kumradhi jamani!!

Chabo

JF-Expert Member
Jul 20, 2011
990
1,000
habari za saa hii wadau!,
naomba kujua ni mahali gani pazuri pa kwenda kufurahi na famili dar es salaam

nawasilisha.
 

pilau

JF-Expert Member
Aug 16, 2012
1,591
1,500
habari za saa hii wadau!, naomba kujua ni mahali gani pazuri pa kwenda kufurahi na famili dar es salaam nawasilisha.
Nduhu, YAH: MAOMBI YA KUTAFUNA MPUNGA WA X-MAS na nyuu YEA ...Tafadhali husika na somo la hapo mwanzo....Mimi ni kijana ,wenye umri wa kutosha ni M - TZ halisi, naomba kukaribishwa kwenye sikukuu ya X- Mas na Nyuu Yea... naamini nitatafuna vizuri ubweche pasipo kumwagamwaga hovyo chini... kwani nina uzoefu wa kuatosha na nina HOTPOT yangu maalumu kwa ajili vitakavyo baki napia sina aleji ya chakula chochote... nimeona niwahi kutuma maombi kwa sababu cku hiyo naweza nisiwe na vocha kwenye cmu... maana nimetuma maombi sehemu nyingi sana... ahsante ..... wako mtiifu mlaji mzuri.......
 
  • Thanks
Reactions: PhD

PSM

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
542
0
You can't be serious?yaani mpaka sehemu hizo nikulizia jf,sisi Kwani tunajua kipato chako hadi tujue tukuelekeze?kwel jf sasa imevamiwa kma Huna issue jamani una soma tu na kuchangia za wenzio Kah!
 

MLERAI

JF-Expert Member
Apr 4, 2012
669
475
Nenda uwanja wa fisi ukafanye utalii wa ndani utaona jinsi machangudoa wanavyoopolewa
 

Father of All

JF-Expert Member
Feb 26, 2012
4,695
2,000
Ingawa kuomba ushauri na msaada ni jambo jema, laweza kuwa baya iwapo watu wataamua kutofikiri wala kuwajibika ilmradi wataandika thread wapate wanachotaka. Kwa ufupi ni kwamba fanya utafiti wako utapata hiyo sehemu. Kwenda kufurahi na familia ni tegemezi. Wapo wanaopenda kwenda sehemu kuogelea, kushangaa shangaa maghorofa, kuzurura, kulala tu na mengine mengi. Hivyo angalia category yako ufanye utafiti.
habari za saa hii wadau!,
naomba kujua ni mahali gani pazuri pa kwenda kufurahi na famili dar es salaam

nawasilisha.
 

hippocratessocrates

JF-Expert Member
Jul 1, 2012
3,601
2,000
Sasa mkuu Chabo, unajua ungeshirikisha kwanza utafiti kidogo na akili yako kabla ya kuja hapa kuuliza, ni kweli JF ni kila kitu(encompasses all) lakini haimaanishi kuuuliza kila kitu(and dont say sasa, niulize/tuulize nini sina orodha ya vitu vinavyopaswa kuuliza JF ila FIKIRI)...na ndio maana ulianza na "kumradhi jamani".

Kufurahi na familia, inategemea sasa
-Familia ya ukubwa gani(hasa umri wa watoto/nduguzo)
- pesa iliyopo,
- wanapendelea nini,
- katika muda gani.

Ni kweli, tunatofautiana wengine hupenda mjini(ghorofa), "madaraja yanayopita juu" mpeleke Manzese darajani tu pale unakuwa umemaliza kila kitu(kama enzi zileeee)-joking.

Sasa kuna sehemu nyingi, fukwe(beach), hoteli(hotel), sehemu za sanaa, sehemu za kutunza wanyama(Zoo), kumbi za starehe n.k Wewe ndio hasa mwenye kujua uwapeleke wapi kulingana na mambo hapo niliyosema hapo juu.

Kuwa makini hasa kipindi hiki cha sikukuu, Goodluck.
 
Last edited by a moderator:

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom