Kumpenda Mtu Si Sababu pekee ya Kuowa/kuolewa Naye

Wengi Katika vijana wa zama hizi ,Tunachukulia mapenzi ndo kigezo kikubwa katika kutafuta wenza wa kuishi nayo,
Mimi binafsi nakataa ,mapenzi si gezo mama cha kutafuta mwenza wa kuishi naye ,

Yapo Mambo Muhimu ya kuzingatia katika kumtafuta Mwenza wa maisha;

1:Dini ,
hiki ni kigezo mama katika kumtafuta mwenza wa kuishi naye ,
Na hapa acha ni weke wazi ,Sio mtu alovamia dini ukubwani,Yatakikana umpate mtu alolelewa katika misingi ya dini na akaishi katika misingi ya dini.
Kwanini nakataa hawa wanaojuwa Dini ukubwani ,wengi ni waigizaji,

2:Tabia,
Hiki ni kigezo cha pili katika kutafta mwenza wa kuishi naye,ni vyema ukampata mtu mwenye Tabia njema,na Tabia njema inatokana na malezi mema aloyapata toka kwa wazee wake,
Na ndomana wazee wa zamani walikuwa wanakwenda kumposea mchumba kijana wake ,Kigezo wanacho angalia kwa bint ni malezi alokulia,

3:Ukoo wake,
Hili pia nalo lina umuhimu sana sana kwa mustakabali wa Mahusiano yenu,Kuna koo huwa hazistahili kuowa/au kuolewa nazo,Kutokana na mambo mbali mbali,ambayo siwezi anisha hapa yote watu wakanielewa,ila zipo Koo zina laana mbali mbali na kama utaowa/Kuolewa nazo utajikuta umeingia matatizo.

Mwisho Ni hitimishe kwa kusema Tena mapenzi Si Kigezo cha kuowa/au kuolewa na Mtu,maana Leo unaweza ukaowa /Au kuolewa na mtu Humpendi ukajifunza kumpenda ,maana mapenzi ni kitu chenye kuja na kuondoka ,wapo waloowana kwa mapenzi makubwa ,matokeo yake wakaachana tena kwa chuki kubwa. Na wapo ambao hawakupendana ila wakajifunza kupendana.

Na ndomana ukiangalia ndoa nyingi za wazazi wetu hasa kina mama wakikupa historia zao utaskia wakikwambia mie nimeolewa na Baba ako sikuwa nampenda.

Kwahiyo hapa tunajifunza mapenzi yanatengenezwa
Uliyoyaweka kwa asilimia 0.01% yana ukweli ilaa asilimia 99.99% si kweli coz wanawake wanabadilika kama pia , saiv hapa baadae pale kesho na kesho kutwa....
 
Unamawazo kama yangu tu nlikua naongea na my friend the same thing mambo ya kuolewa au kuoa only because unampenda mtu na kuacha kuangalia vitu vingne huwa inacost watu wengi sana
umeona eee ,Na hapa mkuu ndipo wengi tulipofeli,Maana wengi wanahisi kumpenda mtu ndo kila kitu ,huwa hawataki kuangalia mambo mengine
 
Ni kweli kabisa unachosema ,maana sasaivi watu hawana subra ,wakuta mtu anakwambia mimi nataka kuolewa na mwenye gari na nyumba,sasa wajiuliza mbona zamani wazee wetu waloowana wakavumiliana na kutafuta mali pamoja
Si mbaya sana kuolewa na mwenye mali,ila kuna gharama ya kulipa. Nina nyumba na gari fine,but I'm eligible kumuoa yeyote na kumuacha wakati wowote pia. Ni vizuri kuanza pamoja na kila mmoja akajua thamani ya kile mlicho nacho.
 
Kwanini hawa wasasahivi wanakosa uvumilivu na wale wa zamani waloweza ?
Kuna tatizo gani happ kati?
ebu tujuze,
Kwa maoni yangu kama upendo tunajifunza,na uvumilivu tunajifunza pia.Hayo yote hayana shule wala vyeti,unajifunza kwa kuchanganyika na watu,mchangamano wa kijamii umeshuka sana, Mtu mmoja hawezi kuwa kila kitu ujue,mfano ukiwa mwanafunzi una marafiki wa kusoma nao,lakini huwezi kucheza nao,wakucheza nao lakini huwezi kukopeshana nao,wakukopeshana nao lakini huwaambii siri zako na wote ni muhimu kwako na unajua jinsi ya kuishi nao. Sasa ukiwapunguza sana akabaki mmoja kuna mambo hayataenda.Na watu wa leo wanadhani kwenye ndoa mke na mume ni lazima kushea kila kitu. Unaweza oa mtu mjingajinga tu na bado ukaishi naye kama mawazo ya maana unayapata kwingineko,na akawa mke mzuri tu japo si mshauri mzuri.
 
Dah nimekupenda bureeeee,maana umefafanua vizuri mpaka raha,mashallah
 
Back
Top Bottom