Miss Tanzania 2006, Wema Sepetu na mama yake wahamia CHADEMA kutoka CCM

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,492
54,892
Habari: Miss Tz 2006, Wema Sepetu na familia yake watakuwa na Press Conference Saa 5 asubuhi nyumbani kwao Sinza-Meeda.

Waandishi wote wanakaribishwa.

Hiyo ndiyo meseji ya kutoka kwa akina Wema wenyewe kwenda kwa waandishi Asubuhi hii.

=======

Wema Last.jpg
wema3.jpg
mama wema2.jpg
25f29bbc-49b1-4927-9fa7-66c068932e15.jpg

wema1.jpg




Wema akidai hajalipwa fedha za kampeni na CCM


Update: 1337hrs: Bado anasubiriwa Wema Sepetu hajafika, wanafamilia wengine akiwemo Mama yake na Baadhi ya viongozi wa CHADEMA ndo wapo.

1345hrs: Wema Amewasili na Kuanza Kuongea kama ifuatavyo:

⁠ ⁠Mama wema: Habari za mchana, nawakaribisha

⁠⁠⁠⁠⁠⁠⁠Wema: Kwa jina naitwa Wema Sepeti Isack Abraham
⁠⁠⁠⁠
⁠⁠⁠⁠⁠⁠⁠⁠⁠⁠Wema: Naomba mnisamehe kwa kufika kwa kuchelewa
⁠⁠⁠⁠
⁠⁠⁠⁠⁠⁠⁠Wema: ⁠⁠⁠Sitakuwa na mengi ya kuongea, nataka kutoa tamko moja kutoka kwa Wema mwenyewe
⁠⁠⁠⁠
⁠⁠⁠⁠⁠⁠⁠Wema: ⁠⁠⁠Nimewaiteni hapa kuja kutamka rasmi kwamba hivi sasa nmehamia CHADEMA kutoka CCM
⁠⁠⁠⁠
⁠⁠⁠⁠⁠⁠⁠Wema: ⁠⁠⁠Sio kwa tuhuma zinazonikabili bali nmefanya maamuzi kama mtu mwingine yoyote

⁠⁠⁠⁠⁠⁠⁠Wema: Nyote mnajua nlikuwa kada wa CCM na nmepigania chama kwa uwezo wangu wote
⁠⁠⁠⁠
⁠⁠⁠⁠⁠⁠⁠Wema: 2015 niligombea ubunge viti maalum Singida na kura hazikutosha na sikufa moyo
⁠⁠⁠⁠
⁠⁠⁠⁠⁠⁠⁠Wema: ⁠⁠⁠Marehemu baba yangu alikuwa kada nguli wa CCM na alipata kuwa hadi mshauri wa rais Zanzibar, Waziri na Balozi wa Urusi. Amekufa akiwa CCM

Wema:
Nimetuhumiwa hivi karibuni, wakati najitoa kwa hali na mali ndani ya CCM na niliamini hawatanitupa na haina maana kwamba nilitaka kubebwa hapana
⁠⁠⁠⁠
Wema: ⁠⁠⁠Kilichotokea kwangu kilikuwa ni uonevu
⁠⁠⁠⁠
Wema: ⁠⁠⁠Nimetafakari sana kwanini hili limetokea
⁠⁠⁠⁠
Wema: ⁠⁠⁠Kama mwanachama kimenivunja moyo. Tenda wema uende zako usingoje shukurani

Wema: Mimi naamin katika demokrasia. Nimefanya reseach yangu na hata wakati wa kampeni CHADEMA ilitupa tabu
⁠⁠⁠⁠
Wema: ⁠⁠⁠CHADEMA inapigania demokrasia na mimi nataka uhuru wa watu
⁠⁠⁠⁠
Wema: ⁠⁠⁠Ningejua mapema ningenijiunga CHADEMA zamani. Najilaumu sana kuchelewa kujiunga CHADEMA

Wema:
Bado sijachelewa kufanya maamuzi. Na hii najua nimeingia kwenye vita na naamini watu wengi wapo wananiunga mkono
⁠⁠⁠⁠
Wema: ⁠⁠⁠Dola ifanye kazi zake na kifuata sheria kama dola. Ila wazingatie haki za binadamu
⁠⁠⁠⁠
Wema: ⁠⁠⁠Naamini ndani ya CHADEMA tunaweza kuleta mabadiliko nchini
⁠⁠⁠⁠
Wema: ⁠⁠⁠Kwa kupitia nguvu ya CHADEMA tunaweza pata ule uhuru tunaoupigania.

