LAMBOFGOD
JF-Expert Member
- Aug 12, 2016
- 1,561
- 1,315
Jimbo katolik Moshi na Arusha laazimia kuondoa kikwazo cha mahali kwa vijana wengi wanaoshindwa kufunga ndoa zao kwa kutozwa mahali kubwa kubwa na wazazi wa mabinti hivyo kuwafanya wawili hao kuendelea kuwa wachumba sugu na wazinzi wazoefu aidha waumini wametakiwa kuondokana na mila zilizopitwa na wakati za kuwatoza mahali vijana wanapotaka kuanzisha familia kwani huo ndio wito wa kwanza mwanadamu kuitwa kule bustanini eden, kwani kufanya hivyo ni kukatili mpango wa Mungu wa kuzaa na kuongezeka. Waumini wametakiwa kutokuchukulia maanani swala la mahali kwani haiwafanyi wapendanao hao kudumu katika upendo wao kwenye maisha ya ndoa yaliyojaa njia panda zinazohitaji maamuzi na machaguzi sahihi ili kuzivuka kwani yule mwovu huvizia katika dhoruba za njia panda kuwatia vishawishini. Mahali kwa wazazi imetakiwa kuchukuliwa kama zawadi za kawaida kabisa kulinganisha na udugu huo mpya unaoanzishwa
Mengi tu yalizungumuzwa ila haya machache nimewafikishia.
Karibuni kuoa/kuolewa moshi na arusha kwani sisi hatuangalii tena mahali ila kuwasaidia kudumu katika ndoa zenu ambazo ni paradise ndogo hapa duniani wala si ndoano kama wengi wanavyozichukulia
NAWASILISHA