Kumbukumbu ya Ibrahim Rajab Juma "jeba" nani kama jeba!

Slim5

JF-Expert Member
Jan 7, 2014
28,108
37,643
Ibrahim Rajab Juma "JEBA" Mchezaji wa Zamani wa AZAM FC, Mtibwa FC na Chuoni FC aliefariki 18-9-2019 Unguja, Zanzibar!

JEBA pia aliwahi kuchezea timu ya Taifa ya Vijana. Jeba aliingia AZAM FC mwaka 2008 akiwa na kizazi cha Mudathir Yahya Abbas, kiungo fundi wa AZAM FC na National team.

Jeba amechezea Azam FC U14, U17 na U20 kuanzia 2008 na baadae akarudi nyumbano Unguja Kuchezea CHUONI kabla ya kuchukuliwa na Mtibwa 2014 - 2017!

Kutoka Mtibwa, Marehemu JEBA akarudi Unguja kwa hoja anahitaji kuwa karibu na familia!

Muda huu AZAM FC na Mtibwa FC wanacheza mechi ya hisani ktk uwanja wa AMANI, Mapato yote yataenda kwa familia yake baada ya kuondoa makato!

Katika mechi hii wachezaji wote wa AZAM FC wamevaa jezi namba 38 wakati wale wa Mtibwa wamevaa namba 22, zikiwa ni namba alizotumia marehemu JEBA wkt akihudumu ktk vilabu hivyo!

Ibrahim Rajab Juma "JEBA" Alizaliwa mwaka 1990!

RIP Jeba
 
Mwaka 2014 Dr. Mwankenda, tabibu wa Azam Fc aliwapa taarifa Wakurugenzi wa Azam Fc kuwa JEBA ana shida ktk moyo!

Uongozi wa Azam Fc ulimfahamisha JEBA na baadae kwenda kumkabidhi kwa wazazi wake Unguja (kumbuka JEBA alijoin Azam angali mdogo U14)

Azam Fc walimshauri JEBA na familia yake kuwa JEBA aachane na soka na kugeukia shughuli zingine!

Haieleweki nini kilitokea baada ya hapo lkn JEBA aliibukia CHUONI na muda mfupi akaenda Mtibwa!
 
kujiunga azam akiwa na miaka 14 halisi ya kuzaliwa ni uongo.
nina wasiwasi hata michuano ile ya copa coca cola under 17 waliobeba ubingwa mkoa wa mjini magharibi marehemu jeba alikuwepo kwenye kikosi
mara yangu ya kwanza kumuona jeba akicheza soka (ligi za ndondo maeneo ya magomeni) alikuwa ni kijana mwenye wastani wa miaka 22 kwenda juu na si kurudi chini.
 
[/QUOooh hii ni hatari
 
Wewe utakuwa sio Mwafrika. Africa marehemu hasemwi!

Back
Top Bottom