Kumiliki Leseni Tanzania ni anasa?

Njowepo

JF-Expert Member
Feb 26, 2008
9,710
2,226
Wananchi watamudu gharama za leseni mpya?




WIKI hii niliandika makala yenye kichwa cha habari kilichosema: "Serikali yajizatiti kudhibiti ughushaji wa leseni za udereva."
Hakika naweza kusema nilipata maoni mengi sana juu ya makala hiyo.

Miongoni mwa maoni yaliyonifanya kuandika mtazamo huo ni msomaji mmoja kuniuliza iwapo serikali inafanya maamuzi hayo iliwafikiria nini baadhi ya madereva hasa wanaokabiliwa na hali ngumu ambao wamesomea nafasi hiyo kwa msaada wa ndugu.

"Hivi huu mpango wa leseni mpya ulizingatia haki zetu madereva…au wanatukandamiza kwa kuwa hatuwezi kupinga? Hakika serikali inatumia mabavu." Huo ni ujumbe nilioupokea kutoka 01 kwa msomaji mmoja.
Lakini wapo wengi waliopiga simu na kutaka kujua zaidi kuhusiana na mpango huu ambao umeanza katika baadhi ya mikoa.

Napenda kuwaeleza wahusika, hasa wale waliobuni mpango wa kubadilisha leseni za zamani ili kuweza kukabiliana na tatizo la kughushi kwa kuweka kumbukumbu sahihi za madereva pamoja na kudhibiti mapato yanayopotea, hakika hiyo ni hatua njema na ya kufurahisha kwa kuwa serikali imefikiria namna ya kudhibiti vyanzo vya mapato.


Lakini swali la kujiuliza, je, wananchi wote wataweza kumudu gharama za upatikanaji wa hizo leseni ambazo ni sh 40,000? Au kuna wimbi kubwa la madereva kubaki vijiweni?
Kwa mtazamo wangu naamini kuna baadhi ya watu wanakwenda kupoteza nafasi zao na kazi zao kutokana na kukosa fedha za kununua leseni.

Nasema hayo kutokana na kuongezeka kwa wimbi la umaskini ambapo hadi sasa watu wengi wanaishi chini ya dola moja ambayo haitoshi kwa manunuzi ya kitu chochote.
Sasa leo kuna baadhi ya watu wameweza kupata wafadhili au hata kukopa sehemu mbalimbali ili kuweza kuwa na ujuzi katika fani ya udereva, huyu atafanikiwa kumiliki leseni hiyo ambayo kwa sasa inaonekana kama mali ghafi?

Je, serikali imeshirikisha wananchi wakati wa uandaaji wa mpango huo? Ninaamini kabisa katika suala hili la kubadilisha leseni hakuna mwananchi aliyeshirikishwa bali ni maamuzi ya wataalamu na baadhi ya viongozi wamekaa na kubuni huo mpango.
Sipendi kuukosoa sana lakini kuna utaratibu unaofanyika pindi unapoandaa jambo, si katika suala hili tu bali hata katika familia mtu anapohitaji kuoa au kuolewa ni lazima familia ishirikishe watu ili kuweza kuandaa vikao na kupata michango yao.

Sasa iweje katika masuala yanayohusu masilahi ya watu wengi kama si taifa zima kushindwa kutoa hata miezi kadhaa ili jamii iweze kujadili masuala hayo muhimu hasa hili la upatikanaji wa leseni ambalo limeonyesha kuumiza asilimia kubwa ya watu.

Kipindi cha nyuma leseni ilivyokuwa inatolewa kwa kiasi kidogo bado wimbi kubwa la watu walishindwa kumudu sasa leo imefika kiasi hicho, je, Mtanzania wa hali ya chini ataweza kumudu gharama yake.
Ni kweli leseni mpya zitaweza kupunguza ongezeko la ajali za barabarani kama baadhi ya viongozi walivyodai?
Lakini ikumbukwe hata kama tutafanikiwa pia serikali itasababisha kuwepo kwa wimbi kubwa la watu watakaoshindwa kumudu gharama.
Hakika kwa sasa lazima Watanzania wabuni njia mbalimbali za kuongeza kipato maana bado wanakabiliwa na majukumu ya elimu ya kuwapatia watoto walionao, tena ikiwemo michango lukuki kutoka katika baadhi ya shule.

Kuna masuala ya madawati yanayohitaji fedha, kodi ya pango, umeme, maji bado na suala la afya, sasa hapa lazima tujiulize, serikali hii inamsaidia Mtanzania hasa wa kipato cha chini au inamkandamiza kama msomaji wetu alivyodai?

Kila siku nimekuwa mstari wa mbele kuisii serikali inapofanya maamuzi yanayogusa jamii haina budi kuwashirikisha au kama sivyo kuna vyombo mbalimbali vinavyoshiriki kuzungumza kwa ajili ya wananchi.
Kwanini suala la leseni halikupelekwa hata ndani ya Bunge ambao ni wasemaji wa wananchi kama wanaandaa mpango huo walishindwa kushirikisha wahusika?

Iwapo serikali inaandaa mikakati au mipango inayogusa wananchi ni haki kushirikisha wahusika ili kuondoa utata kama huu uliojitokeza kwa wasiokuwa na taarifa au wasiojua kinachoendelea juu ya leseni mpya za udereva ili kuondoa utata.
MY TAKE
Am sure huu utakuwa mradi wa mtu tshs 40,000 ni hela nyingi kwa mtanzania wa kawaida.
 
Serikali ni watu, na hawa watu wanawakilishwa na wabunge. Kwa hiyo. Taratibu ni kama ifuatavyo. Kila mtu wa kupata haya malalamiko ni Mbunge. Wabunge ndio wanaowapa ruhusa ya kufanya hivo, ni vyama vyote vinahusika. Kiwastani ukimuliza hizi khabar mbunge wako atakupa vizuri hekima ya serikali kukusanya hizi pesa, ikiwemo ya mbinu ya kupunguza ajali barabarani. Kuendesha gari ni Haki ya Mtanzania. "Uhuru wa kutembea" kwenye katiba.

Mtu anayeweza kuendesha gari, anayo hekima ya kutosha kufanya kazi zingine, akionyesha mbinu na akazifuata. Kinachohitajika ni kujua kusoma na kuandika na hesabu za primary school.

Nice work!
 
Lesen elfu 40, passport (haki yako) shs elfu 50 na zaidi, bado hujalipa bili ya umeme, maji, nauli, mafuta, mchele kwa mangi hujanunua hapo, ada za shule, mchango wa mwenge n.k.
Hiyo ndiyo CCM bana. mkiendelea kuiendekeza kuna mengi yatakuja zaidi ya haya.
 
yani nchi hii mpaka dr slaa atawale vinginevyo tunakokwenda tutakuja kudaiwa kodi ya kuishi wakati kuishi ni haki ya mtu kikatiba ila tunakokwenda ubunifu utawaishia wataanzza kutudai kulipia punzi kwa sekunde
 
Back
Top Bottom