Kumbukumbumbu ya Miaka 23 ya Kifo cha Baba Wa Taifa

Lady Whistledown

JF-Expert Member
Aug 2, 2021
1,024
1,611
Siku ya Leo Watanzania Duniani Kote wanaungana kuadhimisha Kumbukumbu ya Miaka 23 ya Kifo cha aliyekuwa Rais Wa Kwanza wa Tanganyika na Baadaye Tanzania, Mwalimu Julius K. Nyerere

Mwalimu Nyerere anaenziwa kwa mengi ikiwemo Falsafa yake ya Elimu ya Kujitegemea, Rushwa ni adui na Haki, Muungano wa Kitaifa pamoja na Umahiri, Ujasiri na Busara zake katika Kuongoza harakati za Uhuru wa Tanganyika kutoka kwa Waingereza Mwaka 1961
 
Hakika mwalimu alifanya Mambo mengi kwa maendeleo ya nchi yetu,Kwa uchache nilikuwa napitia ujenzi wa wa reli Tazara. Reli iliyojengwa kipindi nchi za Afrika zinapigania Uhuru wake, reli ilijenjwa kupambana na ukoloni;pia kuimarisha uchumi wetu.

Sina hakika nikwakiwango gani alipambana na nchi za magharibi kuhusiana na mambo ya mazingira.Yapo Mambo aliyoyafanya ni muhimu kuendelea kuyasimamia na kufundisha watoto wa kizazi hiki, wenzetu wachina walikuwa wanafundisha kwenye mashule yao umuhimu wa mradi wa reli ya Tazara, ulikuwa mradi wa kwanza mkubwa kuitambulisha China nje ya mipaka yao.
 
Kulitakiwa kuwe na 'Kambona day' ambayo mimi ningeisheherekea.

Nyerere aliua Elimu na Uchumi na ndie aliyetufikisha hapa tulipo.kwenye "Bora liende"
 
Nyerere alipinga kwa vitendo RUSHWA, Na yeye alikuwa adui namba moja wa RUSHWA ktk maisha yake yote!
RUSHWA ilizaliwa, ikalelewa na kukua hadi kuwa dude kubwa kabisa katika awamu zilizofuata hasa awamu za 3, 4, 5 na 6! RUSHWA imekuwa ni UJANJA ndani ya CCM.
 
Siku ya Leo Watanzania Duniani Kote wanaungana kuadhimisha Kumbukumbu ya Miaka 23 ya Kifo cha aliyekuwa Rais Wa Kwanza wa Tanganyika na Baadaye Tanzania, Mwalimu Julius K. Nyerere

Mwalimu Nyerere anaenziwa kwa mengi ikiwemo Falsafa yake ya Elimu ya Kujitegemea, Rushwa ni adui na Haki, Muungano wa Kitaifa pamoja na Umahiri, Ujasiri na Busara zake katika Kuongoza harakati za Uhuru wa Tanganyika kutoka kwa Waingereza Mwaka 1961
Nyerere alikuwa anakipenda zaidi Chama Cha Mapinduzi kuliko Tanzania.
 
Back
Top Bottom