binti wa kirombo
JF-Expert Member
- May 17, 2016
- 847
- 967
Habari za kazi wana JF,
Leo katika pilika zangu za ujenzi wa taifa kama mwl. Mkuu nikapita ofisini kwa walimu wenzangu kuwasabahi kama ilivyo dada.
Mwl mmoja akasema mkuu unaonaje kabla ya kufunga Ijumaa sisi walimu wote tukajumuika na wenzi wetu tukasherekea kumaliza mwaka wa masomo salama? nikamjibu haiwezekani! Kwa gharama ya nani?
Akasema watachangisha mchango kila mtu elfu 50 nikasema hapana ile namaliza kujibu walimu wote wameinuka nakunishambulia kwa maneno, ooh mkuu acha ubahili, unatubania riziki watu tunastress tunataka tukatoe stress na maneno mengine kibao.
Wakaanza wachaga bwana ubahili umewazidi, nikawaambia kama mnatakuorganize fanyieni nje ya eneo la shule na chochote kitakachotokea sitawajibika juu yenu.
Hawakuamini majibu niliyoyatoa mwalimu mmoja ambae ni rafiki yangu akaropoka hana wakuja nae INJINIA WAKE ALIMWACHA TANGU ILE JANUARY, aisee nilichotaka kumjibu huyu mwalimu Mungu aliniziba mdomo hakika.
Nikaondoka huku wakicheka sasa kwa tarifa yao hakuna cha sherehe wala nini! Ijumaa skuli itafungwa watu waende makwao wakapumzike. Sasa na sijui hela ya likizo atamsainia nani huyo mropokaji.🙄😎😎