Naombeni ushauri kama ni sahihi
Nilikuwa na rafiki wangu wa kiume ambaye tuliachana zaidi ya mwaka mmoja uliopita. sasa wakati tukiwa kwenye mahusiano yeye alikuwa chuo anasoma ila alikuwa ameajiriwa na mimi nilikuwa nimeajiriwa. kwa kuwa tulikuwa na mipango mingi ya kimaisha nilikuwa mamshirikisha mipango yangu naye ananishirikisha ya kwake. kuna kipindi nikawa nimefunga biashara yangu na fedha ikawa ipo tu benki sasa akaniambia kwa kuwa hufanyi biashara kwa sasa nipe hiyo fedha niongezee kwenye biashara yangu then ukishafikiria biashara ya kufanya nitakupa fedha yako, mimi nikampa hiyo fedha. ila baada ya kumaliza chuo na kurudi kazini kwake mawasiliano nami yakaanza kupungua na baada ya muda tukawa tumeachana ila hakukuwa na sababu ya msingi ya yeye kuachana na mimi ila akaniambia usijali fedha yako nitakupa sitakurusha. baada ya hapo akanipa asilimia 75% ya hiyo fedha. nilipomuambia kiasi kilichobaki akawa hapokei simu na hata siku moja akampa mwanamke simu anitukane.nilipata maumivu sana sijui kama nilikosea kudai fedha yangu au nilitakiwa nisimdai kwani makubaliano yalikuwa nikibuni biashara anipe fedha. ushauri maana tangu nitukanwe sijampigia tena simu.