Kumpenda Mtu Si Sababu pekee ya Kuowa/kuolewa Naye

Nyoka_mzee

JF-Expert Member
Nov 26, 2016
3,695
5,522
Wengi Katika vijana wa zama hizi ,Tunachukulia mapenzi ndo kigezo kikubwa katika kutafuta wenza wa kuishi nayo,
Mimi binafsi nakataa ,mapenzi si gezo mama cha kutafuta mwenza wa kuishi naye ,

Yapo Mambo Muhimu ya kuzingatia katika kumtafuta Mwenza wa maisha;

1:Dini ,
hiki ni kigezo mama katika kumtafuta mwenza wa kuishi naye ,
Na hapa acha ni weke wazi ,Sio mtu alovamia dini ukubwani,Yatakikana umpate mtu alolelewa katika misingi ya dini na akaishi katika misingi ya dini.
Kwanini nakataa hawa wanaojuwa Dini ukubwani ,wengi ni waigizaji,

2:Tabia,
Hiki ni kigezo cha pili katika kutafta mwenza wa kuishi naye,ni vyema ukampata mtu mwenye Tabia njema,na Tabia njema inatokana na malezi mema aloyapata toka kwa wazee wake,
Na ndomana wazee wa zamani walikuwa wanakwenda kumposea mchumba kijana wake ,Kigezo wanacho angalia kwa bint ni malezi alokulia,

3:Ukoo wake,
Hili pia nalo lina umuhimu sana sana kwa mustakabali wa Mahusiano yenu,Kuna koo huwa hazistahili kuowa/au kuolewa nazo,Kutokana na mambo mbali mbali,ambayo siwezi anisha hapa yote watu wakanielewa,ila zipo Koo zina laana mbali mbali na kama utaowa/Kuolewa nazo utajikuta umeingia matatizo.

Mwisho Ni hitimishe kwa kusema Tena mapenzi Si Kigezo cha kuowa/au kuolewa na Mtu,maana Leo unaweza ukaowa /Au kuolewa na mtu Humpendi ukajifunza kumpenda ,maana mapenzi ni kitu chenye kuja na kuondoka ,wapo waloowana kwa mapenzi makubwa ,matokeo yake wakaachana tena kwa chuki kubwa. Na wapo ambao hawakupendana ila wakajifunza kupendana.

Na ndomana ukiangalia ndoa nyingi za wazazi wetu hasa kina mama wakikupa historia zao utaskia wakikwambia mie nimeolewa na Baba ako sikuwa nampenda.

Kwahiyo hapa tunajifunza mapenzi yanatengenezwa
 
NAKUUNGA MKONO MKUU NDOA NI ZAIDI YA UPENDO.HUMO KUNA UVUMILIVU,NIA,KUTHUBUTU,HESHIMA NA UAMINIFU PIA.
Nashkuru mkuu na wengi wanajua msingi wa ndoa ni upendo lakini wanasahau Ndoa inamisingi yake ili hata uwo upendo uje
 
Umesema kitu ambacho daima nakiamini. Mapenzi/ upendo ni jambo mtu unaweza kujifunza. Ndiyo maana mama zetu walikutana na baba zetu kanisani siku ya kufunga ndoa ( yaani hawakujuana kihivyo) lakini waliishi mpaka kifo au uzee wao. Msingi ulikuwa moja vetting ya nguvu iliyofanywa na wazazi au ndugu wa wanandoa watarajiwa
 
Yote kwa yote ndoa ya amani ni ile ambayo wote mnapendana hizo nyingine mbwembwe
Agata ipo siku utanielewa ,maana sikuandika kwa hisia zangu ,nimefanya uchunguzi na kuweka hisia zangu ,maana hata mie binafsi ukiniuliza mnamaoni yangu tofauti na haya ila hayafanyi nikaacha kuuwona ukweli
 
Umesema kitu ambacho daima nakiamini. Mapenzi/ upendo ni jambo mtu unaweza kujifunza. Ndiyo maana mama zetu walikutana na baba zetu kanisani siku ya kufunga ndoa ( yaani hawakujuana kihivyo) lakini waliishi mpaka kifo au uzee wao. Msingi ulikuwa moja vetting ya nguvu iliyofanywa na wazazi au ndugu wa wanandoa watarajiwa
umeona eee ,sasa jiulize sie ambaye tunajitia kuyajua mapenzi na kuamini mapenzi ndo msingi wa ndoa je ndoa zetu zinadumu?

