Kumbukizi ya miaka 4 ya ajali ya watoto wa Lucky Vincent iliyotokea Arusha mwaka 2017

Kasomi

JF-Expert Member
Sep 3, 2014
11,036
20,337
Simanzi na majonzi kutoka kwa wazazi, walimu na wanafunzi wa St Lucky Vincent katika kumbukumbu ya ajali iliyouwa watoto 32, walimu wawili na dereva mmoja mnamo Mei 6 2017.

Mamia ya watu walihudhuria katika ajali hiyo iliyo tokea mei 6,2017 katika wilaya ya Karatu mkoani Arusha ambayo iliibua majonzi kwa watanzania wote.

FB_IMG_16202791769835484.jpg

Hata hivyo macho ya wengi yalikuwa kwa manusura watatu ambao walitaja kuwa ni watoto wa miujiza.

Manusura hao ambao ni Doreen Elibariki, Wilson Tarimo na Sadia Awadh, kila mmoja kwa nafasi yake waliweza kutoa shukrani zao za dhati kwa huduma ya afya huko nchini Marekani na kupata ufadhili wa elimu nzuri ya sekondari.

Lakini kwa sasa Sadia yupo kidato cha nne.

Sadia mwenye umri wa miaka kumi na saba, mama ake anasema alipoteza kumbukumbu kwa muda baada ya ajali na kukiri kuwa alijikuta yuko nchi ya kigeni mara baada ya tukio hilo.

Aliongeza kuwa ana kila sababu ya kushukuru kwa kupata nafasi nyingine katika maisha.

''Sasa anaweza kukumbuka jinsi dereva alivyoshindwa kulihimili gari mpaka ajali ikatokea" alisimulia.

Hiyo ndio ilikuwa ajali ya watoto wa Lucky Vincent.

 
May their Soul Rest In Peace. Nakumbuka pia member mwenzetu humu alipoteza kijana wake hapo. Hatujawasahau malaika wale.

Tunawatakia maisha mema waliopona/walionusurika kwenye ajali hio.
 
ile mahali huwa napita mara kwa mara huwa nikiuona huo mnara nahisi kukosa utulivu kabisa.hunifanya moyo kuzidi mapigo isivyo kawaida.
mungu azidi kuwapa watoto hawa makazi ya janat firdaous
 
Lazaro Nyalandu : Rais Magufuli ndiyo alitoa vibali hao watoto wakatibiwe nje.
 
Back
Top Bottom