Cereal Killer
Senior Member
- Aug 17, 2015
- 130
- 55
Hatuishi kwa siasa peke yake. Kila kitu siasa, tumechoka sasa. Hili ni jukwaa la mapenzi, mahusiano na urafiki. Hayo mambo ya vichinjio, sijui mkoloni mweusi, sijui nini peleka jukwaa la siasa.
Halafu hilo jina lako, eti Cereal Killer, hebu jaribu kulicheki vizuri. Kuna kitu hakipo sawa hapo.Tulia dawa ikuingie wewe
Halafu hilo jina lako, eti Cereal Killer, hebu jaribu kulicheki vizuri. Kuna kitu hakipo sawa hapo.
Habar wakuu, kuna kitu leo kimenishitua kidogo kuna binti mmoja tuko naye mtaa mmoja na tunaabudu kanisa moja kuonana kwetu huwa ni kanisan japo tulikuwa tunaangaliana tu hakuna mtu aliyekuwa anaenda kumpa salamu mwezake,lakin sura zetu wote zilionesha shauku ya kila mtu kutaka kuongea na mwezake sasa jumapil iliyopita tuliweza kuongozana wote kurud nyumban lakn tulikuwa watatu na kila mmoja alifurah yaan ndo ilikuwa siku ya 1 kuongea naye,pia leo jumapil baad ya ibada tulikuwa tunatakiwa twende kweny ibada nyngne tofauti na kanisa letu akaniulza utaenda nikamjibu ndio nikamuomb anipitie home akakubali, kwel badae akapita na tuanza kwenda huku tukioneshara ishara za mapenzi, nikaona nimtongoze akaniambia nimpe wiki mbil ndo atanijbu, sasa cha ajabu wakat tunarud home nikajarbu kumbembeleza apunguze hzo wiki mbil huku nikijarbu kumshka mkono akawa mkali ghafla akasema hapendwi kushikwa,wanajamvi naomb ushaur, maan hap mwanzo wakat kaja kunipitia tulikaa ziro distance na nilikuwa namshika mkono kawaida.
Nenda taratibu na mlokole wawatu
Mkuu umenena yote,huyu dogo aache papara bana....Hahaha..lol..Nimecheka mbavu sinaπ
Ni kweli kabisa huyu bwana anachotakiwa ni kwenda nae asti asti tu huyo mlokole wa watu. Naamini 'mlokole' kishalainika lakini bwana mdogo nafikiri ana 'kiraru' cha siku nyingi hivyo hana subira. Inaelekea yuko excited sana na pia 'aggressive' kidogo hivi. Sasa yule mwenzie amekuwa un comfortable kidogo.
Anatakiwa aonyeshe u-gentleman fulani hivi na mlokole atafunguka mwenyewe mpaka siku na saa ya kumletea 'mzigo'. Na tena basi itakuwa kabla ya hata hizo wiki mbili alizozisemaπ. Kijana yeye anachotakiwa ni kuongeza kasi ya kuimba mashairi tu ya "I love you babe"π
Nawajua watoto wa kilokole 'uchepe' wao ni wa chini chini na hivyo sitarajii kama mtoto wa kilokole utatembea nae mitaani umemshika mkono na kuonyesha affections tena barabarani...Sasa mkikutana na wazee wake? ama wazee wa kanisa je? au ndugu? au watu anaowaheshimu huko barabarani si ataonekana ameshaanza ku lost tu?
Hivyo kijana tulizana.... 'zabibu ni zako hizo lakini wacha papara"π
Goodluck!
Hizo nguvu za kumshika mkono zihamishie katika kukishika kichinjio chako vizuri ili oct 25 tumchinje mkoloni wetu mweusi
Habari wakuu,
Kuna kitu leo kimenishitua kidogo kuna binti mmoja tuko naye mtaa mmoja na tunaabudu Kanisa moja kuonana kwetu huwa ni kanisani japo tulikuwa tunaangaliana tu hakuna mtu aliyekuwa anaenda kumpa salam mwezake,lakini sura zetu wote zilionesha shauku ya kila mtu kutaka kuongea na mwezake.
Sasa jumapili iliyopita tuliweza kuongozana wote kurudi nyumbani lakini tulikuwa watatu na kila mmoja alifurahi yaani ndo ilikuwa siku ya 1 kuongea naye,pia leo jumapili baada ya ibada tulikuwa tunatakiwa twende kwenye ibada nyingine tofauti na Kanisa letu akaniuliza utaenda nikamjibu ndio nikamuomba anipitie home akakubali.
Kweli badae akapita na tuanza kwenda huku tukioneshara ishara za mapenzi, nikaona nimtongoze akaniambia nimpe wiki mbili ndo atanijbu, sasa cha ajabu wakati tunarudi home nikajaribu kumbembeleza apunguze hizo wiki mbili huku nikijaribu kumshika mkono akawa mkali ghafla akasema hapendwi kushikwa.
Wanajamvi naomba ushauri, maana hapa mwanzo wakati kaja kunipitia tulikaa ziro distance na nilikuwa namshika mkono kawaida.