Kumbe wanawake wanahitaj assurance!!

Daudi1

JF-Expert Member
Dec 14, 2013
8,805
8,717
Habari ya mchana wapendwa, nimeikuta sehemu hiii
......................................

By nature nadhani mwanamke ameumbiwa kujua "assurance" hata kama hatakuwa na matumizi nayo lakini kuwa assured a.k.a kuhakikishiwa kwao huwa inahusu sana.

Suala la usalama wao wa nafsi na akili na mwili ni muhimu sana ndio maana kwa wale wanaosoma Biblia utaona nyoka alimwambia Hawa "Hakika Hamtakufa" ndipo akachuma tunda alitamani kujua "hatma" ya jambo kabla hajaamua kulifanya. Kwa wale wakaka wanaokwazika sana mdada akiuliza "unafanya kazi wapi"?unafanya kazi gani?kuna wanaume wanadhani ni kwamba wanawake wanapenda watu wenye kazi na hela hapana by nature wanapenda "assurance". Umewahi jiuliza kwanini wanawake wanapenda wanaume wenye hela?its more of Psychological kuliko economical. Mwenye hela anampa assurance kwenda salun, mwenye hela anampa assurance ya pampas za kila mwezi mwenye hela anampa assurance ya usafiri wa uhakika.

Ndio maana Sara alicheka aliposikia kuwa atapata mtoto sababu gani?hakuwa na uhakika. Si kweli kwamba wanawake wanapenda wanaume wenye hela na mali na kazi nzuri ila wanapenda mwanaume anayejitambua. Kama haujitambui usitegemee upata mke yeyote atakayeuwa anaku challenge. Maswali ya wanawake wengi sana katika mambo ya mahusiano mpaka kwenye ndoa yanataka kujibu maswali aliyonayo ndani yake wengi tumekutana na maswali kama Hivi kwanini Unanipenda Mimi?, Kati ya Wanawake zako woooooote na marafiki zako wa kike kwanini unataka mimi niwe mpenzi wako?Unafanya kazi wapi?Unakaa wapi?wanawake wanapenda mtu mwenye Identity. Ukiwa haujitambui upo upo tu, kulala unalala kwa washikaji unabebwa,maisha yako ni ya kubangaiza bangaiza hujulikani hasa unafanya nini kwenye maisha basi jua utasubiri sana. Hivi unadhani Mungu hakuwa na akili umpa kwanza Adam bustani ya eden?Mungu alimpa kwanza shughuli ya kuendesha maisha hawa akija. Na hawa haunyanyua mguu mpaka Adam alipompa assurance "wewe ni nyama katika nyama yangu...."

Wanawake huwa wanawaza "Ye Mwenyewe Hajitambui" nitampeleka wapi?unaweza ukawa huna hela wala mali ila Vision yako, Plans yako, maneno yako na yale uliyoyaanza kuyafanya maishani yanampa mwanamke assurance "ndani ya huyu jamaa kuna kitu". Watu wanasema kila katika mafanikio ya mwanamme una mwanamke nyuma yake ni kweli kabisa kwa sababu wanawake huwa wanachagua watu wanaojitambua kazi yake kubwa ni kuhakikisha kuwa ile mipango, zile ndoto ile mikakati inatimia kwenye maisha yao. Wanawake sio ma mbulula kiasi kwamba wachague tu wasio jitambua ndio maana wanachagua. Ukijitambua na wakatambua kwamba unajitambua wataanza kuja wao. We hujawahi ona mwanaume zamani alikuwa fala fala na hakuna mtu alikuwa anamfata wala umsikiliza siku alipokamata destiny na "uhakika" basi hata kama ni Mzee kama nannii watakuita baby. Wanaume wengi sana wenye hela hudhani wanapendwa wao hasa si kweli ni ule Uhakika wa kesho, Uhakika ukiondoka ndo watu wanasema Kosapesa ujue tabia ya mkeo. Ukweli nikwamba pesa hainunui mapenzi lakini fedha inauhusiano na amani za mahusiano ya watu wengi sana. Biblia inasema Fedha ni Jawabu la Mambo Yote.

Natoa Rai kwa wanaume wenzangu hasa wale wavivu ambao wanapenda kulelewa ambao kizazi hiki wako wengi sana, wanapenda kununuliwa vitu na wapenzi wao, wapenzi wao wakiishiwa hela kwenye simu ujue mazungumzo ndo yameisha hawezi hata kutuma buku amaapige yeye unashangaa tuu uhusianoumeshikiliwa sana na mwanamke kuliko mwanaume mdada akipata shida ama tabu ujue Mungu ndo atajibu ila yeye akipata tabu mdada aisema hana utasikia tu "si najua hunipendi".

