Bernard bakari
JF-Expert Member
- Mar 30, 2016
- 407
- 780
Kuna maisha yamejengeka katika jamii kuwa mwanamke ndiye anatakiwa afanye kazi zote za ndani kama vile kufua, kupika, kuosha vyombo, kufanya usafi na kazi zingine nyingi za kifamilia.
Kuna wakati unaona kabisa mwanamke anachoka yeye apige deki nyumba, akimaliza akapike chai, akafue nguo akimaliza achote maji aanze kuandaa chakula cha mchana mwanaume amekaa tu anasubiri chai kisha anashinda na Tv anasubiri chakula cha mchana kisha anaangalia mpira anasubiri chakula cha usiku. Maisha hayo yamepitwa na wakati wanaume tubadilike Mwanamke si mtumwa.
Mwanamke anatakiwa kusaidiwa kazi wakati yeye anapiga deki mwanaume anza kujaza maji kwenye vyombo kama nyumba yako ina mfumo wa maji kila sehemu ni vyema ukaanza kuosha vyombo akimaliza wakati anapika chai chukua nguo anza kufua atakuja kukusaidia chai ikiwa tayari kisha mnamaliza kwa mda mfupi mnakunywa chai mtajikuta kazi zinaisha mapema naye anapata mda wa kupumzika na kuandaa chakula cha mchana pole pole kwa furaha.
Maisha ya sasa ni ya kusaidiana tusiwafanye wake zetu kama watumwa. Mwanamke anayohaki ya kupumzika na anastahili kusaidiwa kazi. Niwatakie jumatatu njema