Ifike mahali tukubali kuna mahali tunakosea ,na pia tujifunze kuziruhusu nafsi zetu kujifunza kutoka kwa wale walotutangulia na si kuishi kwa mazoea au kwa hisia zetu.
 
Ndoa ni taasisi pana sana na ni msingi wa mambo yote hapa duniani,sikupingi kwa hoja yako lakini nitaongeza tu. Upendo nao ni sehemu ya maisha ya ndoa,tatizo la leo ni kuwa hatuandai vijana wetu kuishi katika jamii (,ndoa ni sehemu ya jamii pia) Jamani kuna watu haiwezikani tu kuishi nao,hawawezi kuchangia kitu,hawamfikirii mtu,hawajali hisia za wengine,yaani wao ni wao tu basi,sawa atapenda ila hawezi kuvumilia mapungufu ya mtu wala hajui kama na yeye ana madhaifu mengi tu.
 
Nishukuru sana kwa mchango wako ,na pia kwa kukubaliana na hoja ,na mimi nimeutoa upendo kuwa msingi mkubwa wa ndoa sbabu baada ya kufanya tafiti mbali mbali,maana hata mimi mwanzo nilikuwa muumini wa uamini mapenzi ndo msingi katika mahusiano,lakini nikajaribu kufanya utafiti nikagundua wengi wanaopendana sana ndio wanaoongoza kugombana na kuachana kwa sababu mbali mbali ,na wapo ambao mpaka leo wanashindwa kuishi pamoja kwa sababu mbali mbali ,japo wanapendana tena sana,

Kwahiyo ulichosema ww nakubaliana nacho kwa asilimia zote maana umeongeza nyama kwenye mada husika na shukran kwa mchango wako
 
Ila mkuu hata zile shule za bweni nazo zilikuwa zinasaidia,na pia yale maisha yetu ya kizamani ya kwenda visimani,kutafuta kuni,sokoni yalikuwa yanatuzowesha kuwavumilia watu wengine, Siku hizi maji ndani,shule kila mtoto analetwa na mzazi,shopping supermarket,hatuchezi hatuzungumzi hatuzoeani hatujuani,tunaoanaje?
 
Ni kweli kabisa unachosema ,maana sasaivi watu hawana subra ,wakuta mtu anakwambia mimi nataka kuolewa na mwenye gari na nyumba,sasa wajiuliza mbona zamani wazee wetu waloowana wakavumiliana na kutafuta mali pamoja
 
People don't like love, they like that flittery flirty feelings. They don't love love-love is sacrificial, love is ferocious, it's not emotive. Our culture doesn't love love, it loves the idea of love. It want the emotion without paying anything for it.
 
katika mafundisho ya dini ya kiislamu.yanasema ni vigezo vinne .sio vitatu .
1.uzuri wa muhusika
2.twabia zake muhusika
3.ukoo aliotokana
4.Mali zake .
lakini katika hivyo vinne viwili ni muhimus sana na vimesisitizwa.
1.Dini..mfano hairuhusiwi muislamu kumuoa/kuolewa na ahlil kitaabu yaani mayahudi na manaswara (wakristo) na ukifanya hivyo utakuwa umepingana na maagizo ya dini yako.,nadhani ni logic kwa7bu kila mmoja amelelewa na makuzi na ibada tofauti hilo litawachanganya watoto na mwisho wa siku ni migogoro katika hii familia na pia katika mazishi.pia
2.Tabia..hapa kuna logic pia na kuna maingiliano makubwa na dini au malezi ya muhusika.mfano mume ni mlevi au mzinifu au hataki kufanya ibada lakini mke hana hayo mambo hapo ni majanga ktk hii familia.
naomba kuwasilisha
 
Ndugu nilipoleta mada sikutumia kigezo cha hadithi hiyo ambayo mtume amesema mwanammke anaolewa kwa sifa nne,
Mimi nimelenga kwa wanaume na wanawake ,kwa sababu kila mmoja ana haki ya kupata mtu mwenye kuwa na dini na tabia njema ,

Sikutaka kuongia kwenyw Dini maana huko kuna mjadala mrefu ,na kwanza umezungumza haifai kumuowa watu wa ahli kitaabu hili jambo si kweli?
Na pia hao uliowataja Sio Ahli kitabu.

