Kumbe watoto wa uswazi ni washenzi kiasi hiki? Yamenikuta leo

Abunuwasi aliwahi kujipata ana Nywele nyingi kichwani. Alihitaji kwenda saloon. Akampata mtoto mwenye nywele nyingi mtaani. Akamshika mkono kwenda nae saloon. Kule saloon wa kwanza kunyoa akawa Abunuasi. Alipomalizwa kunyoa akaondoka. Mtoto nae akanyolewa. Alipomalizwa akaulizwa kaenda wapi babako! Mtoto akajibu yule sio Babangu. Kanikuta mtaani akanambia twende tukanyoe saloon!
 
Jr
 
mshana swala la askofu vipi
Yuko
IMG-20200723-WA0039.jpg

Jr
 
mbona kama ya emanuella hii?!!!!!
We sema hii kama ya Emmanuella wakati wengine tumefanya sana hii michezo miaka ya 90's.
Nakumbuka wengine tulifika mbali mpaka kupiga simu polisi au kitengo cha zimamoto kupitia zile phone box za barabarani za TTCL kuwa kuna nyumba inaungua au ajari imetokea sehemu fulani alafu tunakaa sehemu kuskilizia king'ora😂😂😂
Utoto bhana haha.. It was kind of amusement😊😊
 
sipati picha hiko kichurachura ambacho mngerushwa kama mngekamatwa
 
Huwezi kuamini kilichonikuta mchana tuu..bado binafsi siamini kama nimeweza kuingizwa chaka na vitoto vidogo ambavyo vinaweza kuwa vijukuu vyangu...

Niko mitaa ya Mikocheni nyuma ya Tanesco nilikuwa mpitanjia kuingia mtaa wa pili..sio mwenyeji kivile..nimejikuta naibukia mtaa wa madon lakini huruma zangu kidogo ziniponze.

Nimekuta vitoto vitatu kwenye geti la nyumba ya maana vinajitahidi kurukia kengele ya getini..basi nikajua wana uhitaji na wenye nyumba nikasema ngoja niwasaidie.

Ile kusogea tu wakakaa pembeni..nikaamini nachukua point 3 muhimu za upendo nikanyoosha kono langu na kubonyeza kengele ..nikasikia inaita...kugeuka nione furaha na shukrani kwa wahitaji,kwa mshangao na tarahuki nikawaona wanakimbia ..mmoja akasema wee hapo sio kwetu..

Natamani ungeniona hatua nilizoondoka nazo hapo... Watoto wa uswazi wa uswazi wapuuzi sana

Jr
Ndo treand tayari et
 
Back
Top Bottom