Hebu semeni jamani ni kweli mwanamke anahitaj assurence tu? Na ni kweli assurance inapatikana kwenye vitu? Na inakuaje vitu vikiisha si atatafuta assurance kwingine?
 
1466521087125.jpg
 
VIp unaweza kufanya kazi kwa mikataba ya miezi mitatu mitatu kwa kutegemea fedha za wahisani....
 
Yaani wewe acha tu, ndiyo maana wale makapuku wenye confidence wanachukua watoto wazuri, wewe jiamani na hata kama huna pesa mwambie don't worry baby, every thing is under control, hiyo tu inatosha. Sasa wewe kwenye situation unapanick unataka binti afanye nini?
 
Je mifano aliyotoa ndo inajustify? Kama tunavyojua maisha yanabadilika siku assurance imetoweka mwanamke itakuwa katika hali gani?
Mkuu,umegusa kitu muhimu ambacho sisi wanaume tulio wengi hatukijui,assurance kwa mwanamke kiu na maji,yaani mwanamke ni delicate kwa jinsi alivyoumbwa,kuanzia mwili na akili,namaanisha mwanamke katika uahi wake wote anahitaji faraja(peace of mind),ili aweze kuishi,hii inamaanisha asipate misukosuko ya aina yoyote sababu yeye ni mtu waa kubaki kambini kwa wakati wote mwanaume anapokwenda kuwinda,hivyo basi yeye niwakuletewa mawindo na kupewa hug na bwana wake,huku akibembelezwa,na hii ina apply mpaka leo dot com au kidigitali,ukitaka demu akuzimie na akupende basi wewe muhakikishie kiukweli kwamba wewe ndio ngao yake au mlinzi wake against any hassle au worry ya aina yoyote,kuanzia finance,security,emotional things,grief,yaani uwe multy purpose kwake yeye.
 
kwa maana hiyo zile ndoa zilizofungwa Enzi za utawala wa JK sasa ziko mbioni kuvunjika? Kuna wadada wanajitoa muhanga na kujihaibisha mitandaoni kuwa Baba JK ninakumiss, mara utawasikia sijuwi JK yuko wapi anisaidie.....Maisha ni nusu nusu, you work, I work tunasukuma gurudumu la maisha pamoja si kutegemea kutoka kwa mwanamme tu. Ni ujinga kwa mwanamke hataki kufanya kazi au kujituma kwa namna yeyote kisa mwanamme atamsaidia kimaisha. Mademu wa kibongo muvi kwa kweli ni nuksi na ndiyo maana wanazidi kuchezewa akili na kuzeeshwa bila kuolewa.
 
Hahahahaha wanataka assurence wewe acha mbwembwe
 
Yaani wewe acha tu, ndiyo maana wale makapuku wenye confidence wanachukua watoto wazuri, wewe jiamani na hata kama huna pesa mwambie don't worry baby, every thing is under control, hiyo tu inatosha. Sasa wewe kwenye situation unapanick unataka binti afanye nini?
Mmmh wanataka assurence si maneno matupu ulisema beby nimeishiwa mafuta akasema sina mtihani hapoo
 
Mkuu,umegusa kitu muhimu ambacho sisi wanaume tulio wengi hatukijui,assurance kwa mwanamke kiu na maji,yaani mwanamke ni delicate kwa jinsi alivyoumbwa,kuanzia mwili na akili,namaanisha mwanamke katika uahi wake wote anahitaji faraja(peace of mind),ili aweze kuishi,hii inamaanisha asipate misukosuko ya aina yoyote sababu yeye ni mtu waa kubaki kambini kwa wakati wote mwanaume anapokwenda kuwinda,hivyo basi yeye niwakuletewa mawindo na kupewa hug na bwana wake,huku akibembelezwa,na hii ina apply mpaka leo dot com au kidigitali,ukitaka demu akuzimie na akupende basi wewe muhakikishie kiukweli kwamba wewe ndio ngao yake au mlinzi wake against any hassle au worry ya aina yoyote,kuanzia finance,security,emotional things,grief,yaani uwe multy purpose kwake yeye.
Kwa hiyo unashauri nini kulingana na maisha ya sasa waendelee kupata uhakika wa kesho kwa mwanaume au watafute wa kwao?
 
Back
Top Bottom