big-diamond
JF-Expert Member
- May 23, 2009
- 421
- 551
Kwenye harakati za kupunguza zile kauli kupata tabu sana na biti za watembea na ilani basi jioni hii najirudisha uswekeni kwenda kujificha hadi hapo kesho (Maana kuna watu huenda kulala na wengine kijificha)
Hapa nipo kwa daladala iliyojaa ile kisawa sawa, basi kuna Mama tumepanda nae daladala akiwa na mtoto mgongoni kwenye kitenge(Heshma zenu wamama wote mliolea na kupenda watoto wenu)
Basi mtoto akaanza kulia kwa kulalamika huku mama akihangaika kumbembeleza huku kashikilia bomba,(wale wa mbagala wananielewa hapa), tumeendelea na safar bas imefika sehem foleni ikawa kubwa(nahisi kuna Mamajusi wameenda kuona mtoto), bas mtoto analia na mama anahangaika ili asiwe kikwazo kwa wana daresalama.
Ni kama malaika alimwambia dada mmoja aliyekuwa amekaa kwenye kiti(Makonda huita sofa) kuwa yule mwanamke mwenzie na mwanae wanahitaji msaada, bas akamwita yule dada na kumwambia aje akae na mwanae pale alipokuwa yeye, na yeye kushika bomba(kupaka rangi).
Hili tukio limenifanya nimtazame mara mbili mbili huyu dada na kwakweli nisingekuwa nimeoa Mama Nyonzo wangu pale Itinde bas leo ninge propose...
Heshma yenu wanawake na madada wote mnaopendana na kusaidiana kwenye mazuri..
Ora Et Labora..