Mwifwa
JF-Expert Member
- Apr 3, 2017
- 46,863
- 122,083
Kila jambo lazima liwe na athari chanya au hasi.
Marufuku ya vifungashio vya mifuko ya plastiki inaendelea kuzua gumzo mtaani.
Vifungashio mbadala vilivyoingia mtaani havina ubora wowote kuanzia kuhimili kiasi fulani cha uzito, kubeba aina fulani ya bidhaa hasa zenye unyevu unyevu....
Wafanya biashara wadogo ambao ndio wauzaji wa mwisho wa bidhaa mbali mbali za kila aina(hapa naomba tuweke bidhaa za vyakula), wamepigwa na butwaa hawajui hili wala lile juu ya mbadala bora wautumie katika biashara zao wakati wa kuhudumia mteja.
Unaenda kununua mathalani matunda unamwambia nifungie, anabaki anakukodolea macho(hana kifungashio) akitarajia mteja uwe na kifungashio ubebe bidhaa yako uliyonunua huku akisahau kuwa kumfungia mteja bidhaa ni haki yake...
Utafanyaje biashara huna vitendea kazi...? Wateja wakigoma kununua bidhaa zako kisa umeshindwa kuwafungia, hasara ni ya nani.?
Katika biashara lazima upambane na hali yoyote ile ili uweze kufanikiwa katika biashara yako...
Wafanya biashara wadogo tafuteni vifungashio mbadala hata kama hamtaki kutumia vifungashio vilivyoingia mtaani. Hata magazeti kama mnashindwa kununua ili muweze kutimiza haki ya mteja ya kufungiwa bidhaa..?
Serikali ishafanya yake na sidhani kama walifikiria adha zitakazojitokeza katika biashara zenu, imetimiza dhamira yake. Kilichobaki ni ninyi kupambana na hali zetu huku mkiendelea kujiepusha na mkono wake juu ya sheria na kanuni iliyozisimika.