Kumekucha Bodi ya Filamu Tanzania

Kumekucha Bodi ya Filamu Tanzania

Joined
Aug 12, 2011
Posts
7,150
Reaction score
14,724
1. PINDI CHANA.jpg
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangara amemteua Mheshimiwa Pindi Chana kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Filamu na Michezo ya kuigiza katika kipindi cha miaka mitatu ijayo. Uteuzi huu unatokana na Mamlaka aliyopewa Waziri huyo chini ya kifungu cha 13(i) cha Sheria ya Filamu na Michezo ya kuigiza Na.4. ya mwaka 1976.

Bishop_Hiluka_2.jpg

Kwa mujibu wa taarifa ya Wizara hiyo kwa Vyombo vya habari uteuzi wa Mwenyekiti na Wajumbe wengine wa Bodi umeanza tarehe 3 Desemba 2013. Aidha Waziri huyo amewateua Wakili wa Kujitegemea Silvester Sengerema, Dr. Vicensia Shule kutoka Chuo Kikuu cha Dar es salaam na Bishop Hiluka kutoka Shirikisho la Filamu Tanzania kuwa wajumbe wa Bodi hiyo katika kipindi cha miaka mitatu ijayo.

Wajumbe wengine ni Jacob Sarungi kutoka Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Ntobi Fredrick kutoka Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania, na Joyce Fissoo ambaye ni Katibu wa Bodi ya Filamu.
 

Attachments

  • Bishop_Hiluka_2.jpg
    Bishop_Hiluka_2.jpg
    416.9 KB · Views: 154
  • Bishop_Hiluka_1.jpg
    Bishop_Hiluka_1.jpg
    520.4 KB · Views: 146
  • Bishop_Hiluka_2.jpg
    Bishop_Hiluka_2.jpg
    45.3 KB · Views: 157
kumbe pindi chana ni mwanamke, nlikuwa nkisikia jina hili nadhan mwanaume.....
 
kumbe pindi chana ni mwanamke, nlikuwa nkisikia jina hili nadhan mwanaume.....
Mkuu,
Ni kama hio avatar yako kwa haraka-haraka unadhani wenzako humu tunajua wewe ni gender gani?:wink2:
 
anza kufurahia wewe ndio utakuwa mwenyekiti mteule sasa
Duh, hata sioti ndoto hiyo, hii nafasi ya ujumbe tu sikuitarajia.
Hata hivyo nina taarifa rasmi kuwa Waziri Dk. Fenella Mukangara
anajiandaa kuteua mwenyekiti mwingine wa bodi baada ya huyu
kuukwaa Unaibu waziri...
 
Back
Top Bottom