Kumbe walilipwa kuhudhuria mkutano wa CCM Dar! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kumbe walilipwa kuhudhuria mkutano wa CCM Dar!

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Zak Malang, Aug 24, 2010.

 1. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #1
  Aug 24, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0


  [FONT=&quot]Wananchi wengi katika umati mkubwa wa watu waliohudhuria mkutano wa uzinduzi wa kampeni za CCM kule Jangwani siku ya Jumamosi iliyopita walifika hapo baada ya kuliupwa kufanya hivyo.

  [/FONT] [FONT=&quot]Baadhi ya watu niliozungumza nao wanaotoka sehemu za Mbagala Rangi Tatu na Mbande wanasema mabasi ya daladala yalikodishwa na CCM kusomba watu kuwaleta jijini kuhudhuria mkutano na waliokubali kupanda walilipwa Sh 5,000 kwamba hizo fedha ni za usumbufu na nauli yao ya kurudi baada ya mkutano.

  [/FONT] [FONT=&quot]Kila moja ya mabasi haya yaliyokodishwa yalikuwa yanalipwa mapato yao ya siku mbili.


  [/FONT] [FONT=&quot]WanaJF, hizi habari ni za uhakika nilizopata kutoka kwa watu watatu waliopanda mabasi hayo na kulipwa kutoka sehemu hizo mbili nilizotaja. Wanasema tangu asubuhi majira ya saa 3 mabasi yalifika maeneo hayo na kuegesha huku viongozi na makada wa CCM wakihamasisha watu kuingia. Sh 5,000 ni nyingi sana katika sehemu hizo.

  [/FONT] [FONT=&quot]Hali hii bila shaka ilijitokeza katika sehemu nyingi tu pembezoni mwa Jiji siku hiyo – watu kulipwa na kutafutiwa usafiri ili wahudhurie mkutano.

  [/FONT] [FONT=&quot]Mapesa yaliyotumika ni mengi kwa tafsiri yoyote ile, na bila shaka ni kati ya zile Sh Bilioni 50 ambazo CCM imetenga kwa ajili ya kampeni mwaka huu.

  [/FONT] [FONT=&quot]Tatizo langu hapa si uhalali au la kwa CCM kulipa watu kuhudhuria mkutano wao wa kampeni, ingawa pengine ni suala linaloweza kutazamwa kama ni njia mojawapo ya kuwahonga wapiga kura.

  [/FONT] [FONT=&quot]Tatizo langu hasa ni ile dhana inayojengwa kwamba CCM bado ina wafuasi wengi, dhana ambayo siyo kweli kwani iwapo wananchi wangeachwa kufika hiari yao, mkutano ule ungehudhuriwa labda na nusu tu ya watu waliojitokeza.
  [/FONT]
  Wanachofanya CCM ni kujenga muonekano wa ufuasi mkubwa katika mikutano yao kwa nguvu fedha walizonazo – na siyo kwa hiari ya wananchi wenyewe bila kushawishia kwa njia ya pesa.
   
 2. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #2
  Aug 24, 2010
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  kaka hiyo ni tactic ya vita.

  lazima umtishe adui wako.

  kama pesa zilizotumika ni halali basi hapa inabidi tuipe point ccm kwa kuweza kuwa na mbinu za kuwatisha wapinzani wake. iko katika njia za kujihakikishia inapata ushindi tu.

  lakini hizo pesa kweli za halali?
   
 3. K

  Kyachakiche JF-Expert Member

  #3
  Aug 24, 2010
  Joined: Feb 16, 2009
  Messages: 911
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 45
  Mimi naweza kuamini kwani nilipita maeneo ya Magomeni, Mabibo na Kawe nikaona daladala zaidi ya moja zikiwa zimeegeshwa kwenye ofisi za CCM zikiwa na mabango ya CCM huku watu wakihamasishana kuwahi kwenye mkutano wa ufunguzi. Sikuweza kujua mara moja kama magari hayo yalikodiwa na wanachama wenyewe au waliwezeshwa.
   
 4. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #4
  Aug 24, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  BASI KAMA HALI NI HII INATISHA SANA!..I wish ningalikuwa ndo mgawaji wa hizo pesa..huh!
   
 5. Kachanchabuseta

  Kachanchabuseta JF-Expert Member

  #5
  Aug 24, 2010
  Joined: Mar 8, 2010
  Messages: 7,290
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Very sad, najua hata ingewafikia TAKAKURU wasingefanya lolote

  TAKAKURU wanasubiri VYAMA vya Upinzani vianze kampeni hili viwakamate
   
 6. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #6
  Aug 24, 2010
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,126
  Likes Received: 1,705
  Trophy Points: 280
  Ni mbinu tu hizo na kawaida yao kutumia pesa kufanya chochote halali na haramu!
   
 7. Sokomoko

  Sokomoko JF-Expert Member

  #7
  Aug 24, 2010
  Joined: Mar 29, 2008
  Messages: 1,918
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135


  Wwnafanya hivyo ili iwe rahisi kuchakachua KURA
   
 8. Uncle Rukus

  Uncle Rukus JF-Expert Member

  #8
  Aug 24, 2010
  Joined: Jun 16, 2010
  Messages: 2,430
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  I wish mwaka huu kutatokea ***************************** nyie subirini tu mtaona matokeo yake.
   
 9. Kachanchabuseta

  Kachanchabuseta JF-Expert Member

  #9
  Aug 24, 2010
  Joined: Mar 8, 2010
  Messages: 7,290
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135

  Nini?
   
 10. Ndibalema

  Ndibalema JF-Expert Member

  #10
  Aug 24, 2010
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 10,916
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  Sijakuelewa hapo. Ufafanuzi tafadhali.
   
