Kumbe wabunge wa ccm ni wahalifu! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kumbe wabunge wa ccm ni wahalifu!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MBURE JASHA, Nov 3, 2011.

 1. MBURE JASHA

  MBURE JASHA JF-Expert Member

  #1
  Nov 3, 2011
  Joined: May 7, 2011
  Messages: 200
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Salaam Wadau wa JF
  Ndugu zangu kuna tukio limetokea hapa Jimboni kwa Mhe. Prof Maghembe. Prof. Huyu amembambikia kijana mmoja ambaye ni Green guard wa Chama chake kesi ya kuvunja ,kujeruhi na kuiba anayeitwa Arafati Shabani. Kesi hiyo imefunguliwa katika Kituo cha Polisi cha Gymkana Dar Es Salaam.
  Sakata hilo liko kama ifauatavyo:-
  Mnamo tarehe 18 October 2011 Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Kilimanjaro alifanya ziara wilayani hapo na kwenye mazungumzo yake na vijana wa Mwanga aligusia kuhusu mgogoro ndani ya CCM wilaya ya mwanga na kuuliza kwa nini makundi hayo hayamalizwi watu wakaheshimiana. Wajumbe wote akiwemo huyo Arafati walisema tatizo ni Maghembe ambaye ndiye anayehubiri uhasama katika mikutano yake. Kulikuwepo na mtumishi wa Ofisi yake ambaye ni mjumbe wa kikao hicho akapaniki sana baada ya Bosi wake kutuhumiwa kuwagawa wana mwanga. Baada ya siku 4 Mwenyekiti wa CCM wa kata ya Mwanga Ombeni Stephano Msangi (Ifolongo) alifika Ofisi za CCM wilaya ambapo pia Ofisi za Jumuia zipo akiwa na askari polisi akamkuta Arafati kwenye Kikao cha Jumuia yake na kuwaamuru Polisi wamkamate!
  Baada ya viongozi wenzake akiwemo Mwenyekiti wao walifika Polisi na kukuta kuwa Shitaka hilo linadai kuwa Arafati amfuata Maghembe amtafutie kazi ya ulinzi huko Dar. Naye maghembe akampatia kazi huko Chuo cha usimamizi wa Fedha IFM ndipo mwezi february arafati na wenzake wakavunja nyumba ya Mhadhiri anayeitwa Dr. Mrutu na kuiba Laptop Mbili na kukimbilia kwao Kileo.
  TLUCHOGUNDUA baadae kwa mujibu wa Viongozi wake wa vijana waliofuatilia sakata hilo Polisi ni kuwa.
  1. Arafati Shabani hajawahi kutoka Mwanga tangu mwaka huu uanze!
  2. Rb iliyomkamata ni ya kugushi na haipo Polisi ila ipo kama text msg iliyopo kwenye simu ya Ifolong'o RB yenyewe ni Namba GYMKNA/RB/915/2011 iliyofunguliwa tarehe 16 October 2011 na tukio linadaiwa kufanyika mwezi wa february 2011
  3. Kwa taratibu za jeshi la Polisi kama kuna tukio la namna hiyo ni kuwa yanafanyika mawasiliano Official kwa kwa kila ngazi lakini hakuna kitu kama hicho kilichofanyika.
  4. Police wenyewe wa Mwanga na Dar wanarushiana mpira juu ya kumsafirisha Arafati ambaye yupo tayari kwenda huko Dar. OCID wa Mwanga amekataa kabisa kumruhusu ARAFATI kwenda mwenyewe Dar kujisalimisha.\
  5. IFM kuna kampuni iliyoajiriwa pale ambayo inatoa ulinzi ambayo ni ULTIMATE SECURITY na polisi. ambapo huyu bwana hajawahi kuajiriwa maisha yake yote ni Mkulima ambaye anajimudu kwa kila kitu.

  Ndugu zagu je huu si uhalifu! wanaojua sheria kidogo tuelimisheni kidogo tumsaidie huyu Bwana
   
 2. Mwita25

  Mwita25 JF-Expert Member

  #2
  Nov 3, 2011
  Joined: Apr 15, 2011
  Messages: 3,840
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Tungepata ushahidi wa mshtaki kwanza ili tubalance hii story. Sawa ndugu?
   
 3. Inkoskaz

  Inkoskaz JF-Expert Member

  #3
  Nov 3, 2011
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 6,319
  Likes Received: 439
  Trophy Points: 180
  chedi avae! wapare kwa kupenda kesi bana.hapo ng'ombe atauzwa kugombea kuku
   
 4. Mkulima wa Kuku

  Mkulima wa Kuku JF-Expert Member

  #4
  Nov 3, 2011
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 1,259
  Likes Received: 81
  Trophy Points: 145
  Nasikitika kama jambo hilo ni la kweli, basi like Lowassa, like Chenge, like Rostam, like Maghembe, like makamanda wa polisi wa wilaya na mikoa vibaraka like Riziwani...orodha inaendelea. Wote ni mafisadi wanaofanya mambo watakavyo kwa manufaa yao hata kama wanaoathirika ni wengine. ni suala la muda mambo yatabadilika na ukweli utachukua mkondo wake
   
 5. MBURE JASHA

  MBURE JASHA JF-Expert Member

  #5
  Nov 3, 2011
  Joined: May 7, 2011
  Messages: 200
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Hii ni taarifa ambayo imepatikana Polisi. Ili upate ushahidi lazima wa mshtaki wa kwanza ni lazima ipande kwa mahakama kwanza. we Vipi!
   
 6. mama D

  mama D JF-Expert Member

  #6
  Nov 3, 2011
  Joined: Nov 22, 2010
  Messages: 1,755
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 145
  Movie inaendelea.............
   
 7. Kombo

  Kombo JF-Expert Member

  #7
  Nov 3, 2011
  Joined: Oct 29, 2010
  Messages: 1,819
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Dr. Mrutu anasemaje katika hili?
   
 8. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #8
  Nov 3, 2011
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,475
  Likes Received: 4,134
  Trophy Points: 280
  Lakini hiyo title ya habari yako haijatulia, si wote kuwa ni wahalifu..
   
Loading...