Kumbe wanawake nao wana mkono katika jambo hili...!

Kumbe wanawake nao wana mkono katika jambo hili...!

Mtambuzi

Platinum Member
Joined
Oct 29, 2008
Posts
8,809
Reaction score
15,443


Tofauti na inavyodhaniwa, kwamba wanaume ndiyo wanaoanza kuwatamkia wanawake kuhusu tendo la ndoa, kumbe wanawake nao wana mkono katika jambo hili. Kumbuka hapa siwazungumzii wale wanawake makahaba au wale wanawake wanaojilengesha kwa wanaume kwa ajili ya kutafuta nafuu za kimaisha.

Kwa mujibu wa takwimu zisizo rasmi imebainika kwamba, kwa kawaida robo au zaidi kidogo ya wanawake ambao hutoka nje ya ndoa zao, wao ndiyo waliowatongoza wanaume kwa njia mbalimbali.

Nusu ya matukio inahusisha wote wawili, yaani mwanamke na mwanaume kuanzisha uhusiano huo, yaani wamevutana na kupeana ujumbe kwa njia mbalimbali, kwamba wanavutana na mara nyingi mwanamke anafanya vibweka kwa kumtega mwanaume aliyevutiwa naye kwa njia mbalimbai ikiwemo kumvalia mavazi yenye utata n yanayoamsha hasia za kimapenzi, mikao mbalimbali nk.

Kumbuka kwamba, kuna wakati mwanaume na mwanamke wanatakana na kila mmoja anajua, hivyo kinachotafutwa ni namna ya kupeana taarifa rasmi.


Je nani aanze? Hapo ndipo unaweza kushangaa jinsi mwanamke atakavyoanza kujifaragua kwa sitaki nataka kumbe ana lake moyoni…….
 
I find it romantic mwanamke akiniambia anahitaji tendo kuliko nikimwambia kila mara.
 
Mtambuzi.... sikuhizi wanawake hawana longolongo anakwambia tu kama kakumind...

Kumbe hata wake za watu ka wamempenjda mwanaume huwa wanasema tu bila kujali...?
sSasa huyo ni mke au kahaba? Badili Tabia.........
 
Siku hizi kufunguka tu ndo mpango mzima,ila hapa kwa walioolewa tu akijiskia anataka amwambie tu mumewe si mpaka aombwe.
 
Kumbe hata wake za watu ka wamempenjda mwanaume huwa wanasema tu bila kujali...?
sSasa huyo ni mke au kahaba? Badili Tabia.........

Mkuu,sijui unawezaje kuhusisha hayo mawili ....!!
 
yeah! Hata mi mwanamke akinambia anataka najsikia better kuliko ninavyomwambia mimi sema huwa wanaogopa nin sjui
 
Hiyo ni kweli kabisa

Binafsi nimeshakutana na haya matukio na ni zaidi ya mara 3

Kimsingi wanawake walioolewa kwenye hili ndio wanaokuwa wa kwanza "kulianzisha"
Tofauti hapa inaweza kuwa ni namna ya kuufikisha ujumbe tu!
 
Back
Top Bottom