa
 
Mkuu mimi naamini katika mizimu na kuzuru makaburi. Japo naamini murungu yupo sio kupiga makelele a kuvaa kama watu wa nje.
 
Mimi dini yangu ya kiislam haijaletwa na Mzungu Wala Muarabu, Ni dini ya Mwenyezi Mungu, nimetambua Hilo baada ya kuisoma Quraan, yaliyomo humo hakuna binaadam anaeweza kuyaandika na kuyaweka humo.
Quran iliandikwa na nani?? Tuanzie hapo
 
Nitakujibu hivi,Ingawa sijajua Elimu yako ya Dini iko vipi,Mungu alimuumba mwanadamu kwa ajili ya lengo moja tu,kumuabudu,hiyo ndiyo tofauti kati ya Wanadamu na Wanyama. Sasa wewe mleta maada ni wajibu wako kumuabudi
Linapokuja swali la dini zililetwa na waarabu sijui wazungu,iko hivi naamini utakuwa na elimu ya darasani.Tunaposema zamani jamii haikuwa imesambaa kama unavyoona leo watu walikuwa wanakaa sehemu moja au eneo moja tuseme ambalo linajumuisha Shamu,palestina mpaka Misri hiyo ni miji ya zamani sana ukisoma historia za Dini. Pindi mwanadamu anapomkosea Mwenyezi Mungu kwa kumkubusha amekuwa akiwaletea mitume,nazani hoja yako hapo ndipo inapoanzia
Wale wazazi wetu walikuwa wanaabudi kisichokuwa Mwenyezi Mungu kabla ya kuwafikia Mitume hawana dhambi kwani hawakulijua hilo,
Lakini wewe mwenzangu ambeya Dini ipo mlangoni kwako lakini bado unaulizwa swali kama hilo usipomfuata Mwenyezi Mungu kifo kikakukuta basi wewe ni moja kwa moja motoni.
Kuhusu Dini Mwenyezi Mungu ana dini moja tu,hata mitume wake hawakutofautiana bali aliyekuja alianzia pale aipoishia Mwingine. Mfano Ibrahimu hakusema Nuhu hafai wala Yesu hakusema Musa hafaina hata Mtume Muhammad hakusema Yesu hafai. Sasa Dini ya kweli ni ile amabyo haibagui mitume wa Mwenyezi Mungu ambayo ni Uisilamu
Uneandika upupu katika uzi wa great thinkers. Thinking is not beleiving. Wewe umeandika beleaving hapa
 
Kwa kukusaidia ndugu yangu mtafute padri ukamuulize hicho ulichokiandika,halafu mtafute mchungaji muulize swali hilohilo,kamalizie Kwa kumuuliza Shekhe.Utapima majibu yapi ya kweli
 
Sijajua umekusudia nini au Mwenzangu unaujuzi zaidi ungenifundisha baadala ya kunilaumu
 
Dini nini? Ni kuwapa pole wagonjwa,kusaidia maskini,Kuwajali yatima na wajane kuwapenda jirani zako kama nafsi yako hii ndio dini Safi. MUNGU NI NANI? MUNGU NI ROHO NA WAMWABUDUO YAPASA WAABUDU KATIKA Roho na kweli. Roho ni nini Roho ni Dhamiri na nia. Kuna dhamiri ngapi? Ziko mbili dhamiri safi na dhamiri mbaya hivyo hivyo kuna nia mbaya na nia nzuri. Hivo basi ukiwa unadhamiria mema na kunia mema tayari wewe ni mcha MUNGU. Mfano umedhamiria kutozini,kutonungunika,kulaumu,kutochukia ,kutoiba na ukafanikiwa kutaacha mambo hayo hakika utakuwa na MUNGU na utaisikia sauti yako ila kama wewe ni mzinzi kama mimi jua uko mbali na MUNGU TU hata kama unaingia kanisani kila Siku maana MUNGU hachangamani na dhambi hata babu zetu na bibi zetu wakale wanajua ndio maana walijua kabisa kwamba ili ukweli udhihirike lazima uape kwa MJNGU ambae ni kweli na hapendi uongo wala hajawahi kuwa baba wa uongo kama shetani anavotudanganya na wanasiasa
 
Back
Top Bottom