Na naomba huko tusiingie maana kuna mjadala mrefu na unahitaji wasaa na uzi wake
 
Wengi Katika vijana wa zama hizi ,Tunachukulia mapenzi ndo kigezo kikubwa katika kutafuta wenza wa kuishi nayo,
Mimi binafsi nakataa ,mapenzi si gezo mama cha kutafuta mwenza wa kuishi naye ,

Yapo Mambo Muhimu ya kuzingatia katika kumtafuta Mwenza wa maisha;

1:Dini ,
hiki ni kigezo mama katika kumtafuta mwenza wa kuishi naye ,
Na hapa acha ni weke wazi ,Sio mtu alovamia dini ukubwani,Yatakikana umpate mtu alolelewa katika misingi ya dini na akaishi katika misingi ya dini.
Kwanini nakataa hawa wanaojuwa Dini ukubwani ,wengi ni waigizaji,

2:Tabia,
Hiki ni kigezo cha pili katika kutafta mwenza wa kuishi naye,ni vyema ukampata mtu mwenye Tabia njema,na Tabia njema inatokana na malezi mema aloyapata toka kwa wazee wake,
Na ndomana wazee wa zamani walikuwa wanakwenda kumposea mchumba kijana wake ,Kigezo wanacho angalia kwa bint ni malezi alokulia,

3:Ukoo wake,
Hili pia nalo lina umuhimu sana sana kwa mustakabali wa Mahusiano yenu,Kuna koo huwa hazistahili kuowa/au kuolewa nazo,Kutokana na mambo mbali mbali,ambayo siwezi anisha hapa yote watu wakanielewa,ila zipo Koo zina laana mbali mbali na kama utaowa/Kuolewa nazo utajikuta umeingia matatizo.

Mwisho Ni hitimishe kwa kusema Tena mapenzi Si Kigezo cha kuowa/au kuolewa na Mtu,maana Leo unaweza ukaowa /Au kuolewa na mtu Humpendi ukajifunza kumpenda ,maana mapenzi ni kitu chenye kuja na kuondoka ,wapo waloowana kwa mapenzi makubwa ,matokeo yake wakaachana tena kwa chuki kubwa. Na wapo ambao hawakupendana ila wakajifunza kupendana.

Na ndomana ukiangalia ndoa nyingi za wazazi wetu hasa kina mama wakikupa historia zao utaskia wakikwambia mie nimeolewa na Baba ako sikuwa nampenda.

Kwahiyo hapa tunajifunza mapenzi yanatengenezwa

Huyu Mtu aliyehalalisha kugegedana kabla ya Ndoa ndio yanayoleta hizi Hoja .. Ngoja wadada waje kumbe wao wanachotaka ni kugegedana tu
 
umeona eee ,sasa jiulize sie ambaye tunajitia kuyajua mapenzi na kuamini mapenzi ndo msingi wa ndoa je ndoa zetu zinadumu?

Ifike mahali tukubali kuna mahali tunakosea ,na pia tujifunze kuziruhusu nafsi zetu kujifunza kutoka kwa wale walotutangulia na si kuishi kwa mazoea au kwa hisia zetu.
Tofauti ya zamani na sasa ni kiwango cha uvumilivu zamani wamama zetu walikuwa na 98% ya uvumilivu but hawa daa zetu wa sasa ni aslimia chini ya 30.
 
Kwanini hawa wasasahivi wanakosa uvumilivu na wale wa zamani waloweza ?
Kuna tatizo gani happ kati?
ebu tujuze,
 
Back
Top Bottom