Suley2019
JF-Expert Member
- Oct 7, 2019
- 1,817
- 4,568
Jana tarehe 29/06/2023 Rais Samia amemteua Balozi Omary Ramadhani Mapuri kuwa Mjumbe wa NEC wakati kiongozi huyo alishawahi kushika nafasi ya Katibu Uenezi ndani ya CCM. Nimepita mtandaoni nikaona malalamiko ya wadau kuwa katiba imevunjwa. Hivyo katika uzi huu nimeona nilete hivyo vifungu tuvisome pamoja.
Ibara ndogo ya (14),
Itakuwa ni marufuku kwa watu wanaohusika na uchaguzi kujiunga na chama chochote cha siasa, isipokuwa tu kwamba kila mmoja wao atakuwa na haki ya kupiga kura iliyotajwa katika ibara ya 5 ya Katiba hii.
Ibara ndogo ya (15),
Kwa madhumuni ya ibara ndogo ya (14) watu wanaohusika na uchaguzi ni-
(a) Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi,
(b) Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi,
(c) Wajumbe wote wa Tume ya Uchaguzi,
(d) Mkurugenzi wa Uchaguzi pamoja na watumishi wote wa Tume ya Uchaguzi,
(e) Wasimamizi wote wa Uchaguzi katika miji na wilaya zote na Majimbo ya Uchaguzi