Pole mkuu, naona unatetea ugali, ila in a mattee of time, ikishaingia kwenye social circle ikaeleweka mtaelewa maana yake.Hivi nani aliyewafukuza bungeni?
Unajua mkifanyacho ni kama wenza waliotengana na mmoja kaenda kwao. Anakaa siku alizotegemea mwenzie lazima amrudie zinapita anarudi na kufanya kitimbi kingine kama alimuacha mtoto anamrudia na kuondoka naye. Bado anaona arejewi anarudi kudai vyombo. Bado arejewi wala ndugu hawaingilii anashitaki ustawi wa jamii. Bado arejewi antishia kunywa sumu. Bado arejewi sana anataka kuchoma nyumba moto.
Kuishi katika ndoa unataka vitimbi vya nini? Hiki chama cha watoa matamko hawana akili. Mtu wa kumtolea matamko ni nani hasa? Mh Magufuli? Kweli viroba vibaya. Hapa ni kazi tu mmelikoroga kunyweni wenyewe. Waambieni hao wakosa adabu wenu huko bungeni waache ujinga warudi wafanyekazi.
Hivi wanachotaka wafanyweje hasa? Semeni, kwani hakuna amri ya NS kuwafukuzeni. Ndio maana inakuwa ngumu viongozi wa dini na wazee wenyekuheshimika sana humu nchini kuliingilia. Nyie ndio waathirika nyinyi ndio wasababisha uathirika wenu na uwezo wa kuacha vitendo vya kujiathiri mnao wanashindwa waingie wapi kuwasaidia.
Huenda huu ujinga waliouamua huwa unauraibu kiasi kwamba mtu hushindwa kujiondoa mwenyewe. Waseme basi kuwa wamekuwa mateja wa kutoka nje ili waanzekutumia dawa ya kuondokana na huo ujinga.
Unamsemea na Nani hapo?labda familia yako tuUZURI ni kwamba WATANZANIA hatujafikia level hii ya kufanya MAIGIZO mnayotaka tufanye..afu MKAE MJUE vyama vya SIASA SI DINI ZETU wala MAKABILA YETU kiasi kwamba inaweza tenganisha umoja wetu.....NA KATIKA HILI MNAJIDANGANYA maana CDM haina ushawishi wowote kwa WATANZANIA kwa kipindi hichi ambacho WATANZANIA wote tunamuona MAGUFULI NDIO MKOMBOZI WETU.....kuthibitisha hili tuone kama mtafanikiwa mnachotaka kukifanya.....
AFU na nyie BAVICHA ebu mtuambie TOKEA huu mwaka umeanza mmeisha toa matamko mangapi juu ya SERIKALI HII na JE MAFANIKIO yenu juu ya HAYA MATAMKO ni yepi???...EBU TUPENI MREJESHO ili tuwasapoti katika hili....MAANA TUMEISHA WACHOKA NA MATAMKO YENU YA SIYO KUA NA KICHWA WALA MIGUU
Hiyo misuguano yenu isije kutusumbua tusiokuwa na kadi,maana mmeshajiona sasa ndio wenye nchi wakati watanzania zaidi ya million 30 hawazijui hata kadi za vyama.
Hapa natoa darasa ili tupunguze wajinga. Wewe huenda umeelewa. Ndio ninavyopunguza wajinga hivyo.Pole mkuu, naona unatetea ugali, ila in a mattee of time, ikishaingia kwenye social circle ikaeleweka mtaelewa maana yake.
Siasa ina nguvu sana hapa duniani na kwa jamii, busara ni muhimu, udongo uwah ungal maji
MAMBO yanazidi kwenda mrama kati ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA), anaandika Dani Tibason. Msimamo uliotolewa na Baraza la Vijana wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (BAVICHA) unaakisi mwanzo mpya wa msuguano wa kisiasa nchini.
Tayari BAVICHA wametangaza msimamo wa kutoshirikiana na vijana wa CCM katika tukio la aina yoyote. Mbali na kutangaza msimamo huo pia wametangaza kuzuia mikutano yote ambayo itaandaliwa na CCM kama inavyozuiwa ya CHADEMA.
Msimamo huo umetolewa leo na Julius Mwita, Katibu Mkuu wa BAVICHA wakati akizungumza na waandishi wa habari Dodoma.
Mwita amesema, kutokana na kitendo cha Serikali ya CCM kushirikiana na Jeshi la Polisi kuzuia mikutano ya Chadema kinaonesha wazi kuwa, serikali ina mpango wa kuhakikisha inaua upinzani jambo ambalo haliwezi kukubalika.
Amesema, kutokana na hali hiyo kwa sasa BAVICHA wametangaza kutoshirikiana na vijana wa CCM katika mazingira yoyote ikiwa ni pamoja na katika masomo, nyumba walizopanga, misiba na katika majamga mengine mbalimbali.
“Kutokana na kuwepo kwa vitendo vya kikatili vinavyofanywa na Serikali ya CCM vya kuzuia mikutano ya upinzani, sasa tunatangaza sisi vijana wa Bavicha hatutashirikiana na wanachama wa CCM kwa njia yoyote ya kijamii wala kimaendeleo.
