Kinachosababisha sasa bifu kati ya matajiri hawa Mengi na Manji si kingine bali ni Urais wa Oct 2015

MINOCYCLINE

JF-Expert Member
Apr 2, 2015
8,011
16,748
Naomba kwa leo nitoe tu observation yangu ndogo tu lakini ninayoamini itaweza kuwafungua wengi wenu japo naamini kuna wengine wenye maono ya kina wameshaliona hili.

je kulikoni?

Kwa takribani miaka kadhaa sasa ya hivi karibuni pamekuwepo na mvurugano usio na kichwa wala miguu kwa wafanyabiashara wakubwa na maarufu hapa nchini Tanzania.
Mmoja akiwa ni mtanzania halisi bwana Reginald Mengi na mwingine akiwa ni mtanzania mwenye asili ya Asia Yusuf Mehboob Manji.

Wawili hawa kama utakumbuka wamekuwa katika bifu zito tokea miaka ile ya 1997 / 1998 ambapo kama mtakumbuka bwana Mengi alikuwa ndiyo mdhamini kama siyo mfadhili mkuu wa klabu pinzani kwangu ( namaanisha Yanga F.C ).

Lakini uongozi wake unasemekana ulikuwa na misukosuko mingi sana ambayo hata hivyo wachambuzi wa mambo wanasema ilikuwa ikichochewa na bwana Manji ili kumuharibia bwana Mengi na ashindwe kuiongoza au kuwaongoza watani zangu kimpira timu ya yanga F.C .

Kitu ambacho kwa kiasi kikubwa sana kilifanikiwa ambapo kama mtakumbuka mwaka 1998 hapo wakati wa mkutano wa Yanga pale hotel ya starlight palitokea fujo kubwa mno ambayo ilipelekea mlinzi wa karibu wa bwana Mengi kupigwa na watu waliokuwa wakimkataa bwana Mengi kuendelea kuwaongoza.

Na nakumbuka sana siku hiyo bwana Mengi ilibidi akimbie na aende kujificha ktk moja ya vyoo pale Starlight ili kujiokoa mpaka pale baadhi ya wazee wenye busara zao na haswa alikuwa ni mzee Msumi alipoenda kumwokoa na kumtoa pale ukumbini .

Kisha baada ya muda mchache tu Mengi akaachia ngazi kuwa mfadhili na mdhamini wa klabu ya Yanga.

nini kiliendelea?

mara tu baada ya bwana mengi kujitoa yanga hasa katika nafasi ya ufadhili mkuu inasemekana na yeye alihakikisha kuwa klabu ya yanga haitawaliki na kama mnakumbuka pia kuna wakati fulani hali ya hewa jangwani haswa kipesa ilikuwa ni mbaya sana ambapo ilisababisha timu kufanya vibaya watu kuchapana sana viboko ( kama mnavyowajua watani zangu yanga kwa kuchapa viboko hawajambo ) hivyo kwa kiasi fulani lengo la bwana mengi likatimia. lakini ikumbukwe pia kuwa wakati bwana mengi akifanya hayo huyu bwana manji na yeye alikuwa ameshajipenyeza yanga kikamilifu na akaanza kwa kuwaweka madarakani watu wake haswa tajiri mosha na wengineo akiwepo hata rais wa sasa wa tff bwana malinzi ili wamtengenezee mazingira ya yeye kuja kuingia yanga. na mbinu kubwa ambayo bwana manji aliitumia ni kuwaweka hao vibaraka wake yanga huku tena akiwazunguka kwa kuwafelisha ktk mambo yao ya kiuongozi ili kusudi tu waonekane hawafai na yeye akatafuta watu wa mjini ambao aliwaweka sawa ( kipesa ) kisha wakaanza kumpigia chapuo bwana manji apewe klabu ya yanga mpango ambao ulifanikiwa kwa kiasi kikubwa sana na mpaka leo bado anadunda klabuni yanga huku bwana mengi akiwa haamini alivyozidiwa ujanja na kanjibai / panjuani.

uadui uliongezekaje?

mara baada tu ya bwana manji kupewa mikoba ya kuidhamini na kuiongoza yanga habari za ndani zinasema kwamba kitendo hicho hakikumfurahisha kabisa bwana mengi hivyo na yeye akaamua sasa atumie vyombo vyake vya habari ambavyo kiukweli ni super brand kwa sasa hapa tanzania ( ukibisha ktk hili utakuwa una lako jambo tu ila ukweli ndiyo huo ) ili kummaliza bwana manji na kwa kiasi kikubwa sana bwana mengi alifanikiwa kwani kama mtakumbuka hapo miaka kadhaa tu iliyopita bwana mengi alidiriki hata kujitokeza waziwazi na kumshutumu bwana manji kuwa ni mnyonyaji na haswa ktk lile sakata lililovuta hisia za watanzania wengi la mengi kutaka kuuziwa hotel ya kilimanjaro lakini pakatokea na figisu figisu hapa katikati na ikala kwake huku bwana manji akihusishwa na uuzwaji wake na hadi kuwa na share hapo. hali hii ya chuki za hawa watu ziliendelea na mpaka leo bado hazijakoma na ili kulidhihirisha hilo ni kwamba hapa majuzi tu gazeti la nipashe liliandika habari moja inayohusisha kampuni ya bwana manji ya quality engineering iliyokwepa kulipa kodi kiasi cha shilingi bilioni 9 za kitanzania na hapo hapo bwana manji nae akikaririwa akimtaja bwana manji kuwa ni fisadi, mwizi na mwongo. leo hii tena bwana manji na yeye amekuja na mpya kwa kusema kuwa shabiki namba moja wa klabu yanga ni hayati baba wa taifa mwalimu nyerere lakini akasema tena kwa msisitizo kuwa adui namba moja wa klabu ya yanga ni bwana reginald mengi na kwamba amemvumilia kwa mambo mengi tu na sasa amemchoka hivyo anataka kuwe na mdahalo wa wazi kati yake bwana manji na bwana mengi ili kila mmoja aje na uthibitisho wake wa tuhuma anazotupiwa kisha watanzania tupige kura nani kati yao ndiyo mwongo, mfitini, mnafiki na mwizi ( ila sidhani kama ktk zoezi hili sisi wanachama, wapenzi na mashabiki wa simba sports club tutahusishwa kwani tuna allergy na masuala ya yanga na mpaka timu yao wenyewe ).

mtazamo wangu wa kimantiki.

nikiwa kama mmoja wa mfuatiliaji mzuri sana wa siasa za maji taka za tanzania na haswa ukizingatia kuwa mwaka huu kuna kindumbwe ndumbwe na michakato imeshaanza huku na kule kuna mambo kadhaa nimeyagundua na yaliyojificha ktk ugomvi wa hawa wafanyabishara wakubwa ( japo siwaiti matajiri kwakuwa hawajafikia hata robo tatu bado ya kuitwa matajiri wa kufananishwa na akina mzee aliko dangote na wengineo wengi tu wa duniani ) ambayo ni kama yafuatayo :

  • nina uhakika kuwa ugomvi wao hawa jamaa sasa umekuwa mkubwa haswa kutokana na maslahi ya kisiasa zaidi kuliko hata biashara zao kwani hakuna ukweli usiojulikana kuwa bwana mengi ameshaamua kujilipua ( kumuunga mkono ) mtangaza nia edward lowassa huku pakiwa hakuna ubishi kuwa bwana manji ana ukaribu sana na familia ya kikwete hasa kupitia kwa mwanae riziwani huku familia ya kikwete haswa kupitia kwa ridhiwani na mama yake ( salma kikwete ) wote wakiwa nyuma ya harakati za mtangaza nia mwingine na ambaye ni mpinzani mkubwa wa lowassa na si mwingine bali ni bernard membe hivyo automatically tu bwana manji amejikuta akiangukia kwa swahiba wake ridhiwani kikwete ktk kumsapoti membe.
  • kitendo cha kuenea kwa tetesi kuwa bwana manji anataka kuwania ubunge jimbo la kigamboni nalo limeonekana kuwa ni sababu nyingine ya vita vya bwana mengi kwa bwana manji na kinachofanyika sasa ni kwa bwana mengi kuzidi kumchafua bwana manji ili jamii imuone kuwa hafai na asiweze kufanikisha hiyo azma yake ya kutaka kuwania ubunge jimbo la kigamboni.

