Kumfungia mteja bidhaa ni haki yake, Wafanya biashara tafuteni mbadala wa vifungashio hata kama hamtaki vifungashio mbadala vilivyotolewa.

Mwifwa

JF-Expert Member
Apr 3, 2017
46,971
122,292
Kila jambo lazima liwe na athari chanya au hasi.

Marufuku ya vifungashio vya mifuko ya plastiki inaendelea kuzua gumzo mtaani.

Vifungashio mbadala vilivyoingia mtaani havina ubora wowote kuanzia kuhimili kiasi fulani cha uzito, kubeba aina fulani ya bidhaa hasa zenye unyevu unyevu....

Wafanya biashara wadogo ambao ndio wauzaji wa mwisho wa bidhaa mbali mbali za kila aina(hapa naomba tuweke bidhaa za vyakula), wamepigwa na butwaa hawajui hili wala lile juu ya mbadala bora wautumie katika biashara zao wakati wa kuhudumia mteja.

Unaenda kununua mathalani matunda unamwambia nifungie, anabaki anakukodolea macho(hana kifungashio) akitarajia mteja uwe na kifungashio ubebe bidhaa yako uliyonunua huku akisahau kuwa kumfungia mteja bidhaa ni haki yake...

Utafanyaje biashara huna vitendea kazi...? Wateja wakigoma kununua bidhaa zako kisa umeshindwa kuwafungia, hasara ni ya nani.?

Katika biashara lazima upambane na hali yoyote ile ili uweze kufanikiwa katika biashara yako...

Wafanya biashara wadogo tafuteni vifungashio mbadala hata kama hamtaki kutumia vifungashio vilivyoingia mtaani. Hata magazeti kama mnashindwa kununua ili muweze kutimiza haki ya mteja ya kufungiwa bidhaa..?

Serikali ishafanya yake na sidhani kama walifikiria adha zitakazojitokeza katika biashara zenu, imetimiza dhamira yake. Kilichobaki ni ninyi kupambana na hali zetu huku mkiendelea kujiepusha na mkono wake juu ya sheria na kanuni iliyozisimika.
 
Mkuu usemayo nikweli kabisa ila wa Tanzania tunapaswa kubadilika zile zama zakupewa mifuko bure bure zime pitwa nawakati, nivizuri mteja unapoenda dukani kununua bidhaa na unajuwa kuwa bidhaa utakazo nunua ni nyingi ni vema ukabeba kibebeo kabisa, kuhusu magazeti yapo madukani ila sasa ndugu yangu kwamfano mteja anataka ngano kilo 5 utamfungia kwenye gazeti? Haya tufanye utamfungia kilo moja moja je atabebaje kama hana kibebeo? Mteja anakuja kununua soda 4 utamfungia kwenye gazeti?
 
Vuta picha unanunua samaki mfano sato , sangara waliohifadhiwa kwenye barafu. Halafu unawaweka kwenye hii mifuko ya serekali.
Sitaki kukumbuka mimi,
.
Kama unaenda kununua samaki chukuwa froil ile ambayo inatumika kufungia chakula weka samaki wako funga vizuri, tafuta mfuko wa sukari toa ile yandani nenda nayo tia samakiwako wakutosha weka kwamfuko hakuna atakae kuuliza ile si kibebeo ile nikifungashio kina kuja na sukari, vitu vidogo kama hivi visi kuumize akili
 
Ki ukweli ni shida ilaoi mfanyabiashara aweke na mifuko ya kuuza.ukisema akupe bure haiwezekani
Sikatai mtu kununua mfuko wa kubebea bidhaa.

Kuwa na vifungashio ni kitu ambacho lazima mfanya biashara awe nacho katika shughuli yake.

Haki yetu ya kuhudumiwa isiwe fursa mara mbili kwa mfanya biashara..
 
Apa nmenunua vitu vya elfu 50 wananiambia ninunue na mfuko..shenzy zao nmewaachia vitu vyao

Na hela pia umewaachia? Uweze kununua vitu vya elfu 50,000 ushindwe kununua mifuko ya 300 kwa 500 ambayo utaitumia tena tena? Au umevuta cha Arusha au unajishaua hujanunua vitu hata vya 100.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…