Kumpa pole, au kumpongeza aliyetumbuliwa lipi bora?

Maguge Maguge

JF-Expert Member
Joined
Sep 1, 2016
Posts
2,734
Reaction score
1,781
Wana bodi, heshima kwenu!

Mimi ni mjasiliatumbo, nafanya kazi za mikono baada ya biashara kunitupa mkono;
Ila nina jamaa zangu na rafiki zangu, wafanyakazi wa serikali, wengine miongoni mwao wametolewa ndagu na JPM kwa kuwatumbua.

Swali langu moja,

baada ya kujua kwamba jamaa au rafiki yangu ametumbuliwa, nikimpigia simu au kukutana nae, nimpongeze kwa hatua alizopitia kula fedha ya umma, au nimpe pole?
 
Mtukane, mwambie ni fala tu, kama anataka maisha ya kuwa mtumishi asome! Tena hao Anko Magu anawatafta!
 
Pole ya nini kwani kafiwa?si katumbuliwa?mpongeze tu kwa hatua aliyofikia.
 
Kwani lazima umpe pole au umpongeze? Wewe jifanye tu kama hujui kua katumbuliwa.
 
Naona umefurahi saaana, mwenzio kutumbuliwa
 
Mimi natoa salamu pekee yake,naanzisha stori za RONALDO vs MESSI basi
 
Mpongeze kwa sababu amenusurika kwenda JELA miaka 15 na kazi ngumu.
 
Kakwambia anataka pole yako?? Ingekuwa ni baba yako ungempa??
 
Pecial mbona umejibu kwa ukali ama nawe upo kwenye orodha?Sasa hivi ni mwendo wa list tu.
 
Kama ana nyumba, gari, biznesi na watoto mpe pole kama hana achana nae asije kukuzibuwa [emoji1][emoji1]
 
UNATAKIWA UKIMUONA UMZIBUE VIBAO KWA KUWA UWEPO WAKE SERIKALINI ATAKUWA AMEHARIBU MAMBO MENGI SANA IKIWEMO KUUWA KWA KUTOJUA ANACHOFANYA.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…