“Natangaza kwa vijana wote wa CHADEMA hatutashiriki katika mazizi, hatutashiriki kusoma nao wale waliopo katika vyuo, hatutashiriki sherehe mbalimbali zinazowahusu wao wala hatutashiriki katika jambo lolote la kimaendeleo, na hii ni msimamo wetu.
“Pia tunawapongeza wabunge wetu kwa kususia shughuli zote za ambazo zinafanywa na CCM kwani kwa kufanya hivyo inaonesha kuwa sasa tumechoka na uongozi wa kiimla,” amesema Mwita.
Hata hivyo amedai, Rais John Magufuli ni muoga kuliko marais wote kwa kuwa ni rais ambaye hapendi kukosolewa na kuambiwa ukweli pale ambao amekuwa akikosea jambo ambalo anatakiwa kujitafakari na kujikosoa.
“Sasa vijana vijana tumejipanga kuhakikisha Jeshi la Polisi linazuia mikutano au mikusanyiko ambayo inafanywa na CCM na ikumbukwe kuwa, 23 Julai mwaka huu CCM watakuwa na vikao vya kumkabidhi rais Magufuli kuwa mwenyekiti wa CCM.
“Sasa tunataka Jeshi la Polisi kuzuia mkusanyiko huo na kama haitawezekana vijana wa CHADEMA na UKAWA watazui mikutano hiyo.
“Haiwezekani mikutano ya CHADEMA ikawa ndiyo inayozuiliwa wakati mikutano na mikusanyiko ya CCM inaendelea kufanyika, jambo hili kamwe haiwezi kukubalika na tunasema sasa imefika mwisho wa uvumilivu,” amesema Mwita.
Edward Simbeye, Katibu Mwenezi BAVICHA amesema, yeye ndiye mratibu wa mahafali za wanafunzi wa CHADEMA vyuo vikuu (Chaso) nchini hivyo polisi walipaswa kumkamate yeye na si kuzuia mahafali hayo.
hakuna dhambi mbaya kama unafki.Sijui kama inawezekana
[emoji13] [emoji2] [emoji2] [emoji2] nimeipenda hiii...Inanikumbusha Pemba kuna mnunuzi wa samaki ambae ni kada wa CCM kwenye mnada wa samaki alifika bei ya 170,000 kwa tenga na kufaninikiwa kushinda .Lakini mchuuzi akamwuzia mnunuzi aliefika bei ya 70,000 ambae ni kada wa CUF mwenzie.
Kada wa CCM alipohoji nae akajibiwa na yule mchuuzi wa CUF kwamba mbona na sisi tukishinda uchaguzi hatupewi madaraka
Umeongea kama nilivyokuwa nawaza......True storyMbuyu huanza kama mchicha. Huku tunakoelekea na ugumu huu wa maisha usishangae kupata support kubwa ya watu. Mpaka sasa bado Magufuli hajafanya kile watanzania walichotarajia zaidi ya hadithi ya majipu. Sasa hivi ukimsifia Magu huoni watu wengi wakisupport kama ilivyokuwa miezi mitatu ya mwanzo, sasa hivi ni kama watu wamepoteana wanangoja tu mawazo mbadala ili rasmi wamtoe maanani. Kama ugali mezani unakuja kwa shida hata utoe ahadi gani itakuwa ngumu kuungwa mkono, sana sana wananchi wataingiwa tu na hofu dhidi ya dola ila sio kukufurahia. Fanya utafiti wa kutosha, wanaosifia wamebaki wanaccm tena kwa unafiki lakini kwa ugumu huu wa maisha hata hiyo pumzi ya kusifia inaanza kukata.
Na hao Bavicha nani ata wawasemee watanzania au siku hizi vijikundi vya siasa vina power ya kuwasemea watanzania? kuwa kimawazo wewe dogo.Huo ndio msimamo wa bavicha, upende husipende na watu tupo tayari kujiunga na ushauri wao, we nani hadi unawasemea watanzania?
UZURI ni kwamba WATANZANIA hatujafikia level hii ya kufanya MAIGIZO mnayotaka tufanye..afu MKAE MJUE vyama vya SIASA SI DINI ZETU wala MAKABILA YETU kiasi kwamba inaweza tenganisha umoja wetu.....NA KATIKA HILI MNAJIDANGANYA maana CDM haina ushawishi wowote kwa WATANZANIA kwa kipindi hichi ambacho WATANZANIA wote tunamuona MAGUFULI NDIO MKOMBOZI WETU.....kuthibitisha hili tuone kama mtafanikiwa mnachotaka kukifanya.....
AFU na nyie BAVICHA ebu mtuambie TOKEA huu mwaka umeanza mmeisha toa matamko mangapi juu ya SERIKALI HII na JE MAFANIKIO yenu juu ya HAYA MATAMKO ni yepi???...EBU TUPENI MREJESHO ili tuwasapoti katika hili....MAANA TUMEISHA WACHOKA NA MATAMKO YENU YA SIYO KUA NA KICHWA WALA MIGUU