Tangu leo mimi sio mwanachama wa CCM. Mimi na mama tulikuwa wanachama hai wa CCM

Kwa upande wake mama Sepetu, alikuwa na haya ya kusema;

Mama Sepetu :Mmekuwa mnasema natoa mapovu,mimi sitoi mapovu

Mama Sepetu :
Uchungu wa mwana aujuae mzazi

Mama Sepetu :Nmehangaika sana mwanangu alipowekwa ndani

Mama Sepetu :Ningejua mapema ningejiunga CHADEMA zamani.

Mama Sepetu :Najilaumu sana kuchelewa jiunga CHADEMA.

Mama Sepetu :Wema hakuzungumza sana mimi sasa ndo nguli nazungumza

Mama Sepetu :Ametuhumiwa sana. Amekaa sero hamjamuona mwanangu akiwa alosto. Anayetumia unga wiki moja tu akikosa unga anaishiwa nguvu, Mtumia madawa anakuwa hivi?

Mama Sepetu :Hamna kiongozi wa CCM alokuja kuniuliza kulikoni

Mama Sepetu :Mpaka usiku wakina wema walikuwa wanafuatwa mahabusu na Makonda

Mama Sepetu :Haki za binadamu hazikuzingatiwa, watu wanaua wanapewa dhamana.

Mama Sepetu :Lakini yeye(Wema) kahangaishwa sana

Mama Sepetu :Mimi ni mwenyekiti wa CCM tawi la Nzasa kata Kijitonyama tulikuwa na kura nyingi 2015

Mama Sepetu :
Nchi hii Mambo hayaendi vizuri, Wengi hawataki kuzungumza wanauguliwa sana

Mama Sepetu :Sisi ni Watanzania tumebanwa tupo kwenye kitanzi

Mama Sepetu: Mimi kama mama nimesema siwezi kuteswa na mwanangu kudhalilishwa tukiwa chama cha mapinduzi

Mama Sepetu: Mwanangu amezunguka na CCM anainadi nchi nzima

Mama Sepetu :Tangu leo mimi sio CCM tena. Na nitatembea nchi nzima kukinadi chama cha demokrasia na maendeleo.

Mama Sepetu
:Nashangaa CHADEMA hawatupi kadi zao.

Mimi ni mwenyeji wa Singida. Baba katuacha tupo 72. Naenda kupokea kadi za CCM Singida na wote wameahidi kuhamia CHADEMA

Wema: Naomba maswali matatu yanayohusiana na mimi kuhama

Swali: Unaidai CCM?

Majibu ya Wema: Wasanii wengi ikiwemo mimi nawadai, nikianza kuzungumzia madeni watasema ni kwa sababu tumehama. Mimi na wasanii wengine tunawadai CCM lakini wanatujibu tukamdai Kikwete rais mstaafu.

Mariam anauliza swali kuhusu voice note

Majibu ya Mama Wema: Mimi siku nyingi nimezima simu yangu, sijui wala sijaangalia kitu gani kimezungumzwa. Japokuwa nmesikia kwamba kuna sauti. Siijui kabisa

Mimi simu yangu ina matatizo, siwezi kuisikiliza hiyo sauti, mlioisikia ni nyinyi sio mimi

Steve ni mtoto wangu sasa hiyo sauti yangu na Steve siijui

Wala sijawahi kuisikia ila nina mpango wa kuisikiliza simu ikipona

Je huu uamuzi ni wa hasira?

