Kumbukumbu ya Ramadhani 4

Mohamed Said

JF-Expert Member
Nov 2, 2008
20,920
30,263
KUMBUKUMBU YA RAMADHANI 4
FUNGA YA ZIMBABWE 1993

Nimefunga Ramadhani Harare, mwaka wa 1993.
Naikumbuka safari hii vyema sana.

Nimepanda ndege ya alfajir ATC kuelekea Harare.

Uwanja wa ndege nimemkuta marehemu Dr. Buyuni Jahazi na yeye anaelekea Harare safari yetu moja.

Safari hii mimi na Dr. Jahazi ina mengi lakini In Shaa Allah hayo tutahadithiana siku nyingine ikitokea fursa.

Tulipofika Harare tunaelekea hotelini niko kwenye taxi moja na Dr. Jahazi nikamuomba dereva wa taxi anionyeshe msikiti na kusudio langu ni kuwa niwe nasali hapo sala ya tarwehe.

Tunazungumza Kiingereza na mimi namtajia ‘’mosque.’’

Ilipitika kazi labda kwa dakika mbili tatu dereva wa taxi hajaelewa ‘’mosque,’’ ni kitu gani wala neno ‘’masjid,’’ halikutusaidia kuelewana.

Nilipomwambia, ‘’the place where Muslims pray,’’ hapo haraka akanijibu, ‘’You mean Muslim church.’’

Hakika kusafiri peke yake ni elimu tosha.
Akanipitisha katikati ya mji wa Harare akanionyesha msikiti.

Mambo bado hayajesha.
Nimepanga Ambassador Hotel, hoteli nzuri lau ya zamani toka 1950s.

Baada ya siku mbili hivi Meneja wa hoteli akanitafuta na sababu ni kuwa alikuwa hanioni kwenye kifungua kinywa asubuhi.

Nikamfahamisha kuwa mimi nafunga mfugo wa Ramadhani.

Yule bwana akaniambia kuwa atawaagiza watu wa jiko kuwa jioni waliniletee futari chumbani kwangu, yaani ‘’room service,’’ yote, ‘’on the house,’’ ‘’zero cost’’ silipi kitu.

Chef akaelezwa kuwa anitengenezee chai, juice, mikate, nyama, salads na mapochopocho mengine kila siku jioni hadi nitakapoondoka hotelini baada ya majuma matatu.

Jioni ile wakati wa kufungua umefika nikapiga simu Room Service hata dakika tatu hazijapita nagongewa mlango msichana anaingia na tray imefunikwa vizuri kwa makawa yale ya ‘’silver,’’ makubwa maarufu kwa kufunika vyakula katika mahoteli makubwa.

Haraka yule bint akanifunulia.
Hakika ilikuwa futari iliyokidhi viwango.

Binti kasimama ananiangalia.
Mimi jicho langu liko kwenye sahani za vyakula.

Kuna nyama nimeiona pale sura yake sijaizoea.
Nikamwuliza hiyo ni nyama gani?

"What's this?"
‘’Bacon Sir.’’

‘’You mean pork?’’
‘’Yes Sir it is pork.’’

Mpishi kanitengenezea futari ya nyama ya nguruwe.

Siku ya pili asubuhi nikahama hoteli ile nikaenda hoteli nyingine inaitwa Holiday Inn.

Usidhani hii Holiday Inn ni ile ya Nyota Tano ya kimataifa.
Afrika tuna ujanja wetu na kwengine kwingi haya utayakuta.

Nimekuta Misri jina kubwa lakini si lile la kimataifa.
Hadi leo nikisafiri nikijua kuwa hoteli niliyofikia wanapika nguruwe nahama.

Wenyeji wakanionyesha restaurant nzuri sana ya Waismailia hapo ndipo nikawa nakwenda kufuturu.

Picha: Msikiti wa Harare.

1710433789066.png

1710433891742.png
 
Mkuu japo umesema ulihama hotel. Je bacon uliyoletewa uliila ama?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom