Kumpiga mizinga mpenzi wako ni ushamba wa mapenzi

Kumpiga mizinga mpenzi wako ni ushamba wa mapenzi

Hi
Nyie walimbwende wa jamii forums embu piteni hapa muone mwenzenu alivyo na akili na busara mnaweza jifunza kitu hapa

Ule uamuzi wa kupinga ndoa kidogo naweza ulegeza kumbe kuna wanawake wana akili unaweza weka ndani

Waambie bwana pesa sio kipimo cha mapenzi pia kumbuka pesa inauza utu wako
Hiyo sio akili ni matope 🏃🏃🏃🏃🏃🏃🏃
 
Walahi nawambia,sisi wanawake tuna kajitabia fulani tulikoaminishwa kuwa kupendwa lazima upewe hela

Yaani ili uonekane unapendwa akupe hela ya matumizi,huo ni ushamba

Utawakuta wanawake salon,oooh nataka kumuacha peter kwa sababu hanipi hela ya matumizi,miezi 3 hanipi hata senti,yeye ni kuniita tu anataka papuchi

Mwingine anasema,Mudy ananipenda balaa,nikiomba tu hela hana chenga,ananipa,

Yaani sisi tumejijengea mawazo kuwa mwanamke ndo anayetakiwa kutoa,kutoa,kutoa,kutoa tu,tena na tena,jamani haya sio mapenzi ni kuumizana

Pia tumejijengea mawazo kuwa unapokuwa na mwanaume basi shida zimeisha,basi unakaa kusoviwa matatizo yako,dah!

Unakuta mwanamke ana kazi yake nzuri tu,ana kipato kizuri tu,lakini anapata mwanaume,anaanza kumuomba hela,anaomba hela,ili mwanamke aonekane anapendwa atakapopewa hiyo hela,huu ni ushamba wa mapenzi,asipopewa atachukia,atakunja sura kama ameonja ndimu,ila ana mshahara wake

Na nyie wanaume, kinachosababisha wanawake wanawaomba hela,au kuwapiga mizinga,ni tabia zenu za kuwa na wanawake wengi

Tunahisi una mwanamke ambaye unamgaharamikia unatuacha sisi tulio na real love kwako,coz kwa michepuko hamjambo

Unamuwezesha hela ya kuzungukia mtaani,labda elfu 50,anampelekea Mwajuma,au anawaza kumhonga mpenzi mpya,wanaume akili zenu muda mwingine hamnazo
Wape ukweli shogaangu....
 
Anahudumiwa mke tu, hawara hahudumiwi, hawara anapewa kulingana na anavyotoa. Ukimhitaji kingono unampa ili akupe( I think the rule applies so well kwa michepuko)
 
Hi
Hiyo sio akili ni matope [emoji125][emoji125][emoji125][emoji125][emoji125][emoji125][emoji125]
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Back
Top Bottom