GENTAMYCINE
JF-Expert Member
- Jul 13, 2013
- 59,949
- 119,216
Kila nikisikia Mwenyekiti wa Yanga Yusuph Mehboob Manji akisema anajiuzuru Yanga huwa nawashangaa mno Wana Yanga wanavyoanza kupepesuka huku wakitaka kumlamba hadi Miguu na kumnyenyekea.
Sidhani kama hasa kwa Wanaume waliokamilika kabisa ( namaanisha rijali ) kila mara kumbembeleza Mwanaume mmoja tu ambaye ni Tajiri ili abakie au awe nao ni jambo jema na kwa sisi Wakazi wa Pwani Kitendo hiki cha Wana Yanga wanachokifanya kwa Manji kinaleta taswira mbaya mno ambayo siyo ya Kiume.
Hapa ndipo ninapoikumbuka Kauli ya Manji ambayo aliitoa katika moja ya Mikutano yake na Yanga pale Police Officers Mess aliposema namnukuu " Jamani wana Yanga wenzangu hebu tujipangeni kwa maslahi mapana ya Yanga kwani leo Mimi Yusuph naweza kuwepo na Kesho nisiwepo hivyo msiishi kwa kumtegemea tu Mtu mmoja bali tujitahidi ili Yanga yetu iweze kuwa na Wadhamini wengi na vyanzo vya kutosha vya mapato " mwisho wa Kumnukuu.
Mtu hawataki nyie mnamng'ang'ania wa nini? Hizi njaa za dhiki zitawapelekeni wapi? Hivi Yanga haiwezi kuendelea bila uwepo wa Manji? Bado nasisitiza kusema kuwa kwa Watu wa Pwani ni jambo baya mno ukiona Wanaume wanaojielewa kabisa huku wakijinadi wao ni Vidume / Rijali wakiwa wanajikomba na kujipendekeza kwa Mwanaume Rijali Mkuu mmoja.
Mmeiabisha mno Klabu ya Yanga!