Kumbe "ZENJI" sio ya kitoto kabisa

Polycarp Mdemu

Senior Member
Jun 2, 2019
130
250
+ Katika Vitabu maarufu vya historia vinavyotolewa na "UNESCO World Heritage" kuna Makala ambazo huwa zinahusu orodha ya miji mikongwe ambayo mpaka leo inakaliwa na watu (List of oldest continuously inhabited cities) hapa utakutana na majina ya miji mingi ya kale japo mingine haikaliwi na watu lakini ipo inayokaliwa bado, ndio hupewa heshima katika makala hizi......

Katika nchi za Ocenia kuna mji unaitwa Sydney, huu ndio unaongoza katika bara lake, Ukienda nchi ya Ulaya utakutana na mji unaitwa ARGOS nchini Ugiriki, huu ndio mji wa kalr zaidi ulaya, haujulikani ulianza miaka gani lakini Monuments zake huonyesha una umri zaidi ya miaka 7000, Moja ya Watu maarufu wa Enzi hizo walikuwa akina Acrisius, Ageladas kiufupi hata elimu ya "MYTHOLOGY" ilianzishwa na watu wa hapa.

Barani Asia kuna mji unaitwa RAJGIR kule India, huu unadhaniwa kuwa ulikaliwa na watu toka miaka 2000 K.K Mwanzilishi na Kiongozi wa kwanza alikuwa akiitwa Brihadratha ambaye alikuwa mtoto wa Mfalme Uparichara Vasu.

Ukienda bara la Amerika kuna mji unaitwa Flores kwa sasa lakini zamani uliitwa Nojpetén nchini Guatemala unakadiriwa kukaliwa na watu toka miaka 900 K.K

Ukija Barani Africa tunaweza Gawanya bara hili mara mbili kwakuwa upande wa Kaskazini ulikuwa mashuhuri zamani kuliko Kusini (Sub Saharan) hivyo kwa Upande wa Africa Kaskazini mji wa kale zaidi uliitwa LUXOR japo ulijulikana zaidi kwa jina la kigiriki THEBES mji huu unakaliwa na Watu toka miaka ya 3200 Kabla ya Kristu,

Ukija Kwenye nchi za Kusini mwa jangwa la sahara Mji wa kale huitwa Benin City unapatikana nchini Nigeria unafuata mji wa Ife upo Nigeria Pia, miji hii miwili yote hukaliwa na Watu toka miaka ya karne ya kwanza.

Mji wa Tatu ni Zanzibar, Ukikaliwa na watu toka Karne ya Kwanza, Uthibitisho wa Uwepo wa mji huu haukuwepo toka zamani sana, lakini kuna maandishi ya Kigiriki-Kirumi (Greco-Roman) yaliyoandikwa karne ya Kwanza yanayoitwa "Periplus Maris Erythraei" hii ilikuwa kama maandishi au jarida linaloelezea Fursa za biashara Kwa warumi na wagiriki walioishi Huko Misri na Ulaya kwa ujumla, Katika Jarida hilo kilitajwa kisiwa kimoja chenye fursa ya biashara kilichoitwa "Menuthias" ambacho bila shaka ndio "Unguja" ya sasa, Maandishi yale kwa kiingereza huitwa "Periplus of the Erythraean Sea" na ndiyo huonyesha Mji huu mkongwe Tanzania ukifuatiwa na Tanga.

Polycarp Mdemu View attachment 1796245 View attachment 1796242
800px-Gr%C3%A6kenlands_%C3%A6ldste_teater_i_Argos(10.07.05).jpg
View attachment 1796243 View attachment 1796244 View attachment 1796246
 
sailas

Member
Apr 6, 2020
5
45
Halafu anatoka mlevi mmoja anasema Zanzibar ni mali ya Wabara wale wapemba wamevamia toka makwao arabuni. Wakati hao wapemba wapo Zanzibar kabla ya hao wanaosema Zanzibar ni yao hata hapo Bara hawajafika wapo Gambia huko hata nguo hawajaanza kuvaa.
Umeanza ukorofi Sasa watakuja hapa wabara maada itaharibika
 
rodrick alexander

JF-Expert Member
Feb 12, 2012
9,880
2,000
Halafu anatoka mlevi mmoja anasema Zanzibar ni mali ya Wabara wale wapemba wamevamia toka makwao arabuni. Wakati hao wapemba wapo Zanzibar kabla ya hao wanaosema Zanzibar ni yao hata hapo Bara hawajafika wapo Gambia huko hata nguo hawajaanza kuvaa.
wapemba kwao Oman Zanzibar walihamia mababu zao
 
Rogojin The Idiot

JF-Expert Member
Jul 25, 2017
1,615
2,000
Halafu anatoka mlevi mmoja anasema Zanzibar ni mali ya Wabara wale wapemba wamevamia toka makwao arabuni. Wakati hao wapemba wapo Zanzibar kabla ya hao wanaosema Zanzibar ni yao hata hapo Bara hawajafika wapo Gambia huko hata nguo hawajaanza kuvaa.
Zanzibar haijawahi kuwa mali ya wabara. Kwanini tunapenda kuwa waongo waongo? Zanzibar imeungana na bara. Moja ya ushahidi mdogo ni jinsi wazanzibar wanavyokaa kama watanzania wengine huku bara. Mnajaribu sana kuonyesha Zanzibar ni unique na mnalazimishwa. Kitu ambacho sio kweli.
Mkianza kunyanyasa wa bara msisahau hisani zao pia. Waarabu wakija mtageuka wakimbizi
 
Giningi01

Senior Member
Nov 19, 2020
112
225

Acha ukorofi dogo,Zenj ni ya wote na sehemu ya bara,kumbuka Zinjantropus ndio babu yetu na alizaliwa Babati.
 
Giningi01

Senior Member
Nov 19, 2020
112
225
Safari moja nilikuwa White Sands Hotel kwa kazi fulani,team leader alikuwa Mmarekani mmoja,wakati wa chai alionekana ku admire sana hali iliyopo hapo,nilipomuuliza kwa nini? Alisema: Hii hotel ni jengo la kisasa sana kama hotel zingine za kisasa huko kwao,lakini yenyewe imebeba historia ya Zanzibar kwa hiyo architecture yake,furniture iliyoko huko ndani ni aina ya furniture za Zanzibar karne ya 14,hapo ndio mshangao wangu ulipoanzia maana mi najua historia ya Zanzibar inaanza na Said Said.
 
dos.2020

JF-Expert Member
Feb 17, 2009
4,401

CCM ndio hawaitaki historia ya Zanzibar pre Said Said, kwa sababu inawaweka uchi na uwongo wao wote
 
dos.2020

JF-Expert Member
Feb 17, 2009
4,401
2,000
Zanzibar haijawahi kuwa mali ya wabara. Kwanini tunapenda kuwa waongo waongo? Zanzibar imeungana na bara. Moja ya ushahidi mdogo ni jinsi wazanzibar wanavyokaa kama watanzania wengine huku bara. Mnajaribu sana kuonyesha Zanzibar ni unique na mnalazimishwa. Kitu ambacho sio kweli.
Mkianza kunyanyasa wa bara msisahau hisani zao pia. Waarabu wakija mtageuka wakimbizi

Wabara wamenyanyaswa wapi?
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom