Kumekucha Bungeni - PICHA za wabunge wapya wakiwa Dodoma

Status
Not open for further replies.

Lucchese DeCavalcante

JF-Expert Member
Jan 10, 2009
5,471
734



Mbunge wa Jimbo la Urambo mashariki Samwel Sitta akisalimiana na Mbunge wa Same Mashariki Anna Kilango.


Samwel Sitta Mbunge wa Jimbo la Urambo Mashariki na Spika wa bunge lililopita ambaye pia anagombea nafasi hiyo tena mwaka huu akipongezana na Mbunge kijana wa jimbo la Kawe HalmaMdee katika viwanja vya Bunge

JAMAAANI BUNGENI: Wabunge CCM kupitia viti maalum Vicky Kamata, akiwa na mwenzake katika ofisi za bunge leo ndio vijana hawa wa bunge.


Joseph Mbilinyi mhasisi wa bongo foreva aka Mr II akiwa katika pozi nje ya mjengo wa bunge baadhi ya watu walisema kuwa hataweza lakini mvua ya ushindi wa kura alizopata kutaka kwa wananchi wa jimbo la Mbeya mjini ndizo zilizowakata ngebe wabaya wake.


Aliyekuwa mgombea wa urais kupitia chama cha CHADEMA Dr,Willibrod Slaa akisalimiana na baadhi ya wabunge katika jengo la bunge leo jijini Dodoma baada ya kuwasili katika mkutano na wabunge wake leo mchana. Katikati ni mheshimiwa mbunge Dr. Hassani Mwinyi.​


Mwenyekiti wa Chadema na Mbunge wa jimbo la Hai Freeman Mbowe akijisajili katika ofisi za bunge leo huku Afisa wa Bunge Asia Poul Minja akishuhudia.

Sugu akiongea na wandishi wa habari katika eneo la Bunge leo , aliwaambia waandishi kuwa kuja bungeni ni kama anakuja kuanza Form I lakini baada ya kuwakuta makamanda wa habari aliofarijika sana.



Haya wenje na Highness na Mkosamali mjengoni

Waandishi mbali mbali wakiteta kiutani na mheshimiwa mbunge wa Mbeya mjini Jospeph Mbilinyi

Mheshimiwa Raisi Jakaya Mrisho Kikwete akikaribishwa Dodoma na watoto walifika kumlaki

Mheshimiwa Augustino lyatonga Mrema akijaza foem za usajili bungeni jana, nani kasema mzee kachoka??


Naomba kuwakilisha wakuu.. Aaah sio wakielekea Dodoma bali wakitinga mjengoni...
 

Attachments

  • DSC_0242.JPG
    34.3 KB · Views: 4,930
  • DSC_0359.JPG
    58.8 KB · Views: 5,255
  • DSC_0028.JPG
    68.9 KB · Views: 1,198
  • DSC_0208.JPG
    45.8 KB · Views: 1,112
  • DSC_0032.JPG
    55.1 KB · Views: 4,878
  • DSC_0217.JPG
    44.6 KB · Views: 3,816
  • DSC_0291.JPG
    40.6 KB · Views: 1,287
  • DSC_0919.JPG
    62.4 KB · Views: 4,405
  • Picha no 3.JPG
    47.9 KB · Views: 3,797
  • GO9G7576.jpg
    76.2 KB · Views: 3,765
  • Picha no 5.JPG
    62.7 KB · Views: 3,710

[/CENTER]
JAMAAANI BUNGENI :Wabunge ccm kupitia viti maalum Vicky Kamata, akiwa na mwenzake katika ofisi za bunge leo ndio vijana hawa wa bunge. Mie sisema maana picha zinajionyesha zenyewe bunge la mwaka huu balaaa
Hivi huyu mbunge mwingine upande wa kulia kwa Vicky Kamata ndio nani wajamani?
 
Hivi na hizi chain za miguuni zinaruhusiwa kama vazi rasmi la BUNGENI bora sijachaguliwa najihisi kubaka vile.
 
Ndio maana CHADEMA walisema viti maalumu si pahala pakupeleka watu wasio na staha, ona nini sasa.

 
Hivi ni pamoja na wale waliopita bila kuchaguliwa, maana katika Katiba ya sasa ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hakuna wabunge wa aina hiyo. Au wana JF wakereketwa mnasemaje yaani tuwaache wapete hivi hivi?? NOOOOOOOOOOOOO!!!!!!!!!!!! Mpaka kieleweke!!!!!!
 
Hahahahah! mi sisemi kitu, ila naomba bunge lisiishe ili tuanze upya uchaguzi kabla hata ya bajeti ijayo mwakani. Naimani na hayo maneno, maana kuna kila dalili za kuvunja bunge ndani ya miezi michache ijayo kama Dr Slaa ataamua kuwakaba koo kiukweli.
 

i agreee...Huyu mzee ni makini sanaaaaaa katika mambo ya msingi..mi nina mashaka na mustakabali wa taifa hili mara pale atakapozungumzia uchakachuaji wa kura uliofanya na MAJIZI ccm
 

Hii bila kuiwekea maelezo ingeleta maswali sana vichwani...(ni maoni yangu tu, nasikia wazee huwa wanalea sana!)
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…