Kumekucha: Iran yaunda Kombora la hypersonic

kimsboy

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2016
Posts
11,190
Reaction score
24,620
Iran yaunda kombora la balestiki la Hypersonic
Hawa jamaa Marekani alishachelewa kuwadhibiti mapema hii ndo funga kazi

Kamanda wa Kikosi cha Anga za Mbali cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu IRGC ametangaza kuwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imefanikiwa kuzalisha kombora la balestiki la Hypersonic, lenye uwezo wa kupenya mifumo yote ya ngao ya ulinzi wa makombora duniani.

Brigedia Jenerali Amir Ali Hajizadeh ameyasema hayo leo Alkhamisi pambizoni mwa maadhimisho ya miaka 11, tangu kufariki dunia Hassan Tehrani Moqadam, 'Baba wa sekta ya makombora ya Iran.'

Brigedia Jenerali Hajizadeh ameeleza kuwa, kombora hilo jipya la balestiki la Hypersonic lililoundwa kikamilifu na wataalamu wa Iran, mbali na kuwa na uwezo wa kupenya mifumo ya kisasa ya kutungua makombora, lakini lina uwezo mkubwa wa kupiga shabaha kwa usahihi mkubwa.

Amebainisha kuwa, kombora hilo lina kasi kubwa na uwezo wa aina yake, na kwamba hakuna teknolojia yoyote duniani inayoweza kulitungua hata katika kipindi cha miongo kadhaa ijayo.

Kamanda wa Kikosi cha Anga za Mbali cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ameeleza bayana kuwa, "Kwa miaka mingi, tumekuwa tukiendeleza shughuli zetu katika anga za mbali chini ya vikwazo shadidi na vya kikatili, lakini leo hii tumefanikiwa kuzalisha kombora la kisasa kabisa la balestiki la Hypersonic."

Jenerali Hajizadeh ameongeza kuwa, kombora hilo jipya lina uwezo wa kupiga mifumo ya kupambana na makombora ya maadui, na kwamba uzalishaji wake umefungua ukurasa mpya na ni hatua kubwa kuelekea kwenye uzalishaji wa makombora ya kizazi kipya hapa nchini.

Jamhuri ya Kiislamu ya Iran sasa imejiunga na nchi chache duniani zenye teknolojia ya kutengeneza makombora ya aina hiyo ya Hypersonic yenye kasi zaidi ya sauti; ambazo ni Russia, China, Korea Kaskazini na Marekani.

[https://media]Kombora la Hypersonic lenye kasi ya ajabu zaidi ya sauti

Hii ni katika hali ambayo, Jumapili iliyopita, Wizara ya Ulinzi ya Iran ilizindua mfumo mpya wa makombora ya kujihami ya masafa marefu ya Bavar (Kujiamini) 373 na pia kulifanyia majarbio kombora jipya la Sayyad B4.

Kabla ya hapo, Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu la Iran (IRGC) lilizindua kwa mafanikio roketi la kubebea satalaiti la Qaem-100 katika anga za mbali. Iran imepiga hatua na kupata mafanikio haya yote katika sekta ya makombora, mifumo ya ulinzi na anga za mbali licha ya vikwazo vya kidhalimu na mashinikizo ya maadui wa taifa hili.

4c0wf265344e9a24s4t_800C450.jpg
 
Brigedia General Amir Ali Hajizadeh.

"Jenerali Hajizadeh ameongeza Amebainisha kuwa, kombora hilo lina kasi kubwa na uwezo wa aina yake, na kwamba hakuna teknolojia yoyote duniani inayoweza kulitungua hata katika kipindi cha miongo kadhaa ijayo." Mwisho wa kunukuu.

Niliposoma hapo iikanibidi niishie hapo hapo, mlioendelea kuisoma hiyo hadithi tafadhali niambieni simulizi ilikuwa inaendeleaje?
 
KAMIKAZE zimeiacha Uikrane haina umeme Wala maji,,,,Leo tena balestiki[emoji15][emoji15][emoji15]
 
Iran yaunda kombora la balestiki la Hypersonic
Hawa jamaa Marekani alishachelewa kuwadhibiti mapema hii ndo funga kazi

Kamanda wa Kikosi cha Anga za Mbali cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu IRGC ametangaza kuwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imefanikiwa kuzalisha kombora la balestiki la Hypersonic, lenye uwezo wa kupenya mifumo yote ya ngao ya ulinzi wa makombora duniani.

Brigedia Jenerali Amir Ali Hajizadeh ameyasema hayo leo Alkhamisi pambizoni mwa maadhimisho ya miaka 11, tangu kufariki dunia Hassan Tehrani Moqadam, 'Baba wa sekta ya makombora ya Iran.'

Brigedia Jenerali Hajizadeh ameeleza kuwa, kombora hilo jipya la balestiki la Hypersonic lililoundwa kikamilifu na wataalamu wa Iran, mbali na kuwa na uwezo wa kupenya mifumo ya kisasa ya kutungua makombora, lakini lina uwezo mkubwa wa kupiga shabaha kwa usahihi mkubwa.

Amebainisha kuwa, kombora hilo lina kasi kubwa na uwezo wa aina yake, na kwamba hakuna teknolojia yoyote duniani inayoweza kulitungua hata katika kipindi cha miongo kadhaa ijayo.

Kamanda wa Kikosi cha Anga za Mbali cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ameeleza bayana kuwa, "Kwa miaka mingi, tumekuwa tukiendeleza shughuli zetu katika anga za mbali chini ya vikwazo shadidi na vya kikatili, lakini leo hii tumefanikiwa kuzalisha kombora la kisasa kabisa la balestiki la Hypersonic."

Jenerali Hajizadeh ameongeza kuwa, kombora hilo jipya lina uwezo wa kupiga mifumo ya kupambana na makombora ya maadui, na kwamba uzalishaji wake umefungua ukurasa mpya na ni hatua kubwa kuelekea kwenye uzalishaji wa makombora ya kizazi kipya hapa nchini.

Jamhuri ya Kiislamu ya Iran sasa imejiunga na nchi chache duniani zenye teknolojia ya kutengeneza makombora ya aina hiyo ya Hypersonic yenye kasi zaidi ya sauti; ambazo ni Russia, China, Korea Kaskazini na Marekani.

[https://media]Kombora la Hypersonic lenye kasi ya ajabu zaidi ya sauti

Hii ni katika hali ambayo, Jumapili iliyopita, Wizara ya Ulinzi ya Iran ilizindua mfumo mpya wa makombora ya kujihami ya masafa marefu ya Bavar (Kujiamini) 373 na pia kulifanyia majarbio kombora jipya la Sayyad B4.

Kabla ya hapo, Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu la Iran (IRGC) lilizindua kwa mafanikio roketi la kubebea satalaiti la Qaem-100 katika anga za mbali. Iran imepiga hatua na kupata mafanikio haya yote katika sekta ya makombora, mifumo ya ulinzi na anga za mbali licha ya vikwazo vya kidhalimu na mashinikizo ya maadui wa taifa hili.

View attachment 2415234
Hawa jamaa si ndio walikuwa na general wao sijui mkuu wa majeshi aliitwa sijui nani selemani alitunguliwaga then wakajambisha kurusha vijikombora vyao sijui ilizimwa Vipi... Anyway ila jamaa Nahisi kama ni mikwara tu Kama kiduku
 
Kombora la Hypersonic lishatoka sokoni urusi ilijaribu kutumia Ukraine kuangusha majengo lakini likadhibitiwa na mnyama US sasa kutuletea habari za Iran yeye ndo kwanza anaunda sijui ata tuseme nn
Tuache kupotosha Russia haijawahi kutumia Hypersonic japo inalimiliki mengi tusipotoshe hapa la kuuliza to source ya hizi habari je Iran ni kweli anayo?
 
Nikiskia Iran Wana hypersonic missile Wala sitashangaa. Wametoka mbaali Sana katika hatua hizi za kujikwamua kutoka kuwa nchi inayoagiza kila kitu Kama silaha nzito na leo kufikia nchi inayojitengenezea silaha nzito na kuziuza

Sent from my TECNO RA7 using JamiiForums mobile app
 
Hawa jamaa si ndio walikuwa na general wao sijui mkuu wa majeshi aliitwa sijui nani selemani alitunguliwaga then wakajambisha kurusha vijikombora vyao sijui ilizimwa Vipi... Anyway ila jamaa Nahisi kama ni mikwara tu Kama kiduku
Unaita vijikombora wakati Kambi ya USA ilibaki jivu tupu na trump akaishia kulia lia wakati alisema Iran akishambulia atamshambumlia na yy lakini kapgwa hata kurusha risasi tehrani ameshindwa,Kambi hzo hapo kasaidie kujenga upya.
Screenshot_20221113-174843.jpg
View attachment 2415605
 
Kombora la kutisha ni NUKE tu haya mengine hayawezi kukufanya ushinde Vita! Kombora lenyewe ni kwa ajili ya Targets zisizo tembea Kama majumba, madaraja na mengineyo. Russia kayajaribu pale Ukrein kupiga kambi lakini hajaona maajabu kaamua kuyapotezea. Sijui unahitaji kurusha mangapi ili kuangamiza mji mmoja tu wa USA
 
Back
Top Bottom