mbinu gani sasa inatumika?

wengi wenu mnaweza msilione hili au mkawa bado mnalitafakari ila ukweli ni kwamba bwana manji na hao wenzake haswa akiwa huyo mtangaza nia mpinzani kwa lowassa walichoamua sasa ni kutumia mbinu moja kali sana ya kimafia ambayo ni kumchokonoa bwana mengi ili na yeye awe anajibizana nae na mchezo utakuwa ndiyo huo ili tu kuvifanya vyombo vyake kuhamisha attention yote kutoka ktk hizi harakati na vuguvugu la kuelekea uchaguzi mkuu october na kurudi ktk personal issues za hawa wafanyabiashara wakubwa na maarufu huku nia kubwa ikiwa ni kutovifanya vyombo vya bwana mengi kumpa coverage kubwa mzee lowassa na ni kitu ambacho naamini kitafanikiwa na hii ni kutokana kwamba bwana mengi ni mtu anayependa sana publicity na sympathy hivyo kwa tunavyomjua ni lazima tu atauuingia huu mkenge labda ashtuke baada ya huu uchambuzi wangu.

nani ataathirika zaidi kibiashara?

hapa wala hakuna kupepesa macho wala kutikisa masikio na kama ulimsikia vizuri sana manji akizungumza ktk press conference yake na haswa ukizingatia kuwa anaaminika na anakubalika sana na wana yanga ambao kwa takwimu zisizo rasmi zinasema kuwa yanga ndiyo timu inayoongoza kwa kuwa na washabiki wengi nchini tanzania ile kauli ya bwana manji kuwa bwana mengi ndiyo adui namba moja wa klabu ya yanga inaweza ikamharibia bwana mengi ktk biashara zake ( na hili watu wa marketing mnajua na mtatusaidia kulichambua zaidi ) kwani wadau wa yanga na wao wanaweza wakajikuta wanaanza kususia products za kampuni za bwana mengi hivyo kupelekea kushuka kwa mapato yake. mfano wa hili ulijidhihirisha miaka 4 nyuma wakati wa uongozi wa mheshimiwa rage simba sports club ambapo nakumbuka kuna habari fulani maulid kitenge na mwenzie omary katanga walizitangaza ndivyo sivyo za kuihusu simba na kilichotokea rage aliwaaminisha wana simba wote kuwa redio one na itv zilikuwa na chuki na simba hivyo wasinunue bidhaa yoyote au kujihusisha vyovyote na makampuni ya bwana mengi kitu ambacho kwa mara ya kwanza mengi alidhani simba wanatania lakini kadri siku zilivyokuwa zinaenda mapato ya products zake zilishuka hadi bwana mengi na management yake ilipoomba " po " suluhu na simba ndipo hali ikawa sawa na mambo yakaenda kisha redio one na itv zikaanza kutangaza habari za " mnyama ".

hitimisho ya nini kifanyike.

kwa hali ilipofikia sasa na upepo huu wa kisiasa unavyokwenda nadhani ipo haja ya watu wenye busara ktk taifa hili au nchi hii kuwaita wafanyabiashara hawa na kuwakalisha chini ili wamalize tofauti zao kwani kwa kiasi fulani zina athari kubwa mno kwa wafuasi wao na kinaweza hata kikaharibu upepo mzuri wa amani ya nchi hii haswa kutokana na maneno yao ya kuchafuana na ya kichochezi na nikiwa kama mtanzania napenda kusema kwamba bwana mengi na bwana manji nyie wote ni watanzania wenzetu na wote tunawahitaji kwa namna moja au nyingine hivyo tumieni busara zenu muweze kuyamaliza haya na nawasihi wote kuwa acheni kutumika kisiasa kizembezembe na mkazidi kujishushia hadhi zenu mbele ya jamii inayowazunguka.

akhasateni na naomba kuwasilisha.
 
Ngoja na mimi nipambane niwe tajiri namba moja Tz... Naamanisha na wala sitaniii....
 
Endelea kubuni vingine .... sio mwanayanga yote hayo umeyajuaje kama sio usabasi
 
Hawezi kuwa looser hata kama wakisusia bidhaa zake..still market ni kubwa sana hapatakuwa na impact.
 
Uchambuzi makini ila kitu kimoja umesahau katika sifa za Mengi. Nayo ni mbaguzi wa rangi pia. Tatizo lake kubwa ni ubaguzi kwake yeye watanzania wenye asili ya asia na warabu anawachukia sana..hili ndio tatizo lake kubwa na kijiba hichi humchoma zaidi akiona wanamzidi kubiashara na umaarufu.
Kuibuka kwa Azam Tv yenye nguvu na mikakati endelevu kuna mnyima usingizi lakini anashindwa atamuanzia wapi Bakhressa mtu ambaye ni kipenzi cha walalahoi na pia watawala na waonesha nia wote .
Apunguze jazba za chuki Tanzania ina mchanganyiko ya makabila na rangi tofauti na itabski hivyo hawezi kuibadilisha
 
Hawezi kuwa looser hata kama wakisusia bidhaa zake..still market ni kubwa sana hapatakuwa na impact.

na ndiyo maana niliwaomba michango yenu hasa nyie watu wa marketing kwani naamini mna mengi ya kitaalamu zaidi juu ya hili suala. akhsante kwa mchango wako.
 
Huu sio muda wa kujadili bifu za manj na mengi!! ...watanzania tunavitu vingi vya kujadili...kwanza IKULU SIO ZA BABAZAO
 
Mtanzania mwenye asili ya kiasia!!

Watanzania wengine wana asili ya Wapi

naogopa kujibu maswali ya " kitoto " japo nakuheshimu na huwa naheshimu mno michango yako na sijui leo umeamkia ubavu gani. kwa ninavyokujua sikutegemea swali kama hili kutoka kwa mtu kama wewe. watanisaidia wengine kunijibia swali lako uliloniuliza.
 
mpango wa kuwashobokea wahindi ufe mara moja,wao mbona hawanashobo na majitu meusi.kiukweli hapo hata kama mengi ndio mwenye makosa au hana makosa mi nitakuwa upande wa mniga mwenzangu.huyu manji hela zote anapeleka kwao calcuta na mumbai
 
Ulitafakari kabla ya kuandika?

Nimetafakari sana nimeona mwisho kabla ya mwanzo. Hakuna impact yoyote. Siandiki kwa ushabiki mii sio shabiki wa mpira na hivyo mtu mmoja hawezi shawishi washabiki wote wamchukie mtu mwimgine sababu tuu ya interest zake hiyo haipo na hao watakao shawishika hawana madhara.
 
... sio mwanayanga yote hayo umeyajuaje kama sio usabasi
Kwani habari iliyo mbaya kwa YM ikitoka kwenye chombo cha I-PP huwa ni kwa ajili ya wana-Yanga tu? Kwani YM akiitisha press conference kuelezea uadui wa Dr Reginald Machache kwa klabu ya Yanga, huwa hiyo press inawahusu wana Yanga tu? Very low.
 
nakushukuru mkuu kwa kuweza kumsaidia kujua jinsi ya kufikiri ili aendane na great thinkers wengi waliotukuka waliopo humu jamvini. big up sana.
 
Back
Top Bottom