technically
JF-Expert Member
- Jul 3, 2016
- 12,632
- 51,820
Lazima tuwe wakweli kwenye bomba la Gesi tulipigwa bei Mara mbili ya bei ya kawaida na wachina....
Sakata la bomba hata bado ni bichi mjadala ukianza Sasa tulipigwa pesa karibu Mara mbili na hili watu wanalijua kabisa lakini wanataka tupigwe tena kwenye Reli.......
Lazima tukubali ufisadi ulikuwa umetamalaki ndani ya serikali ingawa bado unaendelea lakini ni vizuri kupunguza.....
Ushahidi pia ni kwa reli ya Kenya wamepigwa pesa 50% ya mradi wote Wa reli yao...
Sasa hivi Uhuru Kenyatta anapata shida kuzungumzia mradi huu kwa sababu ya ufisadi uliofanywa na wanasiasa Wa Kenya kushirikiana na wachina...
Lazima tuwe makini na wachina pia kama tunataka kupambana na ufisadi...
Pongezi kwa Rais kwa hili nakupongeza kwa kuokoa pesa ambazo ni mkopo ambao ungekuja kulipwa na walipa kodi......