Kumbe watoto wa uswazi ni washenzi kiasi hiki? Yamenikuta leo

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
146,099
2,000
Huwezi kuamini kilichonikuta mchana tuu..bado binafsi siamini kama nimeweza kuingizwa chaka na vitoto vidogo ambavyo vinaweza kuwa vijukuu vyangu...

Niko mitaa ya Mikocheni nyuma ya Tanesco nilikuwa mpitanjia kuingia mtaa wa pili..sio mwenyeji kivile..nimejikuta naibukia mtaa wa madon lakini huruma zangu kidogo ziniponze.

Nimekuta vitoto vitatu kwenye geti la nyumba ya maana vinajitahidi kurukia kengele ya getini..basi nikajua wana uhitaji na wenye nyumba nikasema ngoja niwasaidie.

Ile kusogea tu wakakaa pembeni..nikaamini nachukua point 3 muhimu za upendo nikanyoosha kono langu na kubonyeza kengele ..nikasikia inaita...kugeuka nione furaha na shukrani kwa wahitaji,kwa mshangao na tarahuki nikawaona wanakimbia ..mmoja akasema wee hapo sio kwetu..

Natamani ungeniona hatua nilizoondoka nazo hapo... Watoto wa uswazi wa uswazi wapuuzi sana

Jr
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom