Kumsoma mtu alivyo na kunuia

Kumsoma mtu alivyo na kunuia

Mama Sabrina

JF-Expert Member
Joined
Jul 30, 2016
Posts
16,607
Reaction score
27,607
1: Hivi inakuwaje unakutana na mtu mnaelewana kabisa na unaona huyu mtapatana vyema,,kuna vitu mnakua vinafanana
Kuna mwingine ukionana nae tu hutaki tena kumsikia ,,unaona anakuboa tu
Nieleweke inatokea kwenye jamii zetu kuna mtu au watu wao watakuchangamkia lakin wewe hujisikii kabisa hata kuwa nao karibu
Wanaita damu kupatana na kutopatana
Mfano mim nikikaa na mtu awe mdada au mkaka,najua hapa sina mtu kabisa,,au ukimuangalia usoni mtu unaona kama anakuwazia mabaya tu
Mim mtu akiwa hanipendi najua tu huyu haziivi kabisa naepuka nakaa mbali na huyo mtu
Je ushawah msoma mtu ukamuelewa alivyo na ikawa kweli,uso wa mtu una mambo mengi sana

2: je inakuwaje mtu anakuudhi halaf unasema kabisa kwa kunuia yaan wewe ukijapata kazi au ukifanikiwa hivi unishike makalio,,na inakuwa kweli aisee huyo mtu hapati kazi wala nini na hujamroga wala nin umejisemea tu na inakuwa kweli

Kuna mtu nilishawa nuia maneno mabaya kwake na kweli inatokea nishajitahidi kumuombea yaishe lakin naona bado,,ila naona kama hajabadilika hivi aliniudhi sana nilimuambia kua machozi yangu hayaendi bure ,,lakin imefikia hatua nishamsamehe nahitaji afanikiwe na simuhitaji kabisa,,lakin mambo yake yashagoma wenzie wanafanikiwa tu
Basi nawataki jioni njema
 
Neno la Mungu halitufundishi hivyo. Waombeeni adui zenu, wapendeni adui zenu. Wabarikini wanaowaudhi.

Unaonekana umetawaliwa na negative thoughts ktk subconscious mind yko. It takes efforts ku inject positive thoughts kwa mind yko kuliko negative thoughts...

You must read and practice the world of God!
 
Badilika, sio sifa kuwatakia wenzio mabaya huku wewe ukila tamu ya maisha. Hivi, una uhakika hayatakurudia?
Badilika Best
 
Duh! Nahisi nimesoma uzi wa jini Maimuna leo, nilikuwa nasikiaga story tu
 
Mi hakuna baya mtu alishawahi kunitamkia likanipata, kutoa sadaka mbalimbali kwa watu wenye uhitaji ni ufunguo wa mitego yote ya kibinadamu na vyote vya gizani.
 
Back
Top Bottom