Kumbukumbu za Maisha; Ulishapitia kazi ya 'Urumba'?

Wildlifer

JF-Expert Member
May 12, 2021
1,883
5,191
Kuna wakati nilirudi nyumba, sikua na kazi. Siku moja nikakutana na jamaa yangu alikuwa anafanya kazi Tumbaku, akaniambia kazi za ukarani wa tumbaku Zimeshajazwa, ila kuna kazi ya kubeba bales za Tumbaku (mabelo). Nikasema siwezi, tukaachana.

Jioni nikawaza, mimi ni mwili nyumba, ninapiga mazoezi daily, nashindwaje kubeba hizo 'belo'. Asubuhi nikamfuata jamaa, akafanya yake, baada ya siku 2 nikakabiziwa jezi 'ovaroli', nianze kazi. Nikawa rasmi ni Mrumba!

Nilianza mida ya saa 4 asubuhi, nikaungwa Kundi na 2, watu 9 mimi nikawa wa10. Ile nimefika, jamaa likasema "mkaribisheni". Nikainamishwa na kurushiwa belo. Halikuwa, zito. Nikasema, kazi ndogo. NILIJIDANGANYA. Ngoma zilizofuata hadi za kg 90.

Kazi ile niliifanya wiki mbili. Ilinitoa donda kubwa sana shingoni na kichwani. Pia hadi leo imeniachia maumivu kwenye pingili ya uti wa mgongo maeneo ya shingoni.

Niliichukia ile kazi sababu ya malipo kidogo, huna muda wa kufanya mambo mengine na pia lishe ilikuwa duni.

kuna mrumba hapa JF.?
 
Kazi ngumu zishuhudie wenzako wakizifanya lkn kama huna moyo wa uvumilivu lazima uzikimbie tu ukizingatia malipo yake muda mwingine huwa ni madogo sana.
 
Kazi ngumu zishuhudie wenzako wakizifanya lkn kama huna moyo wa uvumilivu lazima uzikimbie tu ukizingatia malipo yake muda mwingine huwa ni madogo sana.
Sure mzee. Shida kubwa ni malipo duni. Halafu, shida sio mzungu, shida ni sisi weusi wenyewe. Mzungu anatoa mara mbili ya hela tuliyokuwa tunapewa!
 
Back
Top Bottom