Kumekucha:Wananchi wazinduka kuikabili Boko Haram

Kumekucha:Wananchi wazinduka kuikabili Boko Haram

luhala

JF-Expert Member
Joined
Feb 25, 2012
Posts
412
Reaction score
142
Kuna taarifa kwamba wanajeshi wa Nigeria sasa wanawastukia makamanda wao wanaoshukiwa kuwa na uswahiba na Boko Haram na kumkosakosa mmoja wa makamanda wanafiki. Wananchi pia wameanzisha vikundi vyao vya kujihami dhidi ya majambazi hawa.
Habari zaidi zinasema wananchi wa vijiji vitatu hivi karibuni "waliwachangamkia" maharamia hawa na kuangamiza 200 kati yao.
Kama habari hii ni kweli basi mapambano dhidi ya wahalifu hawa ni magumu kutokana na ukweli kwamba kundi hili haramu limejipenyeza hadi ndani ya Jeshi la nchi hiyo na mbaya zaidi hadi ndani ya safu ya viongozi waandamizi wanaoonekana kuvuruga mipango ya Jeshi katika kupambana nao.
Haiingii akilini kabisa kuona Jeshi la nchi hiyo limeshindwa kuua idadi hiyo ya magaidi hawa wakati wanavijiji tu wameweza! Kama hili ni sahihi siku za Boko Haram kuendelea "kutanua" zinahesabika kwani hakuna nguvu zinazoweza kuushinda umma ulioungana.

================================================

Wanajeshi nchini Nigeria, wamemfyatulia risasi kamanda wao mkuu katika mji wa Maiduguri Kaskazini Mashariki mwa nchi.
Hata hivyo Meja Jenerali, Ahmed Mohammed alinusurika kifo. Shambulizi lilifanywa dhidi ya gari lake katika kambi ya jeshi ya Maimalari .

140514125524_ejercito_de_nigeria_304x171_ap.jpg

Wanajeshi hao walimlaumu kamanda kwa mauaji ya wanajeshi wenzao walioshambuliwa na kundi la Boko Haram na kuuawa.
Wakati huohuo, Rais wa Goodluck Jonathan amesema hayuko tayari kubadilishana wasichana miambili waliotekwa nyara na wapiganaji wa Boko Haram wanaozuiliwa katika magereza ya Nigeria.

140513071040_nigeria_304x171_reuters_nocredit.jpg

Wazazi wa wasichana waliotekwa nyara na Boko Haram
Waziri wa serikali awali alikuwa amesema kuwa maafisa wa utawala walikuwa tayari kwa mazungumzo na Boko Haram lakini Rais Goodluck Jonathan amesisitiza kwamba swala hilo halitazungumziwa.
"Amesisitiza kwamba hataongea na Boko Haram kuhusu kubadilishana wasichana waliotekwa na wapiganaji wa kundi hilo wanaozuiliwa nchini humo," alisema mwakilishi wa serikali ya Uingereza Mark Simmonds baada ya kukutana na Rais Jonathan kujadili namna ya kuwanusuru wasichana hao.
Hatua ya kutekwa nyara kwa wasichana hao katika jimbo la Borno tarehe 14 Aprili, imesababisha kero kubwa kwa jamii ya kimataifa kiasi cha kulazimisha baadhi ya nchi za kutoa wataalamu kusaidia serikali ya Nigeria kuwatafuta wasichana hao.


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Na sisi watanzania tupeleke kikosi, wenzetu Zimbabwe wako mbioni kuelekea Naija
 
Ukiona kikundi Fulani cha wahalifu kinadumu ujue kuna watawala/wanausalama wanakisupport.

Ukiona kuna series Fulani ya halifu na haikomi, ujue kuna watawala wanapata faida nacho.

Dunia hii kwa sasa, bila kumwaga damu za watu, watu hawakai madarakani!
 
Wananchi kuuwa wanajeshi 200 wa boko haram sio kweli ila wameua watu 200 ambao ni wanahisiwa Kuwa mashabiki au ukaribu na boko.

Sent from my BlackBerry 9380 using JamiiForums
 
Hao Boko Haram walikuwa wamebeba rula (ruller)? wakati wao 200 wanauliwa wao walikuwa wanawatazama macho tu?

Semeni kweli kama mmeshawaua Waislam 200 wasiokuwa na hatia na mnaona mje kwa gia ya Boko Haram.
 
Labda uanze kwanza na Uamsho huko Zanzibar.
Hivi kwanini manapenda sana vurugu za kidini?

Wewe unafikiri yanayotokea Central African Republic ni kitu cha kufurahia?!

Chokochoko za chini chini kama hizi ndio zinazoleta chuki za kidini, halafu matokeo yake wanakuja poteza maisha au kujeruhiwa wasio na hatia.

Unajua hakuna kitu kibaya kama vita za kidini au kikabila, sasa wewe acha chuki binafsi zisizo na msingi na uangalie mpango wako

Jiangalie utakuja Rigwa
 
Hao Boko Haram walikuwa wamebeba rula (ruller)? wakati wao 200 wanauliwa wao walikuwa wanawatazama macho tu?

Semeni kweli kama mmeshawaua Waislam 200 wasiokuwa na hatia na mnaona mje kwa gia ya Boko Haram.

Knowledge Under Mental Application
 
Kama kutakuwa na boko haramu wa kike atayekamatwa wakat wa uokoz wa mabint walotekwa,m ntamwomba niish nae japo nimfunze kulost kitmoto kwa nguvu,ili kaka zake wajifunze jinsi ya kueheshimu madada wa watu wengne
 
Back
Top Bottom