 11. Ntemi Kazwile

  Ntemi Kazwile JF-Expert Member

  #11
  Aug 24, 2010
  Joined: May 14, 2010
  Messages: 2,145
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Pathetic..... !!!!

  Leo Clouds wamekuja na mpya, katika kipindi cha pawa brekifast cha magazeti walikuwa wanasoma habari zilizoko kwenye gazeti la Mtanzania juu ya maisha binafsi ya Dr. Slaa, kwa mtazamo wangu wa harakaharaka lazima kuna pesa imetembea kwa magazeti hayo kusomwa redioni. kwani wanajua kabisa bila kufanya hivyo ni watu wachache sana ndo wangelipata habari zake kutokana na ukweli kwamba magazeti ya New Habari Cooperation hayasomwi na watanzania wengi. Kwa hiyo kwa habari yoyote iliyoandikwa humo kuwafikia watanzania lazima yasomwe redion na nina imani akina PJ na wenzake wamekula hela nzuri kwa kulisoma Mtanzania leo
   
 12. kilemi

  kilemi JF-Expert Member

  #12
  Aug 24, 2010
  Joined: Mar 13, 2009
  Messages: 520
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Basi itakuwa ni bahati mbaya sana, maana waliambulia kuona anavyoanguka badala yahotuba
   
 13. KIMICHIO

  KIMICHIO JF-Expert Member

  #13
  Aug 24, 2010
  Joined: Aug 12, 2010
  Messages: 1,184
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  Hiyo ni kweli kabisa maana juzi nilikuwa moshi na nilishuhudia live na mi pia nikalamba buku tano na nilivyofika kwenye mkutano wao tu nikatorokea kwenye bia.
   
 14. Z

  Zion Daughter JF-Expert Member

  #14
  Aug 24, 2010
  Joined: Jul 9, 2009
  Messages: 8,936
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 145
  Ndio ofutopic hizi tunazisemaga.Title ya habari haihusiani kabisa na haya maelezo waliyotoa,Halafu huna hata ushahidi wowote kwenye habari yako.Poor you!
   
 15. Ntemi Kazwile

  Ntemi Kazwile JF-Expert Member

  #15
  Aug 24, 2010
  Joined: May 14, 2010
  Messages: 2,145
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  My Daughter, habari inahusu thithiem kutoa pesa kwa watu kuhudhuria mkutano, hapa najadiri uwezekano wa pesa kutembea katika kusambaza habari za kumpunguzia umaarufu mgombea fulani.... tofauti yake ni nini kati ya hizi habari. Nadhani wewe ndo unashida ya kuelewa... usibebe kama mawe, tafakari!!!!!!!!!!
   
 16. Kachanchabuseta

  Kachanchabuseta JF-Expert Member

  #16
  Aug 24, 2010
  Joined: Mar 8, 2010
  Messages: 7,290
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Mkuu ungeanzisha thread nyingine.
   
 17. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #17
  Aug 24, 2010
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Hii ni habari nzuri kwani it is somewhere in history kwamba tawala nyingi za kidhalimu huenda mpaka kwenye level ya kukosa umaarufu na hata kuaminiwa na wananchi wake as such hulazimika kuweka kila kitu at a price. Mwisho wa siku dhamira hushinda bei.

  Sasa bssi CCM kwa jinsi ilivyokuwa out of touch inapata shida mno kutokana na kupendwa Dr. Slaa ambayo ni free of charge affection. CCM ingeweza kumcrash Slaa ina day kama mchuano ungekua ni nani ana hela zaidi lakini the game is just different and too different.

  Wewe subiri uzinduzi wa kampeni ya Slaa, utawasikia tu CCM malalamiko ya kienyeji...............
   
 18. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #18
  Aug 24, 2010
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,632
  Trophy Points: 280
  Nadhani CCM wamegundua hawana mvuto mbele ya jamii ndiyo maana wameamua kutoa fedha kwa wananchi ili mikutano yao ionekane ina watu.Mama Batilda Buriani alipokuwa akirejesha fomu watu waliomsindikiza walilipwa fedha sielewi mikutano yake atakuwa akigawa fedha au vipi ?.
   
 19. N

  Nanu JF-Expert Member

  #19
  Aug 24, 2010
  Joined: May 29, 2009
  Messages: 1,224
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Shule za kata ndiyo kiama cha ccm. Hizi shule ijapokuwa siyo za kiwango sana bado form four leaver au failure siyo std seven leaver lazima kuna kitu atakipata. Hiki ndiyo kizazi kitakachoibomoa ccm na kuipa chama mbadala nafasi. Chadema ina nafasi nzuri sana hasa kwa wale ambao wameweza kusoma sera zake na siyo kusikia majina ya viongozi tu na kuanza kuyajadili.
  Ccm inapofikia umma unanunuliwa kuja kwenye mikutano basi ni hatari. Hata hivyo inakuwa ni mbinu mbadala kwa helikopta. Ifikie wakati vyama mbadala viweze kuwashawishi vijana katika level ya chini wajiandikishe kupiga kura na wajue nini cha kuangalia ktk chama na mgombea wake.
  Imani potofu itapotea na watu wote watakuwa wanajua nini cha kufanya wakati wa uchaguzi.
   
 20. M

  MILKYWAY GALAXY JF-Expert Member

  #20
  Aug 24, 2010
  Joined: Dec 12, 2008
  Messages: 201
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  wezee wetu walisema,

  "KIZURI CHAJIUZA, KIBAYA CHAJITEMBEZA"

  We all know kipi ni KIZURI, kipi ni KIBAYA,

  Huu ndio wakati mwafaka wa kununua "KIZURI"
   
Loading...