Wema: Hapana sio wa hasira, nimepata hasira kura za viti maalum na ndo ningehama. Hadi hapo CCM ilipo ina jasho langu na nguvu zangu.
Nimeonewa na nimefanywa nijisikie mnyonge ndani ya chama

Nilijitoa ikibidi nife. Nilipoenda Zanzibar wanachama wa CUF walitaka kunimwagia tindikali kisa mimi ni wa CCM. Walinimwagia michanga. Hiyo yote ni katika harakati za kuitetea CCM

Leo chama ndo kimefanya nipitie yote Haya

Mapenzi ni nipe nikupe, mapenzi yakiwa ya upande mmoja sio mapenzi

Je chadema wamekununua?

Majibu:
CHADEMA hawajanipa hata sh 10. Ni mapenzi yangu tu. Hayo mambo ya fedha tumezoweshwa kwa sababu chama cha mapinduzi ndo mtindo wao.

Huu ni uamzi mgumu sana, na mimi nikishasema basi ni basi. Sirudi nyuma.

CHADEMA wanapigania demokrasia. Tanzania yetu imeanza kupoteza demokrasia kwa kiasi kikubwa.

Sijaingia kwenye mitandao. Natamani niingie na kutoa kale kapicha ka CCM nilichokipost tatizo sijapata muda wa kuingi kwenye mitandao.
Kama ni vita nimeshavaa magwanda nipo tayari kupigana
CHADEMA wamenipokea kwa mikono miwili

Swali: Kuna mtu mkubwa una bifu naye, CCM unafanyiwa hivi, je CHADEMA si itazidi?

Kwanza kabisa sina bifu na mtu yoyote kutoka CCM

Maji ukiyavulia nguo sharti uyaoge

Kumbuka mimi nina kesi mahakamani, tunachopigania ni uhuru na demokrasia. Maswali yametosha. Asanteni sana

~MWISHO~
 
Akili ni nini?
PATO8221 Kuna vitu vitatu ambavyo binadamu aliyekamilika anatakiwa kuwa navyo vitu viwili unavipata bure kimoja ndio unakinunua

1 UTASHI (will)
2 UFAHAMU (knowledge)
3 AKILI(intelligence)

Utashi na Akili ni vitu vinavyopatikana bure kutoka kwa Mungu lakini Utashi tumepewa wote si Akili , Akili wamepewa watu wachache ambao Mungu amewachagua Akili siku zote inakwendana na Hekima yani aliyepewa Akili amepewa na Hekima pia na ndio maana siku zote wenye akili nyingi wanakuwaga kama washamba washamba au mabwege mabwege

Kitu ambacho binadamu tunakinunua ni UFAHAMU (Maarifa) na siku zote ufahamu unapatikana kwa kwenda Shule au Makazini
Shule tunakwenda na Akili zetu na Utashi wetu ila shule au makazini tunakwenda kupata maarifa tu na ndio maana hakuna shule au kazi duniani inayofundisha Akili kwa sababu akili tunakwenda nazo shule au makazini

Sasa bhasi unaweza kwenda Shule mpaka ukawa na kiwango cha PhD husiwe na Akili sana sana utakuwa na Ufahamu tu so ni sawa na dereva wenye leseni lakini ajui kuendesha gari , leseni ni kama cheti tu lakini kuendesha gari ndio ujuzi wenyewe na ndio akili zenyewe

AKILI ni uwezo wa kutumia maarifa (ufahamu) kwa njia sahihi

UTASHI ni kitendo cha kujua mabaya na mazuri utashi ndio unatofautisha binadamu na wanyama ndio maana mpaka leo wanyama wanatembea uchi lakini hawajijui kama wako uchi

UFAHAMU ni mkusanyiko wa ujuzi ,maarifa na habari ambayo binadamu au wanyama(mfano Mbwa ,Panya nao wanafundishwa hata kujua madawa ya kulevya au kujua mabomu yalipofichwa ) wanayapata kwa kupitia uzoefu au kwa kwenda shule
 
Wema ananguvu ya ushawishi achilia mbali mvuto alio nao,hata akitamkacho huwa kina attention katika jamii yake kikubwa anachokosa huyu dada ni team ya kumsimamia na kumuongoza,nadhani hii kadhia aliyokutananayo itamfanya akue kama akiamua,pia itamjenga na itampa umaarufu maradufu akijiongeza within a short time atakaa anga za ma VIP achana na huko ligi za mchangani insta na FB
 
Back
Top Bottom