Man from cuba
JF-Expert Member
- May 2, 2021
- 557
- 1,365
Kwanza kabisa niwape pole ndugu zangu watanzania kwa msoto mkubwa tulioupata kwa mwaka 2022.Wengi wetu tulitegemea mambo angalau yangekuwa nafuu lakini tulikula msoto kama tuko jehanamu😀😀😀😀 umeme, maji, vyakula kupanda bei, mvua kuchelewa ni baadhi ya mambo yaliyowafanya watanzania kupigika haswa.
Tukiachana na hayo kuna list ya Wabunge ambao tulitegemea angalau wangeweza kupigania tasnia iliyowatoa lakini kinyume chake waligeuka kuwa kama Maguire.
Kwa wale wasiomfahamu Maguire ni beki ghali England ambaye hana msaada na mda mwingine anageuka kuwa msaada kwa wapinzani wao.
Hii hapa chini ni list ya Wabunge kumi waliofanya vibaya kwa mwaka 2022 na wanatarajiwa kuendelea kufanya vibaya kwani uwezo wao ni mdogo kama punje ya haradani;

- Hamis Taletale - Mbunge wa Jimbo moja huko morogoro na meneja wa msanii diamond maarufu kama babu tale anashika nafasi ya kwanza kwa wabunge wenye uwezo mdogo Sana bungeni.Ukifuatilia michango yake bungeni utaona aibu.
- Hamis Kigwangala - Mbunge wa Jimbo moja huko tabora mzee wa nje ya box anashika nafasi ya pili kwa wabunge waliofanya vibaya Sana kwa mwaka 2022. Muda mwingi amekuwa akiutumia instagram kupost vitu visivyo na maana huku jimboni kwake hakuna alichokifanya.
- Mwigulu Nchemba - Huyu Sina maelezo mengi ukituma pesa ukakiona cha moto fika iramba kwa msaada zaidi utakutana na Trab na Trat.
- Erick Shigongo - Huyu alidhan ubunge ni sawa na hekaya za rais anampenda mke wangu pale Buchosa hakuna cha maana bungeni hakuna anachofanya.
- January Makamba - Huyu nawaachia Wana jf
- Ali kinanasi - Mbunge wa kyela aliingia kwa matumaini makubwa lakini hakuna alichokifanya jimboni kwake zaidi ya kujivunia miradi iliyoletwa na rais Samia
- Tulia Ackson - Spika wa bunge na mbunge wa mbeya mjini zaidi ya bajaji na kusaidia misibani hakuna cha maana alichokifanya jimboni Hadi wananchi kummis sugu.
- Nape Nnauye - Anzia jimboni mtama Hadi wizarani hakuna cha maana kinachofanyika.
- Alexander Mnyeti - Huyu nadhani ashajikatia tamaa kwa Wana Misungwi
- Mwita Waitara - Huyu Wana Tarime wanatamani hata uchaguzi ufanyike leo.